

































IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI 

 

 

 

 

UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA 
CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI 

 

Jackline Njeri Murimi, Chuo Kikuu cha Tom Mboya 
na 

Jude Muli Mukuta, Chuo Kikuu cha Mount Kenya 

 

IKISIRI 
Masuala ibuka ni mambo yanayoangaziwa na kupewa kipau mbele katika jamii ya leo na 
aghalabu yalipuuzwa katika miaka ya zamani. Fasihi kama zao la wakati hubadilika jinsi jamii 
inavyobadilika ili iyamulike masuala mapya yanayoibuka katika jamii husika. Masuala haya ni 
pamoja na usawa katika jamii, haki za binadamu na mengine mengi. Utafiti huu umelenga 
kuonyesha jinsi haki za watoto zinavyokiukwa katika fasihi kupitia riwaya mbili teule ambazo 
ni:Chozi la Heri (2017) ya Assumpta K.Matei na Nguu za jadi (2021) ya Clara Momanyi. Ili 
kukamilisha lengo hili kuu, malengo mahususi matatu yalizingatiwa.Malengo hayo ni pamoja na; 
Kujadili jinsi ukiukaji wa haki za watoto unavyojitokeza katika riwaya teule,kutathmini madhara 
yanayotokana na ukiukaji wa haki za watoto katika riwaya teule na kuchanganua njia mbadala 
zinazoweza kutumika ili kuondoa ukiukaji wa haki za watoto katika jamii. Utafiti huu 
uliongozwa na nadharia ya uhalisia ambapo mihimili ya nadharia hii ilitusaidia kufikia malengo 
ya utafiti huu.Utafiti huu ulichukua muundo wa kimaelezo. Data ilikusanywa kule maktabani 
pale ambapo riwaya teule zilisomwa pamoja na tasnifu mbalimbali ili kurutubisha utafiti. Data 
ilichanganuliwa kwa njia ya kimaelezo kwa kuzingatia malengo na maswali ya utafiti pamoja na 
nadharia ya uhalisia.Uteuzi wa kimakusudi ulitumika katika utafiti huu kuteua riwaya ya Chozi 
la Heri na Nguu za Jadi. Utafiti huu utasaidia katika kuibua mapendekezo ambayo yatasaidia 
watengenezaji sera wanaojihusisha na suala la ukiukaji wa haki dhidi ya watoto,vilevile,utafiti 
huu utakuwa na mchango mkubwa katika taaluma ya elimu kwani utaihamasisha jamii kuhusu 
dhima ya fasihi ikiwemo kuyamulika matatizo yanayotokea katika jamii na kuyatafutia suluhu. 
Zaidi ya hayo, utafiti huu utawanufaisha waandishi wa kazi za fasihi kwani utawasaidia katika 
kutambua masuala nyeti katika jamii na namna ya kuyatatua. 

 

Usuli wa mada 
Fasihi ni sanaa inayotumia lugha kwa ubunifu wa juu ili kuelezea ujuzi wa viwango mbalimbali 
vya wanajamii anamoishi msanii. Njogu na Chimerah (1999),wanadai kwamba,kazi za fasihi 
huwasilisha mivutano, mikinzano, hali na maingiliano mbalimbali ya maisha ya mwanadamu na 
mazingira anamoishi. Msanii yeyote wa kazi ya fasihi huchota jumla ya mawazo  anayotaka 
kuangazia kulingana na  hali halisi za kisasa zinazomzunguka kiteknolojia,kiuchumi na 
kitamaduni.Ni kupitia kazi hizi  ambapo tunapata taswira kamili ya jamii.Kwa jumla,fasihi kama 
sanaa ni zao halisi la jamii na haiwezi ibuka kutoka ombwe tupu.Masuala yanayoibuliwa katika 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May  2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 1



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI 

 

 

 

 

Chozi la Heri ya Assumpta K. Matei na katika Nguu za jadi ya Clara Momanyi haswa suala la 
ukiukaji wa haki dhidi ya watoto ni taswira kamili ya jamii ya kisasa. 

Hunt (1994) anaeleza kuwa mtoto ni kiumbe ambaye bado hajakomaa kiakili na umri wake upo 
chini ya miaka kumi na minane.Mtoto anafaa kulindwa dhidi ya dhuluma za aina 
yoyote.Kulingana na katiba ya Kenya (2010) mtoto ni mwanadamu yeyote aliye na umri wa 
chini ya miaka kumi na minane.Vilevile,Shirika la Afya Duniani (WHO) linamsawiri mtoto 
kama mtu ambaye umri wake uko chini ya miaka kumi na tisa. 

