

































 

 

 

 

ADHABU KWA MAAJUZA KWA MISINGI YA USHIRIKINA NA UCHAWI  KATIKA  

JAMII YA ABAGUSII 

NA 

JACKLINE NJERI MURIMI, CHUO KIKUU CHA TOM MBOYA 

ABSTRACT 

Licha ya teknolojia kutoa nafasi kwa kila mmoja kuwa sehemu ya mabadiliko yanayoendelea, 
inasikitisha kuwa baadhi ya watu barani Afrika wameamua kukwamilia katika ukale na tamaduni 
hafifu zilizopitwa na wakati. Uchawi ni mojawapo ya shughuli inayotekelezwa na wanaume na 
wanawake katika desturi za jamii nyingi za kiafrika ikiwemo ile ya Abagusii nchini Kenya. Hata 
hivyo hivi karibuni kumetokea hali ambapo adhabu kali imetolewa kwa wachawi maajuza katika 
jamii ya Abagusii jambo ambalo lilipelekea kuzuka kwa ghadhabu kali kutoka kwa wananchi na 
mashirika ya umma yakikemea ubaguzi huu. Mathalan, mifano halisi ya ukale huo ni mtindo wa 
baadhi ya vijana kuwachoma na kuwashambulia maajuza kwa kisingizio cha kuendeleza uchawi 
na ushirikina. Hivyo utafiti huu ulinuia kuchanganua adhabu ya uchawi na jinsia ya kike katika 
Jamii ya Abagusii suala ambalo limeonekana kuwakera wananchi na serikali kwa ujumla. 
Ubaguzi wa jinsia ya kike wakati wa kuwaadhibu wachawi umeonekana kuzua utegano, 
mafarakano, chuki na hata kuyaweka maisha ya wanawake hawa hatarini. Hivyo basi utafiti  huu 
uliangazia utekelezaji wa adhabu kwa wachawi maajuza katika jamii ya Abagusii aidha na 
kutathmini madhara yake. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya ufeministi na uhalisia ajabu 
ambapo mihimili ya nadharia hizi ilitusaidia kufikia lengo kuu la utafiti huu. Katika kukusanya 
data mtafiti alitumia utafiti wa maktaba na ule wa mtandaoni pale ambapo data ya kimsingi 
ilipatikana kutokana na tasnifu zilizoandikwa kuhusu jamii ya Abagusii. Vilevile, utafiti wa 
nyanjani ulitumika pamoja na mbinu ya kimaelezo katika kuchambua data na kuiwasilisha kwa 
lugha ya kinathari kuambatana na malengo ya utafiti. Maarifa yaliyo katika utafiti huu yatakuwa 
mchango katika maarifa yaliyopo kuhusu masuala ya jinsia katika jamii.Zaidi ya hayo,utafiti huu 
utasaidia katika kuibua mapendekezo ambayo yatasaidia watengenezaji sera wanaojihusisha na 
suala la ubaguzi wa kijinsia dhidi ya wanawake. 
 
KEY WORDS: Adhabu, Uchawi,  Maajuza 

 

 

IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 )

Volume 06 | Issue 12 | December 2023 | http://ijojournals.com/index.php/ssh/index 10



 

 

 

1.0 Utangulizi 

Utafiti huu unachunguza adhabu inayotolewa  kwa maajuza kwa misingi  ya ushirikina na 

uchawi katika jamii ya Abagusii.Imani kuhusu uchawi na wachawi umekita mizizi nchini Kenya 

haswa katika kaunti ya kisii na bara la Afrika kwa ujumla na imani hii inaendelea kuwepo. 

Inaamika kuwa, mambo mengi yanayotendeka haswa ajali za barabarani, vifo vya watoto 

wachanga na watu wengine na magonjwa chanzo chake ni uchawi. 

Ni suala la kusikitisha mno wakati huu dunia inashuhudia mabadiliko mengi ya kiteknolojia 

ambapo ni vigumu kudhani kizazi cha sasa kinaweza kushabikia na kuendeleza baadhi ya 

tamaduni ambazo zimepitwa na wakati. Kwa mujibu wa Kamau Wanderi (2021), mabadiliko 

yanayoendelea yanapaswa kukifungua macho kizazi hiki kufahamu kuwa hakipaswi kuachwa 

nyuma dunia inapoendelea kubadilika. Inasikitisha kuwa baadhi ya vijana barani Afrika 

wameamua kukwamilia katika ukale na tamaduni dhaifu ambazo hazina maana yoyote katika 

maisha ya kisasa. Mifano halisi ya ‘ukale’ huo ni mtindo wa baadhi ya vijana kuwachoma na 

kuwashambulia wazee kwa kisingizio cha kuendeleza uchawi na ushirikina. 

Nchini Kenya katika kaunti ya Kisii maajuza ndio wanaosingiziwa kuwa wachawi zaidi na sio 

wanaume. Maajuza hawa wamekuwa wakidhulumiwa na hata kuuwawa katika jamii hii. Huku 

visa vya wazee kwa tuhuma za uchawi vikiendelea kukithiri haswa katika kaunti ya kisii, 

imebainika kuwa wanaotekeleza vitendo hivyo wanavunja sheria yenye adhabu kali. Maswali 

yanayoibuka ni: Ni vigezo vipi wanavyotumia wale wanaowashambulia wazee ili kubaini 

wanaendeleza maovu hayo? Kuna nguvu ama uwezo maalum walio nao? 

Bila shaka kitendo hiki ni cha unyama na kulingana na sheria iliyopo sasa yeyote ambaye 

atapatikana na hatia ya kumsingizia mwenzake kuwa mchawi atatozwa faini ya laki tano au 

asukumwe gerezani kwa miaka mitano. Hii ni kulingana na sheria za kuhusu uchawi sura ya 67 

ambayo pia inaharamisha vitendo vya uchawi au ushirikina. 

Kwa kauli hii, simaanishi visa na vitendo vya uchawi na ushirikina havipo. La hasha! Vipo kwa 

wingi. Hata hivyo, taratibu za kisheria zinapaswa kufuatwa kuchunguza na kubaini ikiwa ni 

kweli washukiwa wanaendesha maovu hayo au la.  

IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 )

Volume 06 | Issue 12 | December 2023 | http://ijojournals.com/index.php/ssh/index 11



 

 

Matokeoya Utafiti 

YafuatayonimawasilishoyamatokeoyamajibuyahojajikuhusumtazamowajamiiyaAbagusiikuhusua
dhabuinayotolewakwamaajuzakwatuhumazauchawinaushirikina 

Jedwali1: 
AdhabukwawachawininjiamwafakayakupunguzavitendovyauchawikatikajamiiyaAbagusii 

Kauli 5 % 4 % 3 % 2 %  1                  %           

Adhabu kwa wachawi ni njia mwafaka ya 

kupunguza vitendo vya uchawi katika jamii 

ya Abagusii 

8 9 2 2.2 1 1.1 70 78.7 8 9.0 

5-Nakubali kabisa, 4-Nakubali kiasi.  3-Nakubali,  2-Sikubali 1-Sina uhakika 

Chanzo: Ukokotozi wa mtafiti 

Kutokana na uchanganuzi wa data, watafitiwa 70 (78.7%) hawakukubaliana na maoni kuwa 

adhabu kwa wachawi ni njia mwafaka ya kupunguza vitendo vya kichawi katika jamii ya 

Abagusii huku watafitiwa 8(9.0%) wakikosa uhakika.Vilevile, idadi ndogo ya wahojiwa 8(9%) 

walikubali kabisa kuhusu madai hayo , wahojiwa 2(2.2%) wakikubali kiasi huku mhojiwa 

1(1.1%) akikubali tu. 

Hivyo basi, kutokana na matokeo ya utafiti  ni ukweli kwamba adhabu ya uchawi  haipunguzi 

vitendo vya kichawi katika jamii ya Abagusii mbali ni vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake 

wazee.Tabia hii ya kishenzi na ukatili kawaida huidhinishwa na baadhi ya wanajamii ambapo 

vitendo hivi vimekithiri.Kutokana na data tuliyokusanya, wanafamilia wa maajuza hawa 

hushirikiana kuanzisha vurugu dhidi ya wanawake na hata mauaji ya maajuza hawa.Vilevile, 

adhabu hii husababisha familia za maajuza hawa kutengwa na jamii na uharibifu wa mali pale 

ambapo adhabu inahusisha kuchomwa kwa maajuza hawa pamoja na mali yao. 

Utekelezaji wa Adhabu kwa Wachawi Maajuza katika Jamii ya Abagusii 
Katika jamii ya Abagusii adhabu kwa maajuza watuhumiwa wa uchawi hutekelezwa kwa njia 

mbalimbali. Kama tulivyoshuhudia katika vyombo vya habari kumekuwapo na adhabu ya papo 

kwa hapo ya watuhumiwa wa uchawi. Hali hii ni tofauti na ilivyokuwa katika historia na 

utamaduni ambapo washukiwa walipitia aina fulani za majaribio yaliyolenga kuthibitisha tuhuma 

zozote dhidi yao kabla ya kuadhibiwa.Ni baada  tu ya majaribio haya  ndipo ambapo 

waliopatikana na hatia walipata adhabu yao. Isitoshe  hali hii si ya kipekee katika jamii hii ya 

IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 )

Volume 06 | Issue 12 | December 2023 | http://ijojournals.com/index.php/ssh/index 12



 

 

kiafrika kwani tunaona hali kama hii ikitokea ulimwenguni ambapo mashtaka ya uhalifu wa 

uchawi yalifikia kiwango cha juu kutoka mwaka wa 1580 hadi 1630. Katika wakati wa 

kupambana na marekebisho ya vita vya dini ya Ulaya, wakati takriban watu elfu hamsini 

waliuawa, na baadhi ya maeneo yakichomwa ambapo takriban asilimia themanini ya 

waliochomwa walikuwa wanawake waliokuwa na umri zaidi ya miaka arobaini. 