Kila mtoto, bila kujali umri wake,rangi,jinsia au mahali alipozaliwa ana haki.Haki hizi 
zimewekwa katika sheria za kimataifa katika mkataba wa haki za mtoto (CRC).Mkataba huu 
unatambua kwamba watoto wote lazima watendewe haki kwa usawa na kwa utu.Sheria za 
mkataba wa haki za mtoto hazina ubaguzi na huwa kwa manufaa ya mtoto kila mara.Haki hizi 
zinajuimsha haki ya kujieleza na kutoa maoni,haki ya usawa,afya,elimu,mazingira safi,mahali 
salama pa kuishi na kulindwa dhidi ya kila aina ya madhara.Haki hizi zimeainishwa katika 
Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Mtoto wa 1989 (UNCRC), mkataba wa haki za 
binadamu ulioidhinishwa zaidi duniani. 

Haki za watoto ni mojawapo ya masuala ibuka ambayo yamekuwa wakishughulikiwa na 
waandishi mbalimbali haswa katika karne hii ya ishirini na moja.Kwa kipindi kirefu,watoto 
wamekuwa wakipuuzwa katika jamii na haki zao kukiukwa jambo ambalo limewapata waandishi 
mbalimbali hamu ya kumlika suala hili kupitia kazi zao za fasihi. 

Aries 1962 na Radbill 1968 wanadai kuwa ushahidi wa kihistoria unaonyesha kwamba,ukiukaji 
wa haki za watoto umekuwepo tangu mwanzo.Watoto wamekuwa wakidhulumiwa na asasi 
mbalimbali za jamii zikiwemo utamaduni na dini.Madai haja yanaungwa mkono na (Burges 
1979) anayesema kwamba, wazazi wamekuwa wakiwadhulumu watoto wao kwa muda mrefu 
sana.Wakati wa zamani, nchini Roma na jamii nyingi za Kiafrika ziliwasawiri watoto kama mali 
ya wazazi wao pale ambapo watoto hawa waliweza kuuawa au kutendewa maovu na wazazi wao 
bila kuchukuliwa hatua yoyote ya sheria (Cicchetti 1980).Wazazi wengi hupata motisha ya 
kuwadhulumu watoto wao kwa madai kuwa Biblia inapendekeza adhabu kali itolewe kwa watoto 
kama njia ya kuwaokoa kutokana na moto (Methali 23:13-14). 

Ukiukaji wa haki dhidi ya watoto,limekuwa tatizo sugu ambalo limesababisha kukatizwa kwa 
ndoto za watoto wengi duniani haswa kutokana na mahusiano ya kimapenzi pale ambapo wengi 
wao haswa wasichana hupata ujauzito na kuishia kuwacha shule.Ripoti zimetolewa na mashirika 
mbalimbali kuhusu suala hili la mimba za mapema na mahusiano ya kimapenzi.Kwa mfano, 
kutokana na data ya utafiti ya Shirika la Afya Duniani (WHO, 2013) ni wazi kwamba, watoto wa 
kike hususan milioni kumi na sita ambao umri wao upo kati ya miaka kumi na tano hadi kumi na 
tisa na hata wengine ambao umri wao upo chini ya miaka kumi na mitano huathirika sana na 
mimba za mapema kila mwaka.Idadi hii ni kubwa zaidi,tatizo ambalo linafaa kutafutiwa suluhu. 

Kule Afrika Mashariki,ni wazi kwamba asilimia kubwa ya watoto hulazimishiwa ndoa za 
mapema.Kutokana na taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto 
(UNICEF,2017),Sudan Kusini iliongoza kwa idadi ya juu zaidi ikiwa na asilimia 52,ikifuatwa na 
Uganda ikiwa na asilimia 40,Tanzania asilimia 28 na Kenya asilimia 23.Kuozwa kwa mtoto wa 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May  2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 2



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI 

 

 

 

 

kike akiwa angali mdogo ni ukiukaji wa haki dhidi ya watoto tendo ambalo limechangia mimba 
za mapema. 

Vilevile,licha ya maendeleo mengi katika miongo ya hivi karibuni,mamilioni ya watoto bado 
wanaishi bila haki zao za kimsingi.Ulimwenguni, inakadiriwa kuwa watoto milioni mia nane 
wanaishi katika maeneo tete na yaliyoathiriwa na migogoro ambapo haki za watoto hukiukwa na 
watoto kuingizwa katika unyonyaji na utumwa(De Young, Kenardy na Cobham 2011).Kulingana 
na ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) iliyotolewa mwaka wa 
2022, kati ya mwaka wa 2005 na 2020, visa zaidi ya elfu mia mbili sitini na sita vya ukiukaji wa 
haki za watoto viliripotiwa barani Afrika,Asia,Mashariki ya kati na Amerika kusini.Kutokana na 
ripoti hiyo, watoto laki moja walidhibitishwa kulemazwa, watoto elfu tisini wameajiriwa ili 
kutumikia jeshi,wengine kutekwa nyara,kubakwa na mengine mengi. 