Aidha kulikuwa na njia ainati Kihistoria  za kwaadhibu washutumiwa wa uchawi auwale 

waliopatikana  wakishiriki uchawi. Miongoni mwa adhabu hizo ni ile ya kifo, wengine 

kuchomwa,kunyongwa na hata kukatwa kichwa. Tukirejelea jamii ya Abagusii, tunapata kuwa  

miongoni mwa njiambalimbali zilizotumika katika kuwaadhibu wachawi ni kama ilivyoelezwa 

katika sehemu ifuatayo. 

i) Uingizaji wa Vifaa Vyenye Ncha Kali katika Sehemu za Siri za Watuhumiwa 
Mojawapo ya aina kali ya adhabu ya uchawi ni jaribu linalohusisha kuingiza vifaa vyenye ncha 

kali kwenye sehemu za siri za washukiwa.Mbali na ukali wake, aina hii ya adhabu inasemwa 

kuwa ya kufedhehesha sana.Utekelezaji wake unahusisha kuingizwa kwa kitu chenye ncha kali, 

hasa kijiti chenye umbo la mshale ndani ya sehemu za siri za mwathiriwa.Kifaa hiki kinaweza 

kuondolewa tu kwa njia ya upasuaji.Kutokana na namna ambayo adhabu hii inatekelezwa, 

wahasiriwa wa adhabu hii ni nadra sana kuishi . 

Washukiwa wa kiume pia wanaweza kuadhibiwa kwa njia hii pia pale ambapo vifaa vyenye ncha 

kali huingizwa kwenye sehemu zao za siri.Njia hii inafedhehesha zaidi wakati inahusisha kiungo 

cha uzazi cha mwanamke.Licha ya umuhimu wa kiungo hiki cha uzazi cha mwanamke katika 

kufanya mapenzi na kuendeleza ukoo na familia, kwa njia zingine uke hupewa mtazamo hasi. 

Miongoni mwa Abagusii ni mwiko kuitaja ile sehemu ya siri ya mwanamke (embere) hasa 

hadharani ikilinganishwa na ile ya mwanamume jambo ambalo linaweza kusemwa kuwa 

linajumuisha ubaguzi wa kijinsia dhidi ya wanawake.Kwa hivyo,adhabu ya kuingiza kifaa 

chenye ncha kali katika uke wakati wa kuadhibiwa kwa mchawi inaonyesha jinsi wanaume 

wanavyowaona wake zao kama viumbe duni.Kama aina nyingine ya adhabu wanazozipokea 

wanawake kwa madai ya uchawi, adhabu hii inajumuisha ubaguzi wa jinsia dhidi ya wanawake. 

Kwa muda mrefu sasa, inaonekana kuwa adhabu ya uchawi katika jamii ya Abagusii inaonyesha 

kuwa kuna misukosuko katika mahusiano kati ya jinsia ya kike na ile ya kiume pale ambapo 

IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 )

Volume 06 | Issue 12 | December 2023 | http://ijojournals.com/index.php/ssh/index 13



 

 

jinsia ya kiume imependelewa sana.Kwa kweli, inaweza kusemwa kuwa, kuna mitazamo potovu 

kuhusu jinsia ya kike na hivyo basi majaribio ya uchawi ni njia tu ya kulazimisha mfumodume. 

Kulingana na wahojiwa wetu, jamii ya Abagusii huwachukulia wanawake kama watu ambao kila 

wakati wanasafiri (abaeti).Jambo hili linamaanisha kwamba,wawe katika nyumba za wazazi wao 

au katika ndoa, hawana makazi maalumu.Vilevile wanapoozwa na kwenda katika nyumba zao za 

ndoa,hubeba jina la wageni(abarwa isiko).Jina hili hutumiwa  kuonyesha kuwa, mwanamke ni 

mpita njia tu na kama watu wengine ambao hawahusiani na jamii ile, wanawake hawa hawapewi 

haki sawa na wenzao wa kiume. 

Kwa jumla, wanawake wa Abagusii huchukuliwa kuwa viumbe dhaifu na hali hii ya 

kuwakumbushwa kila wakati kwamba wao si sawa na wanaume imewafanya kujidumaza.Kwa 

hivyo, dhuluma mbalimbali zinapofanywa dhidi yao, ni vigumu sana kuinua sauti zao 

kulalamika. 

i)  Wachawi Kuchomwa 
Kuwepo kwa wachawi bado ni imani ya kijamii inayoendeshwa na wazo ambalo limechukuliwa 

kuwa la kawaida katika jamii za Kiafrika na jamii kadha nchini Kenya.Imani hizi za uchawi 

zimechochea adhabu kali ya wanaoshukiwa kuwa wachawi.Hivyo basi kuchomwa kwa kwa watu 

wanaoshukiwa kuwa wachawi katika jamii ya Abagusii ni jambo la kawida sana ambapo kesi 

hizi huripotiwa kwenye vyombo vya habari.Serikali imeweka juhudi nyingi hili kuzuia mauaji 

haya ya watuhumiwa wa uchawi ila haijafua dafu.Ingawa kitendo hiki cha kuwachoma watu kwa 

madai ya uchawi ni kitendo cha ukatili ambacho kinapaswa kuwa kimelaaniwa na jamii, hakuna 

suluhu yoyote imepatikana hadi sasa ili kukomesha kitendo hiki 

Wimbi jipya la mashambulizi dhidi ya maajuza wanaoshukiwa kuwa wachawi katika kaunti ya 

Kisii limezua wasisiwasi katika eneo hili.Katika vyombo vya habari ni dhahiri kuwa maajuza 

huteketezwa kila kuchapo.Wauaji wao hudai kuwa maajuza hao hushiriki uchawi.Uchomaji wa 

wachawi hutumika kama njia ya kulipiza kisasi dhidi ya wanawake wazee jambo ambalo 

linaonekana kuleta vurugu. 

Kulingana na habari kutoka gazeti la taifa leo,mnamo Januari 14,wanawake wawili wazee 

walichomwa kiasi cha kutotambulika katika kijiji cha Omokonge,Kaunti ya Nyamira, kwa 

tuhuma za uchawi.Pauline Mogambi,95, na bintiye Rose Mogambi,53, waliuawa na wanakijiji 

IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 )

Volume 06 | Issue 12 | December 2023 | http://ijojournals.com/index.php/ssh/index 14



 

 

wenye hasira.Nyumba nane za watu wanaodaiwa kuwa wachawi pia zilichomwa moto.Baadhi ya 

watu ambao huchomwa wanaweza kuwa hawana hatia.Adhabu hii ni haramu kwani inamnyima 

mshukiwa haki ya kuishi. 

Ingawa wanaume na wanawake hujihusisha katika shughuli za uchawi, kesi zilizoripotiwa 

kwenye vyombo vya habari zinaonyesha asilimia kubwa ya waathiriwa ni wanawake.Mfumo wa 

jamii ya Abagusii kimsingi ni mfumodume.Wanaume tofauti na wanawake ni watu 

wanaoaminika kuwa wa kudumu katika jamii.Ingawa wanawake wanaweza kuonekana kuwa 

watu wa jamii au ukoo ule kwa sababu ya kuzaa watoto, mara nyingi wanachukuliwa kuwa watu 

wasio na uhusiano wa moja kwa moja na jamii ile kwa sababu hawana uhusiano wa damu na 

jamaa zao wa ndoa.Hivyo basi, wakati mwanamume ameshukiwa kufanya uchawi, ukoo 

unaweza kuzuiwa kumuua mwanamume yule kwa vikwazo vya uhusiano wa damu na hofu ya 

kumwaga damu ya jamaa yao. 

Kutokana na utafiti huu,shutuma za uchawi zinazosababisha uteketezaji wa maajuza 

wanaoshukiwa kuwa wachawi ni tabia ya kishenzi ambayo huidhinishwa na baadhi ya wanajamii 

ambapo vitendo hivi vimekithiri.Mauaji haya ambayo yamekuwa yakitokea Kisii kwa miongo 

mingi si mila au desturi za kitamaduni za watu wa Abagusii mbali ni vitendo vya ukatili 

uliokithiri vinavyochochewa na uchoyo, ubinafsi,chuki dhidi ya wanawake na dhana na maadili 

ya  mfumo wa ubabedume ambao unashusha thamani maisha ya wanawake. 

ii)  Wachawi Kufukuzwa Kutoka Koo Zao 
Adhabu hii uhusisha kutengwa kwa mtu au watu kutoka kwa kikundi fulani cha watu au 

jamii.Adhabu hii hutokea kutokana na ukweli kwamba mtu au watu wamekiuka sharia za 

kikundi Fulani au jamii hiyo.Kutoroshwa Katika jamii basi ni aina ya adhabu apatayo mtu 

aendeapo kinyume na matarajio ya jamii yao.Miongoni mwa Abagusii, washukiwa wa uchawi 

hulazimishwa kutoka Katika koo zao au hata jamii zao.Mara tu wanapofukuzwa kutoka koo zao, 

wao huwa kama wale watu waliougua ugonjwa wa ukoma katika Biblia kwa maana kwamba 

hakuna  mwanajamii angetaka kuonekana akishirikiana nao. 

Watu hawa wanapotengwa na wanajamii inakuwa vigumu kushirikiana na wezao hivyo 

inawalazimu kuondoka kwa hiari yao wenyewe kwa sababu ya hisia za kukataliwa.Watu hawa 

huishia na kukaa katika vijiji au koo za kigeni ambapo shughuli zao  hazijulikani.Jambo hili 

limetumika kama mojawapo ya sababu zinazoelezea ni kwa nini tunapata watu wengi kwa kijiji 

IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 )

Volume 06 | Issue 12 | December 2023 | http://ijojournals.com/index.php/ssh/index 15



 

 

kimoja ambao hawana nasaba zinazofanana.Watu hawa kwa kawaida huitwa ‘Abamenyi’.Iwapo 

badaye kuna ushahidi wa kutosha kwamba wamerekebisha tabia zao, wanaweza kuruhusiwa 

kurudi kwenye jamii yao. 

Hata hivyo, hali hii huweza kuwa tofauti pale ambapo mshukiwa anayefukuzwa hutokea kuwa 

mwanamke.Mwanamke aliyetengwa na jamii, mara nyingi harudi katika boma ya wazaziwe 

mbali huchagua kuoleka katika jamii nyingine.Imani za uchawi miongoni mwa Abagusii ni 

sababu mojawapo ilitumika kueleza kwa nini wanawake wa jamii ya Abagusii wameoleka katika 

jamii jirani kama vile wajaluo, wakipsigis na wamaasai. 

Ni muhimu kutambua kwamba Abagusii kama jamii nyingine za Kiafrika hutawaliwa na mfumo 

dume.Kwa hivyo, kumfukuza mwanamume kutoka jamii yake kuliaminika kuleta upungufu wa 

idadi ya watu katika ukoo huo haswa kama bado hao wanaume wana uwezo wa kuzalisha 

watoto.Kwa hivyo, jamii haingemwadhibu vikali mwanamume aliyeshukiwa kuwa mchawi 

kwani walipoomba msamaha waliweza kupewa faini nyepesi na kusamehewa kwa onyo la 

kutojihusisha tena na uovu huo. 