Hata hivyo, waandishi wa kazi za fasihi wamelishughulikiwa suala hili kwa kiasi fulani.Katika 
kazi yake Kavuria (2008), dhuluma dhidi ya watoto katika riwaya za Kiswahili,alitoa maelezo 
kuhusu unyanyasaji wa kimapenzi kama aina moja ya dhuluma za watoto.Alielezea zaidi kuwa, 
watoto wanapodhulumiwa kimapenzi mara nyingi haki huwa haipatikani kwani kesi zao 
hutupiliwa mbali. 

Kwa mujibu wa Kiarie (2005), ukiukaji wa haki za watoto katika jamii ya leo husababishwa na 
tamaduni duni, msukumo wa wanarika na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii. Hivyo basi, 
fasihi ya kiswahili hutumiwa na waandishi mbalimbali kama kurunzi ili kuyamulika mambo jinsi 
yalivyo katika jamii.Kwa sababu hii, utafiti wetu ulijikita katika ukiukaji wa haki za watoto 
katika riwaya mbili kuu za kiswahili;Chozi la Heri (2017) ya Assumpta K. Matei na Nguu za 
Jadi (2021) ya Clara Momanyi. 

Tatizo la utafiti 
Ukiukaji wa haki za watoto limekuwa ni donda sugu katika jamii kwa muda mrefu sasa.Kila 
mtoto, bila kujali umri wake,rangi,jinsia au mahali alipozaliwa ana haki.Haki hizi zimewekwa 
katika sheria za kimataifa katika mkataba wa haki za mtoto (CRC).Mkataba huu unatambua 
kwamba watoto wote lazima watendewe haki kwa usawa na kwa utu.Sheria za mkataba wa haki 
za mtoto hazina ubaguzi na huwa kwa manufaa ya mtoto kila mara.Haki hizi zinajumuisha haki 
ya kujieleza na kutoa maoni,haki ya usawa,afya,elimu,mazingira safi,mahala salama pa kuishi na 
kulindwa dhidi ya kila aina ya madhara.Haki hizi zimeainishwa katika Mkataba wa Umoja wa 
Mataifa wa Haki za Mtoto wa 1989 (UNCRC), mkataba wa haki za binadamu ulioidhinishwa 
zaidi duniani. 

Kulingana na ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) iliyotolewa 
mwaka wa 2022, kati ya mwaka wa 2005 na 2020, visa zaidi ya elfu mia mbili sitini na sita vya 
ukiukaji wa haki za watoto viliripotiwa barani Afrika,Asia,Mashariki ya kati na Amerika 
Kusini.Kutokana na ripoti hiyo, watoto laki moja walidhibitishwa kulemazwa,watoto elfu tisini 
wameajiriwa ili kutumikia jeshi,wengine kutekwa nyara,kubakwa na mengine mengi.Watoto ni 
amali muhimu ya jamii na hivyo ni wahusika wakuu katika fasihi ambayo ni kioo cha 
jamii.Wanapoathirika bila shaka jamii kwa ujumla inaathirika.Utafiti huu hivyo basi unanuia 
kulizama tatizo hili kwa kuangazia ukiukaji wa haki dhidi ya watoto katika riwaya za kiswahili 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May  2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 3



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI 

 

 

 

 

mfano wa Chozi la Heri na Nguu za Jadi kama kipengele cha uhalisia, ambapo uhalisia katika 
maandishi ya kiubunifu hutumika kuendeleza maudhui mbalimbali 

 Ukiukaji wa haki za watoto katika riwaya zaChozi la Heri na Nguu za Jadi 

Mauaji 
Kuua ni hali ya kutoa uhai wa kiumbe au mtu.Haki ya kuishi inatokana na imani kwamba kila 
binadamu ana haki ya kuishi na haswa,hapaswi kuuawa na mtu au kitu kingine,ikiwa pamoja na 
serikali.Kulingana na Cucchetti 1989, nchini  Roma,wakati wa zamani pamoja na jamii nyingi za 
kiafrika, watoto walisawiriwa kama mali ya wazazi wao na wangeweza kuwatendea maovu 
mbalimbali na hata kuwaua bila kuchukuliwa hatua yoyote ya kisheria.Vilevile, katika Biblia, 
kuna visa mbalimbali vya mauaji ya watoto vilivyonakiliwa katika kitabu cha Mathayo 2:16 na 
Kutoka 1:15.Kutokana na vitabu hivi, kiongozi angetoa amri ya kuwaua watoto hata bila 
kupingwa na jamii. 