Mara kwa mara, wanaume wanaoshukiwa kuwa wachawi wanaweza kuwanyooshea kidole wake 

zao kwa lawama za kuwafundisha au kuwapa uchawi(kobaa rirogio) ambapo mwanamke huyo 

alilazimika kubeba hasira za wanajamii (Nyagaka Moraa).Kwa kweli, wanaume walipata 

msamaha ikiwa wangetangaza hadharani kwamba wake zao waliwaathiri kwa kuwafanyia 

uchawi. 

Katika tukio ambalo lilihusisha mwanamke kufukuzwa kutoka kwa nyumba yake kwa tuhuma za 

uchawi, hakuna hisia kali ya hasara inahisiwa ikilinganishwa na kumfukuza mwanamume 

ambaye anaonekana kama mzalishaji mali katika jamii.Mtazamo kwamba wanawake ni viumbe 

dhaifu na wanyenyekevu hufanya iwe rahisi kwao kufukuzwa. 

Katika jamii hii ya Abagusii, wanawake wanaoshutumiwa kwa uchawi hutoroshwa  kutoka kwa 

familia zao na kupelekwa katika ‘kijiji cha wachawi’ambacho wakisii huita ‘Egetii kia 

Abarogi’.Wanawake pekee ndio hutoroshwa kwa sababu wao huonekana kama viumbe dhaifu 

ambao hawawezi kuzitetea haki zao.Ubaguzi unaopelekea kufukuzwa miongoni mwa Abagusii, 

ni ubaguzi wa kijinsia dhidi ya wanawake.Hii kimsingi inatokana na dhana kwamba wanawake 

IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 )

Volume 06 | Issue 12 | December 2023 | http://ijojournals.com/index.php/ssh/index 16



 

 

huoleka kutoka ukoo mmoja kwenda mwingine na hivyo, ukoo utapoteza kidogo sana kwa 

kuwafukuza. 

 

 Madhara Yanayotokana na Adhabu Wanazopokea Maajuza, Washutumiwa wa Uchawi 

Adhabu ya uchawi kwa maajuza wanaoshutumiwa yana athari mbaya si haba kwa mtuhumiwa 

na jamii kwa ujumla (Sambe 2017;Asamoah Gyadu 2015).Madhara haya yanaweza kuwa ya 

kijamii na kiuchumi na pia yanayoathiri maendeleo ya mtu binafsi kama ilivyofafanuliwa katika 

sehemu ifuatayo. 

i)  Athari za Kijamii Zinazotokana na Adhabu ya Uchawi kwa Jnsia ya Kike 
Maajuza wanaotuhumiwa kuwa wachawi,haki zao za binadamu hukiukwa pakubwa.Kulingana 

na Igwe(2013) ukiukaji wa haki za binadamu ni silaha ya madaraka na utaratibu wa 

ukandamizaji wa wanawake walio katika nyadhifa dhaifu za kitamaduni katika 

jamii.Unyanyasaji humfanya aliyeshutumiwa kutengwa na wezake katika jamii 

anamoishi.Unyanyapaa hudumaza na kuzuia maendeleo ya kijamii na vilevile ya wanawake 

kwani wao hudharauliwa na watu wa familia zao. 

Katika maeneo na nyanja ambazo uchawi unaaminika kurithiwa, husababisha unyanyapaa zaidi 

kwa watoto wa mtuhumiwa.Watoto hawa hupokea dhihaka kutoka kwa wanajamii kuwa wao ni 

watoto wa mchawi na hata kuendeleza uchawi(Quarmyne 2011).Matokeo ya utafiti na pia 

mahojiano na wanawake ulidhibitisha madhara haya katika maisha ya walioshutumiwa pamoja 

na watoto wao. Mmoja wa wanawake aliyehojiwa alisema kuwa;’kifo cha ghafla cha mtoto wa 

pekee wa mwenzangu wa nyumbani kililaumiwa juu yangu’. Jambo ambalo lilisababisha 

unyanyapaa kwake na hata kwa watoto wake. 

Matokeo ya utafiti huu ilionyesha kwamba adhabu ya uchawi husababisha kifo.Kutokana na 

ukosefu wa taratibu sahihi na chanya za kuwaadhibu wanaoshtumiwa kuwa wachawi wananchi 

huchukua sheria mkononi jambo ambalo limesababisha kuuwawa kwa watuhumiwa kama 

inavyoripotiwa katika vyombo vya habari.Njia hii ya kuwaadhibu wachawi husababisha matatizo 

ya kisaikolojia kwa wanafamilia wanaoshuhudia kitendo hiki kikitendewa mmoja wao. 