Riwayani, mauaji ya watoto yametokea pale ambapo mzee Kedi analiteketeza jumba la Ridhaa 
kutokana na tofauti zao za  kisiasa.Hii ni baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya Mwekevu 
ambaye alipingwa na wengi ila Ridhaa alimuunga mkono.Wanaoangamia katika mkasa ule wa 
moto ni mjukuu wa Ridhaa kwa jina Becky,Tila na Mukeli bintize Ridhaa.Haya yanajitokeza 
kupitia kauli ifuatayo;”sasa Ridhaa anatazamana na majivu ambayo bila shaka ni miili ya 
wanawe wawili,mkewe, mkaza mwanawe na mjukuu wake, Becky” (uk 5).Utafiti huu unaendana 
sambamba na taarifa iliyochapishwa mnamo Januari 28,2008 na Jeffrey Gettleman.Kutokana na 
taarifa hiyo, vurugu za kikabila ziliongezeka nchini kenya baada ya kuchaguliwa kwa kiongozi 
mpya na maafisa wa polisi walisema takriban watu kumi na tisa wakiwemo watoto kumi na 
mmoja walichomwa hadi kufa ndani ya nyumba na kundi la watu.Hata jeshi la Kenya 
lililotumwa kwa mara ya kwanza kuzuia wapinzani kushambuliana, lilishindwa kusitisha wimbi 
la mauaji ya kulipiza kisasi. 

Vilevile, umati uliodai kuwa Lemi kamwibia mama mmoja simu unamteketeza Lemi 
vibaya.Haya yanadhihirika katika usimulizi wa Dick kisa ambacho anakitamba akilini 
mwake.Katika kisa hiki,Tindi dadake Lemi anakwenda naye katika sherehe ili kusherehekea siku 
ya kuzaliwa kwa Lemi.Sherehe ilianza vyema,mtoto akala shibe yake,kisha akamwambia dadake 
waende nyumbani kwani usiku ulikuwa mpevu ila Tindi alimwambia kuwa ilikuwa mapema na 
amwache asakate midundo miwili kisha waondoke.Lemi alipelekwa kwenye chumba cha 
kutazamia runinga ili kusetiriwa asione asiyostahili kuona.Binti yule aliingia uwanjani na 
kusakata midundo bila kujali mpito wa wakati,wala mtoto aliyekuwa chumbani peke 
yake.Asubuhi jua lilipotaka kuchomoza Tindi alimshika mnuna wake mkono wakaelekea 
nyumbani.Hatua chache kabla ya Lemi na dadake kufika kwao kulitokea vurumai pale ambapo 
mama mmoja ambaye alikuwa ameraukia matwana ya kumpeleka kazini alikuwa akipinga 
ukemi,amenyang’anywa rununu yake akawa anakimbia kuelekea walikokuwa Lemi na dadake 
kwa msaada pasi na kujua alikuwa akiwaelekezea balaa.Umati wa watu uliokuwa umesikia 
kamsa ya mama huyu uliwaelekea kina Lemi na kutaka kuwavaa mawe na tairi.Dadake alikimbia 
na kumwacha Lemi ambaye alisalimiwa kwa mawe na mateke.Baadaye alivikwa tairi kiunoni na 
kumwagiwa petroli na kutiwa moto (uk 120-122). Kutokana na utafiti huu ni wazi kwamba 
watoto wanadhulumiwa haswa kwa madai ya wizi yasiyokuwa na ushahidi  kisha kuchomwa na 
kupokonywa haki yao ya kuishi. 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May  2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 4



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI 

 

 

 

 

 Dhuluma za kimapenzi 

Kulingana na Sneddon (2003), unyanyasaji wa mapenzi hutokea wakati mtoto anashirikishwa 
ngono.Inaweza kujumuisha mtu mzima kutumia mtoto ili kujiridhisha kimapenzi.Baadhi ya tabia 
za kujihusisha kimapenzi kati ya mtoto na mtoto au kati ya mtoto na mtu mzima huzingatiwa 
kuwa unyanyasaji wa kimapenzi.Tabia hizi zinaweza kuhusisha mguso wa mwili na usio wa 
mwili kama vile kufichua sehemu za siri na matumizi ya maneno ya kushawishi mtoto kingono. 

Mfano wa dhuluma za kimapenzi ni ubakaji.Kubaka ni kitendo cha kushirikiana kimapaenzi au 
ngono na mtu bila hiari yake kwa kutumia nguvu.Watoto ambao ni mali ya taifa ya nchi yetu 
wanahitaji kutunzwa na kulindwa kwani kuna ongezeko kubwa la ukiukaji wa haki zao za 
msingi.Ubakaji au unyanyasaji wa kijinsi kwa watoto (CSA) ni miongoni mwa aina za kutisha za 
ukiukaji wa haki zao.Madhara ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto huacha kovu kubwa ndani 
yao pale ambapo ustawi wao katika utu uzima huweza kusumbuliwa pakubwa.Ripoti 
zinazotokana na vyombo vya habari na mijadala kuhusu unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto 
zinaonyesha ongezeko la kitendo hiki kiovu ambacho kinahitaji kuchunguzwa kwa haraka.Kazi 
za fasihi pia zimetumika kulimulika jambo hili kupitia waandishi mbalimbali.Kwa mfano; 

Assumpta K.Matei katika riwaya yake Chozi la Heri amedhihirisha ubakaji katika dondoo 
hili;”Baadaye genge hili la la mabarobaro watano lilifululiza hadi walipokuwa maskini mabinti 
wangu wawili, Lime na Mwanaheri.Sikuweza kuvumilia kuona unyama waliotendewa.Nilijaribu 
kwa jino na ukucha kuwaokoa lakini likawa suala la mume nguvuze! Mahasimu hawa 
walitekeleza unyama wao na kuniacha bila kunigusa,niuguze majeraha ya moyo”(uk 25). 

Kutokana na dondoo hili,Lime na Mwanaheri ni wahadhiriwa wa kitendo hiki cha 
ubakaji.Wawili hawa ni wanawe Kaizari.Kaizari anamsimulia Ridhaa katika kambi ya wakimbizi 
jinsi wanawe walivyobakwa na mabarobaro watano baada ya nchi ya Wahafidhina kumtawaza 
kiongozi mwanamke.Uhafidhina unawafanya baadhi kutokubali uamuzi huu.Kaizari anaelezea 
kuwa, siku ya nane baada ya mapinduzi walisikia hodi mlangoni.Mkewe subira alisalimiwa kwa 
kofi kubwa kisha akaulizwa wapi kile kidume chako kijoga ambacho kimetuuza kwa kumpigia 
kura Mwekevu. 

Ubakaji huu wa Lime na Mwanaheri unaonyesha jinsi tamaa ya uongozi inavyosambaratisha 
mshikamano wa kijamii.Vijana wanatumiwa na viongozi kuendeleza njama zao ovu badala ya 
kuuwajibisha uongozi. 

Vilevile,Sauna anabakwa na Bwana Maya, baba yake wa kambo.Kitendo hiki kinadhihirika 
kupitia dondoo lifuatalo;”Mlaani shetani” Sauna aliumbia moyo wake... “Fikiria wewe, u kigoli, 
kifua ndio kinaanza kuvuvumka, kisha unaamka usiku kumpata baba yako, ba-ba-ya-ko, kwenye 
chumba chako cha malazi.Anakutenda ya kutendwa.Asubuhi huna hata uso wa kumtazamia 
yeyote,wala kinywa cha kumwambia mama yako kuhusu feli uliyotendewa”(uk 154). 

Katika dondoo hili, Sauna anazungumza moja kwa moja na moyo wake kana kwamba ni 
binadamu mwazake.Sauna anaulalamikia moyo wake kuonyesha masikitiko aliyonayo baada ya 
kuvunjiwa heshima na baba yake wa kambo.Kupitia maneno haya, ni wazi kwamba kitendo hiki 
cha ubakaji kinamsababishia Sauna uchungu moyoni kitendo ambacho anakikashifu.Kubakwa 
kwa Sauna kunaonyesha jinsi kinababa wa kambo wanavyowadhulumu wanao wa kike badala ya 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May  2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 5



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI 

 

 

 

 

kuwalinda.Kauli hii inaendana moja kwa moja na utafiti wa Sara Scott,2023 Septemba anapodai 
kuwa baba na baba wa kambo ndio jamaa wanaopatikana na hatia zaidi ya unyanyasaji wa 
kingono wa watoto katika familia.Anaeleza kuwa,kutokana na  kesi nyingi zinazoripotiwa ni 
wazi kwamba, wahalifu waliohukimiwa kwa kosa la ubakaji wa watoto asilimia kubwa ya 
wahalifu hao ni watu wa familia haswa kina baba wa kambo. 

Vilevile,mwalimu Fumba anamdhulumu mwanafunzi wake Rehema kimapenzi.Fumba 
anahusiana kimapenzi na mwanafunzi wake Rehema kisha kumtunga mimba (uk 102-
103).Pia,mwanaharakati analalamikia kulawitiwa kwa wavulana.Katika usemi anauliza kuwa 
“lakini ni wangapi wanaokumbuka kuwa hata maghulamu 
wanalawitiwa?”(uk.17).Vilevile,katika Nguu Za Jadi,wasichana wadogo wanazalishwa wakiwa 
bado hawajatimiza umri wa kujitwika majukumu kama hayo (uk.137-138).Hili linajitokeza 
kupitia taswira anayochora mwandishi kuhusu watoto wenye umri mdogo. 