Adhabu ya uchawi hufanya washutumiwa kukabiliwa na ukiukaji wa haki ambazo zinaanzia haki 

ya kuwa huru kutokana na unyanyasaji, haki ya kupata chakula, haki ya kuheshimu maoni ya 

IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 )

Volume 06 | Issue 12 | December 2023 | http://ijojournals.com/index.php/ssh/index 17



 

 

maajuza wanaotuhumiwa kuwa wachawi, haki ya malazi na kulindwa(Foxcroft na 

Secker,2010).Maajuza hawa hukabiliwa na kifungo na kulazimishwa kushiriki katika sherehe za 

kufukuza pepo walio ndani yao jambo ambalo linawaaharibu kisaikolojia.Kushindwa kwa 

serikali kutoa huduma mbadala za utunzaji kwa wale wanaotuhumiwa kwa shughuli za uchawi ni 

ukiukaji wa haki zao za kuhudumiwa au kulindwa 

Zaidi ya hayo, adhabu ya uchawi huwafanya watuhumiwa kutelekezwa na watoto wao wenyewe, 

familia na wanajamii.Jambo hili linawafanya kutopata huduma za kijamii(Monyenye 

1997).Maajuza wengi walioshutumiwa kuwa wachawi wamekimbilia maeneo ya mjini ili 

kuepuka kutendewa mabaya zaidi.Jambo hili limewasababishia matatizo makubwa ya afya ya 

akili katika kujaribu kukabiliana na ulimwengu sambamba na usasa.(Di Domenico,1982). 

Vilevile, shutuma za uchawi husababisha kusambaratika kwa familia.Kwa vile watuhumiwa 

wengi wa uchawi ni wanawake,wengi wao uhama vitongoji vyao ili kuepuka adhabu kali na ata 

kifo.Katika hali hiyo, watuhumiwa hawa huweza kupoteza watoto wao na waume zao huweza 

kuwataliki ili kuepuka hofu ya kutambuliwa kama washiriki wa uchawi(Monyenye 

1977).Hakika, kulingana na washiriki wetu, hii inaweza kueleza kuwepo kwa idadi kubwa ya 

wanawake waliotalikiwa na waume zao. 

Zaidi ya hayo, mahusiano baina ya majirani na wanajamii humomonyoka.Hii ni kwa sababu 

uchawi huonekana kuleta madhara kwa watu wengine katika jamii.Kama ilivyobainishwa na 

Asamoah Gyadu(2015) majirani na marafiki humshuku na kumtuhumu kila mmoja wakati 

wanaposhindwa kuiendeleza maisha yao jambo ambalo huvuruga maisha na uhusiano mwema 

kati ya marafiki na jamaa. 

ii) Athari za Kiuchumi Zinazotokana na Adhabu ya Uchawi 
Athari kadhaa za uchawi zinapatikana kutokana na adhabu ya uchawi kwa maajuza Katika jamii 

ya Abagusii.Ikizingatiwa kuwa wanawake wanaoadhibiwa kwa madai ya uchawi 

hunyanyapaliwa na kubaguliwa ambapo maendeleo yao ya kiuchumi na hadhi yao huathiriwa 

vibaya. 

Katika baadhi ya matukio, watuhumiwa wa uchawi hulazimika kuhama makazi yao na kuacha 

mali zao nyuma na hata katika hali mbaya vitu vyao huchomwa na kuharibiwa(Dovlo 

2007).Katika matukio mengine, mali binafsi ya watuhumiwa hutwaliwa na washtaki wao na 

IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 )

Volume 06 | Issue 12 | December 2023 | http://ijojournals.com/index.php/ssh/index 18



 

 

jamaa wengine wanaounga mkono mashtaka hayo.Jambo hili hurudisha nyuma maendeleo ya 

kiuchumi ya wanawake hawa na watoto wao na kuwafanya kuwa maskini maishani 

mwao.Ilibainishwa na mwanamke wakati wa mahojiano kuwa;’Baada ya kushtakiwa kwa 

kumuua mtoto wa jirani yangu, nilidharauliwa na wanajamii kisha nikapoteza njia yangu ya 

mapato na biashara ndogo ndogo ambayo nilikuwa nikifanya kwa sababu watu walikataa 

kuninunulia kwa vile waliniona mchawi, hii ilisababisha kuhama kwangu’.Kutokana na hili, 

inaweza kuonekana kuwa watuhumiwa wamewekwa katika hali ya kupoteza hadhi yao ya 

kiuchumi na njia zao za kujikimu kimaisha. 

 

Hitimisho 

Kwa ujumla, adhabu ya uchawi ina athari mbaya kwa ustawi miongoni mwa Abagusii.Kwa 

upande wa jinsia ni muhimu kutambua kuwa miongoni mwa Abagusii wanawake wanajumuisha 

asilimia kubwa ya uzalishaji mali.Kwa hivyo, kuwanyima kazi kupitia adhabu ya uchawi 

inapunguza kasi ya ukuaji wa uchumi na maendeleo 

Kutokana na utafiti huu inaonekana kwamba, adhabu ya uchawi husababisha pengo la kiuchumi 

pale ambapo rasilimali na watu ambao wanaendeleza biashara hupotea.Inabainika kwamba 

washutumiwa pamoja na familia zao hutia kikomo katika shughuli zao za biashara jambo ambalo 

linadunisha maendeleo ya uchumi katika jamii. 

Aidha, kutokana na utafiti ilibainika kuwa,adhabu ya uchawi inarudisha nyuma na kuathiri 

vibaya tija ya kiuchumi.Hii ni kwa sababu katika mazingira mengi ya kifamilia na maisha ya 

kijamii, wanawake wazee huchukua jukumu la kuwalea wajukuu wao jambo ambalo linaruhusu 

kizazi kipya kujihusisha na shughuli za kiuchumi ambazo zinawezesha uzalishaji na mapato ya 

familia(Eboiyehi 2017).Hata hivyo, kwa tuhuma zilizopo maajuza wanalazimishwa kuondoka 

kwao nyumbani na pia katika jamii na kuacha pengo kubwa katika tija ya kijamii na 

kiuchumi.Hili lilithibitishwa na mwanamke mmoja katika mahojiano, ‘Nilipotuhumiwa kuwa 

mchawi na kaka wa marehemu mume wangu na baadhi ya wanafamilia yao, ilinibidi kuondoka 

nyumbani na kumuacha binti yangu mkubwa akimlea na kumtunza mtoto wake peke yake’. 