Ndoa za mapema na za lazima 
Ndoa ya mapema ni ndoa ya kulazimishwa ya mtoto, ambaye kwa kawaida hufafanuliwa kama 
mtu aliye chini ya umri wa miaka  kumi na minane (Encyclopedia of Violence,Peace & Conflict 
Toleo la tatu, 2022).Ndoa za mapema hutokana na ukosefu wa usawa wa jinsia pale ambapo 
mtoto wa kike ndiye huathirika zaidi ikilinganishwa na yule wa kiume.Vilevile, ndoa za mapema 
zimethihirishwa katika Chozi la Heri kupitia mhusika Pete ambaye alilazimishwa kuolewa kama 
mke wa nne kwa mzee Fungo.Licha ya rai za nyanya yake kwamba aachwe afuatilie elimu, 
maneno hayo yaliangukia masikio yaliyotiwa uziwi kwani mama na ndugu zake Pete walikuwa 
wameamua kumuoza Pete kwani waliamini kuwa alikuwa ashaingia utuuzima  baada ya 
kupashwa tohara.Haya yanathihirika kupitia dondoo lifuatalo; 

“Maisha yangu yalichukua mkondo mwingine nilipojiunga na darasa la saba.Katika jamii 
yangu, inaamiwa kuwa msichana akiisha kupashwa tohara, ameingia utuuzima, hivyo ataipaka 
familia yake tope ikiwa ataendelea kuozea kwao bila mume.Wajomba zangu hawakuchelea 
kupokea posa na baadaye mahari kutoka kwa buda mmoja ambaye alinioa kama mke wa nne” 
(148). 

Kutokana na dondoo hili,tunagundua kwamba, Pete anaozwa akiwa na umri mdogo kwani 
alikuwa katika darasa la saba.Pete anaozwa kama mke wa nne kwa mzee Fungo.Ndoa hii ya Pete 
kwa mzee Fungo inasababishwa na imani potovu za jamii ile pale ambapo wanaamini kwamba 
wakati msichana anapashwa tohara anafaa kuolewa. 

Kukatizwa elimu 
Kila mtoto ana haki ya kupata elimu.Elimu ni taaluma inayomsaidia mwanadamu kujiendeleza 
kimaarifa na kiutafiti.Kwa mujibu wa Meyer (1977), elimu ni asasi iliyo na athari ya kuendeleza 
mitagusano ya watu katika jamii.Elimu huwafanya watu kujitegemea na kujikomboa 
kimawazo.Elimu huwapa vijana maadili na maarifa ifaayo katika jamii kwani baadae vijana 
hawa huweza kuajiriwa au kujiajiri.Elimu ni suala muhimu sana miongoni mwa vijana kwani 
huwatoa katika hali duni ya maisha.Kulingana na Taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la 
Kuhudumia Watoto (UNICEF 2023) kila mtoto ana haki ya kupata elimu bila kujali asili 
yake,jinsia au kabila. 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May  2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 6



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI 

 

 

 

 

Vilevile, waandishi mbalimbali wa kazi za fasihi za kiswahili wameliangazia suala hili.Kwa 
mfano,Assumpta K Matei ameliwasilisha suala hili kupitia mhusika Pete.Pete anakatiziwa elimu 
yake akiwa darasa la saba.Pete analazimishwa kuolewa na mzee Fungo kwa hofu kuwa ataipaka 
familia yake tope ikiwa ataendelea kuozea kwao bila mume licha ya nyanya yake kupinga 
kitendo cha mama na wajomba wake kumwoza kabla ya kukamilisha elimu. Hili linathihirika 
kupitia dondoo lifuatalo; 

“Huyu mtoto ni mbichi mno,”...’hatuwezi kumkabidhi mzee wetu huyu kifaranga kiteketeke hivi, 
tutakuwa tunampangaza ulezi.Isitoshe, Pete mwenyewe ana hamu kuu ya kufuatilia elimu, 
tumwache aizime kiu yake.Akiisha kutimiza maazimio yake,atajichagulia kijana mwenzake 
wafunge nakidi’ (Uk 148). 

Kutokana na dondoo hili, elimu ya Pete inakatizwa ili aozwe kwa mzee Fungo.Ingawa Pete ana 
hamu  kuu ya kufuatilia elimu, tamaduni na imani potovu zinamfanya kukatiziwa elimu yake 
akiwa darasa la saba.Mara nyingi, ndoa huthaminiwa sana kuliko elimu.Elimu kwa wasichana 
hupewa thamani ya chini . 

Vilevile, mhusika Zohali analazishwa kuacha masomo yake baada ya kupata ujauzito akiwa 
katika kidato cha pili.Katika masimulizi yake anaeleza kuwa, maisha yake yalianza kwenda 
tenge alipojiunga na kidato cha pili.Anazidi kueleza kwamba, hali ya mtafaruku wa hisia 
iliyowapata vijana katika umri huo aliikumbatia kwa papara za ujana ndipo akajipata 
ameambulia ujauzito.Mwalimu mkuu alitoa hukumu kwamba Zohali arejeshwe nyumbani na 
baada ya kujifungua wazazi wake wamtafutie shule nyingine.Hili linathihirika kupitia dondoo 
ifuatayo; 

“Dadake Zohali,samahani sana lakini uchunguzi unabainisha kwamba Zohali ni 
mjamzito.Nimekuita hapa ili uweze kumrejesha nyumbani.Akijifungua wazazi wake wanaweza 
kumtafutia shule nyingine” (uk 99). 