Utafiti pia umeonyesha kuwa miongoni mwa Abagusii, wanawake wana jukumu muhimu katika 

uzalishaji wa mali.Hakika wanawake ndio wanaojishughulisha zaidi kuliko wanaume kwa ajili 

IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 )

Volume 06 | Issue 12 | December 2023 | http://ijojournals.com/index.php/ssh/index 19



 

 

ya kujikimu kimaisha.Kwa hivyo, kuwanyima haki ya kujishughulisha za mambo ya kijamii kwa 

njia ya kuwaadhibu, kunainyang’anya jamii nguzo yake ya uzalishaji wa kiuchumi.Kwa hivyo 

miongoni mwa Abagusii, kuondolewa kwa wanawake katika jamii kwa madai ya uchawi 

husababisha hasara kubwa. 

Utafiti huu pia umeonyesha kwamba umiliki wa mali miongoni mwa Abagusii unahusishwa na 

wanaume mbali si wanawake.Kwa hivyo, ikiwa mwanamke atajihusisha na uzalishaji wa mali 

yoyote hawezi kudai umiliki.Hivyo, wanawake wanaozalisha mali kisha kudai umiliki 

wanadharauliwa na jamii.Wanaonekana kuwa sio wa kawaida kisha kuitwa wachawi.Hivyo 

basi,wanawake wengi wa Abagusii huondoka kwa hofu ya kuadhibiwa.Kimsingi, jambo hili 

linaua ile hamu ya kuzalisha mali miongoni mwa wanawake wa jamii ya Abagusii.Kwa upande 

wa jinsia inabainika kuwa wanawake ni wazalishaji mali na basi adhabu ya uchawi inapunguza 

kasi ya ukuaji wa uchumi na maendeleo kwa ujumla 

 

MAREJELEO 
 

Acton, H. B. ed., 1961. The philosophy of Punishment. London: Macmillan. 

Adegbola, A.A.E.ED.., 1983. Traditional Religion in West Africa. Ibadan: Daystar Press. 

Akama, S. et. at (2006).Ethnography of the Gusii of Western Kenya.The Edwin Millen 

Press.New York. Akawa and Kadayi (2006). 

Alan Macfarlane, witchcraft in Tudor and Stuart England, Psychology Press, 1999. 

Ashforth, Adam (2000). Madumo, A Man Bewitched. University of Chicago Press. 

Awolalu et.al. 1979. Yoruba Beliefs and Sacrificial Rites. London: Longman. 

Bahemuka, J (1982). Our Religious Heritage.Nairobi. Thomas Nelson and Sons Ltd. 

Bogonko, S (1977). Christian Missionary Education and its Impact on the Abagusii of Western 

Kenya 1909-1963 Nairobi Kenya 

Crawford, J. R. 1967. Witchcraft and Sorcery in Rhodesia.London: OxfordUniversity Press. 

Beauchamp, T. 1982. Philosophical Ethics: An introduction to Moral Philosophy. New York: 

Mc Craw-Hill Publishing Co. 

Behringer, W.2004. Witches and witch-Hunts.A Global History. Malden Massachusetts: 

Polity Press. 

IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 )

Volume 06 | Issue 12 | December 2023 | http://ijojournals.com/index.php/ssh/index 20



 

 

Bever, E (2002). “Witchcraft, Female Aggression and Power in the Early Modern 

Community’’. In Journal of Social History. 

Brooke, E. 1993. Women Healers through History. London: Women’s Press Ltd. 

Bryman, A. (2001).Social Research Methods.New York: Oxford University Press. 

Carlo, J.B. 1965. The World of witches.Glendinning: The University of Chicago Press. 

Crawford, J. R. 1967. Witchcraft and Sorcery in Rhodesia.London: OxfordUniversity Press. 

Cole, D.H. 1955. On the Origin of Equality. Chicago: the Great Books Foundations. 

Daniel A. Offiong. Witchcraft, Sorcery, Magic, Social order among the Ibibio of Nigeria. 

Evans-Prichard, E.E. 1937. Witchcraft, Oracles and Magic among the Azande. Oxford: Oxford 

Favret-Saada, Jeannne (December 1980). Deadly words: Witchraftin the Bocage. Cambridge 

University Press. 

Federici, S. (2004). Caliban and the Witch. Autonomedia. 

Federici, S. (2018). Witches, witch-hunting, and women. PM Press. 

Frankena, K.W. 1989. Ethics. New Delhi: Prentice Hall of India Private Ltd. 

 

Gaskil, M. 1998. “The Devil in the Shape of a Man: Witchcraft, Conflict and Belief in 

Jacobean England’’.In Historical Research. 

Gehman, J.R. 1989. African Traditional Religion in Biblical Perspective. Nairobi: 

Kesho Publications. 