Kutokana na dondoo hili, mwalimu mkuu alitoa hukuma kwa Zohali kurejeshwa nyumbani 
baada ya kuambulia ujauzito na baadaye kutafutiwa shule nyingine akishaajifungua.Kutokana na 
hukumu hii ya mwalimu mkuu ni wazi kwamba Zohali anakatiziwa masomo yake.Vilevile, ami 
za Lucia na Akelo wanapinga elimu yao na kudai kuwa kuwaelimisha wasichana ni kufisidi 
rasilimali.Hili linathihirika kupitia kauli ifuatayo; 

“...si nyinyi mliokuwa hata mkipinga elimu ya mabinti hawa? Hamkusema kwamba kuwapeleka 
shuleni ni kufisidi rasilimali?” (uk 66) 

Kutokana na kauli hii ni wazi kuwa, Ami za Lucia na Akelo hawamthamini mtoto wa kike na  
elimu yake.Kwao kumsomesha msichana ni kuifisidi rasilimali 

Ajira kwa watoto 

Ajira kwa watoto hurejelea unyonyaji wa watoto kupitia aina yoyote ya kazi ambayo 
inawanyima utoto wao,inaingilia uwezo wao wa kuhudhuria shule ya kawaida na inawadhuru 
kimwili,kiakili,kimaadili na kijamii. Ripoti ya Shirika la Kazi Duniani ya mwaka 2021 
inaonyesha jumla ya watoto milioni 3.3 wako katika hali ya kutumikishwa kwa 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May  2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 7



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI 

 

 

 

 

kulazimishwa.Vilevile, katika riwaya ya Chozi la Heri,ajira kwa watoto imeendelezwa kupitia 
wahusika kama vile Sauna pale ambapo mhusika huyu anaajiriwa kwenye machimbo ya 
mawe,kuuza maji na hata pombe baani.Hii ni baada ya kupoteza matumaini na hamu ya 
kuendeleza masomo yake baada ya kuhujumiwa kimapenzi na kihisia.Suala hili linathihirika 
kupitia dondoo ifuatayo; 

“Nimefanya kazi katika machimbo ya mawe, nimewahudumia waungwana kwa namna zote 
katika majumba ya kuuzia pombe, nimeuza maji ya mito na madimbwi yaliyotiwa kwenye chupa 
zenye vibandiko vya kuvutia, ati ni mineral water...” (uk 156). 

Vilevile Chandachema anahusishwa katika ujira wa uchunaji wa majani chai akiwa mtoto wa 
darasa la tano kwenye Shirika la chai la Tengenea.Chandachema alianza kuchuna majanichai 
kwa malipo kidogo ili kuwatua Bi.Kimai na Bw.Tenge mzigo wa kumnunulia sare na 
madaftari.Hili linathihirika kupitia kauli ifuatayo; 

“Nilianza kuchuna majanichai kwa malipo kidogo nikiwa katika darasa la tano.Wakati mwingine 
ningerauka alfajiri na mapema kufanya kazi kabla ya kwenda shuleni saa kumi na mbili 
asubuhi”(uk 106-107). 

Vilevile,katika Nguu za Jadi,ajira kwa watoto inadhihirika kupitia vitendo vya Sihaba.Sihaba 
anawaajiri wasichana wadogo kufanya biashara ya ukahaba ili ajinufaishe kifedha.Hili 
linadhihirika kupitia kauli ifuatayo;Sihaba alitupwa korokoroni asubiri mashtaka ya kuwaajiri 
watoto wadogo kufanya biashara ya ukahaba(uk 143).Sihaba aliendeleza biashara hii kwa muda 
mrefu jambo ambalo lilijulikana na wengi ila waliogopa kutoa habari  hii kwani walimwogopa 
Sihaba sana.Hivyo, wakamwacha kuendeleza hujuma yake. 

Ni haki ya watoto kulindwa dhidi ya unyanyasaji wa kiuchumi na ajira ambayo inatatiza ukuaji 
wao kimaadili,kiakili na kiafya.Ni jukumu la serikali kutoa masharti ya kazi.Nchini Kenya, 
watoto wengi huajiriwa katika mashamba ya majani chai, kahawa, migodi na mikonge ambao 
umri wao upo chini ya miaka kumi na sita.Watoto hawa hupokea ujira mdogo usioweza 
kuyakidhi mahitaji yao licha ya kazi za sulubu wanazofanya. 