Gibblin, J. 2002. “The Criminalization of Witchcraft and the Politics of Chieftainship: A 

history of Unyambuda in Uwanji, Southern Tanzania’’. In Crime in EastAfrica: Past and 

Present perspectives. Naivasha: The British Institute of Eastern Africa. 

HAYES s (1995). Christians Response to witchcraft and Society in Missionalia, vol.23(3 

November. 

 Holmes, R (1974) witchcraft in British History.London. Fredrick Miller Ltd. 

Hutton, Ronald (1999) The Triumph of the Moon: A History of Modern Pagan Witchcraft, 

Oxford, OUP. 

Julia, A. 1976. Plato’s Republic and Feminism. New York: Viking. 

Keeling, M. 1970. Morals in a Free Society. London: SCM Press Ltd. 

Kirby, J. (1994). „Cultural Change and Religious Conversion in West Africa‟, in T.D. Blakely et 

al, eds,.Religion in Africa.Experience and Expression,London, James Currey. 

IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 )

Volume 06 | Issue 12 | December 2023 | http://ijojournals.com/index.php/ssh/index 21



 

 

Kothari, R. C. (2004). Research Methodology: Methods and Techniques, New Delhi: New age 

International (P) Limited Publishers.  

Kothari, R. C (2008). Research Methodology: Methods and Techniques, New Delh: New age 

International Publishing Ltd. 

Levack, Brian P.ed.(2013) The Oxford Handbook of Witchcraft in Early Modern Europe and 

Colonial America. 

Mayer, U. P. (1954) Witches Grahamstown: Rhodes Univ.,Inaugural Lecture. 

Magesa, Laurenti, 1997; African Religion: the Moral Traditions of Abundant Life; Pauline 

publications Africa, Nairobi. 

 Marwick, M.G. 1982. Witchcraft and Sorcery.Harmondsworth: Penguin Books. 

Murimi J.N (2010) Uchanganuzi wa Maoni Andishi ya Walimu wa Kiswahili kwenye insha za 

Wanafunzi katika Shule za Upili Wilayani Transzoia Magharibi.(Tasnifu ya Uzamili) 

Haijachapishwa. 

Ndeti K. (1972). The element of Akamba life.Nairobi East Africa Printing House  

Nthamburi, Z. (1991). From Mission to Church – A handbook of Christianity in East 

Africa.Uzima Press- Nairobi. 

Njogu, K. na Chimera, R. (1999). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na 

Mbinu. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation. 

Offiong, D.A. 1991. Witchcraft, Sorcery, Magic and Social Order among the Ibibio of 

Nigeria.Enugu, Nigeria: Dimension Publishing Co. 

Parrinder G. (1963) Witchcraft: European and African. London: Feber and Faber.  

Parrinder, G. 1963. Witchcraft: European and African. London: Faber and Faber. 

Ranger, T. (1978) „Protestant Missions in Africa: the Dialectic of Conversion in the AMEC in 

Eastern Zimbabwe, 1900-1950‟, in Religion in Africa.  

Ranger, T. (1980).„Introduction‟.Themes in the Christian History of Central Africa. Temples P. 

(1959) Borton Philosophy Paris: Presence African. 

Tinga, K.K., (1998). Cultural Practice of the Mijikenda at Cross roads: Divination, Healing 

Witchcraft and the Statutory Law. AAP. 

Thomson, J.J. 1994. “Goodness and Utilitarianism”. Proceedings and Addresses of the 

American Philosophical Association,67 (4):7-21 

TUKI, (2004), Kamusi ya Kiswahili Sanifu: Oxford University Press.  

IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 )

Volume 06 | Issue 12 | December 2023 | http://ijojournals.com/index.php/ssh/index 22



 

 

TUKI, (2013), Kamusi ya Kiswahili Sanifu (toleo la 3) Nairobi: Oxford University Press. 

Wamitila, K. (2008). Kazi ya Fasihi: Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi. 

Nairobi: Vide~Muwa Publishers. 

Wagner, G. 1970. The Bantu of Western Kenya. London: Oxford University Press. 

Walker, R. 1978 Kant: The Argument of Philosophers. London: Routledge and Kegan Paul. 

Wanyeki, L. Muthoni ed. (2003). Women and Land in Africa: Culture, Religion and Realizing 

Womenn’s Rights.London:Zed Books, 2003. 

Winker, G. and Degele, N. (2011). Intersectionality as Multi-Level Analysis: Dealing with 

Social Inequality, European Journal of Women’s Studies 18(1):51-66 

Women International League for Peace and Freedom (2017). Outcome of CEDAW Review of 

Nigeria-More Action Needed to Implement the WPS Agebda WILPF. 

 

 

 

IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 )

Volume 06 | Issue 12 | December 2023 | http://ijojournals.com/index.php/ssh/index 23


	ABSTRACT
	1.0 Utangulizi
	Utekelezaji wa Adhabu kwa Wachawi Maajuza katika Jamii ya Abagusii
	i) Uingizaji wa Vifaa Vyenye Ncha Kali katika Sehemu za Siri za Watuhumiwa
	i) Wachawi Kuchomwa

	ii) Wachawi Kufukuzwa Kutoka Koo Zao
	i) Athari za Kijamii Zinazotokana na Adhabu ya Uchawi kwa Jnsia ya Kike
	ii) Athari za Kiuchumi Zinazotokana na Adhabu ya Uchawi

	MAREJELEO