Watoto kutelekezwa na wazazi wao 

Kutelekeza mtoto hufafanuliwa kama kutofaulu kwa mzazi au mtu mwingine mwenye wajibu 
kwa mtoto kumpa chakula kinachohitajika,mavazi,makazi,matibabu na ustawi unaostahili 
(Benedictis na wengineo 2006).Kutowatelekeza watoto huwasaidia kukua vyema.Wajibu wa 
wazazi kuwafunza watoto wao maadili mema hutokea wakati huu.Watoto ambao hawatunzwi 
vyema katika utoto wao huishia kukosa maadili mema na wengi wao huingilia matendo maovu 
(Ciccheti 1983).Kuwaonyesha watoto mapenzi ili wahisi wako salama ni mojawapo ya utunzaji 
wa watoto. 

Katika riwaya ya Chozi la Heri, Pete anatelekezwa na mama yake mzazi.Pete analelewa na bibi 
mzaa mama yake baada ya mtafaruku kati ya baba na mama yake kutokea.Pete anapata kujua 
kuwa chanzo cha mama yake kumtelekeza kwa kwa nyanya yake ni kuwa hakuwa na mshabaha 
na baba yake.Katika usimulizi wake, Pete anasema; 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May  2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 8



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI 

 

 

 

 

“Mara tu macho yangu makinda yalipoanza kuutambua ulimwengu,nilijipata kwenye boma la 
bibi mzaa mama,kisa na maana, kumetokea mtafaruku fulani kati ya baba na mama.Sijui ni 
mtafaruku wa aina gani, ila katika pitapita zangu kijijini mwa bibi, alitokea domo kaya fulani 
akaninong’onezea kwamba sikuwa na mshabaha hata chembe na baba” (uk 147). 

Kutelekezwa kwa Pete na mamaye kunapelekea Pete kukosa vitu vya kimsingi.Kwa mfano, Pete 
anakosa sodo baada ya kukabiliana ana kwa ana na hedhi yake ya kwanza jambo ambalo 
linamfanya nyanya yake kumtafutia tambara la blanketi kwani ndilo lilikuwa fimbo ya karibu. 

Vilevile, Subira mkewe Kaizari anawatelekeza wanawe.Subira baada ya kutofautiana na mavyaa 
zake anaondoka na kuwaacha Lime na Mwanaheri bila kujali huzuni 
atakayowasababishia.Mwanaheri anaeleza kuwa,mama yake alitoka katika jamii ya Bamwezi 
jambo lililomsababishia mama yake kuchukuliwa kama mgeni katika boma yao na hata kijijini 
chao.Anaeleza kuwa, “haikuwa ibra kumsikia nyanya yao akimrejelea mama yao Subira kama 
múki,yaani ‘huyo wa kuja’na kusema kwamba msichana wa Bamwezi, hata akiwa na umri wa 
miaka tisini ni msichana wa Bamwezi tu”(uk 94).Maneno hayo ya nyanya yake Mwanaheri 
yalikuwa ya kumkumbusha Subira kwamba yeye hakuwa wa ukoo hule. 

Vilevile, riwayani, vitoto vidogo vinatelekezwa na mama zao baada ya kuzaliwa.Haya yanatokea 
pale ambapo baada ya kuzaliwa vitoto hivi vinatupwa.Neema anamwokoa mtoto aliyetupwa 
jalalani na kumpeleka kwenye kituo cha polisi.Neema anasimulia na kusema, “Nilipokaribia 
biwi hili, nilisikia sauti fulani dhaifu mawazoni mwangu, ‘Ng’aa! Ng’aa!’Niliipuuza sauti hii, 
nikidhani kuwa huu ni mwangwi wa sauti ya kitoto cha jirani yangu ambacho kilikuwa na 
mazoea ya kulia usiku kucha.Mara sauti hiyo ilisikika tena, ikanituma kutazama kando.Hapo 
hapo katikati mwa kilima hiki cha taka, niliona karatasi ya sandarusi ikifurukuta katikati ya 
fondogoo la kila aina.Kufurukuta huku kuliandamana na kilio kile hafifu...”(uk 161).Aidha, 
Mtawa Cizarina anasema kwamba “kuna mtoto aliyetupwa langoni mwa kituo cha watoto cha 
Benefactor akiwa amefungwa kijiblanketi kikuukuu” (uk 162). 

Kutokana na suala hili, ni wazi kwamba binadamu amezika hadhi na utakatifu wa maisha ya mja 
katika kaburi la sahau.Utafiti huu unaenda sambamba na ule wa (Kalume 2014) anapoeleza 
kwamba kitoto cha siku moja kilipatikana katika biwi la taka kule Lamu.Anayefanya kitendo kile 
anashtumiwa na wananchi.Kitoto kile kinapelekwa katika kituo cha kuvilea vitoto 
vilivyotelekezwa. 

Vilevile, babake Kairu anamtelekeza Kairu kwani hamsaidii mkewe katika malezi jambo ambalo 
halimpi amani Kairu katika masomo yake.Hili linatokea baada ya mama yake Kairu kuhusiana 
kimapenzi na baba yake Kairu japo ana familia nyingine.Kairu anazaliwa nje ya ndoa na 
kunyimwa nafasi ya kutunzwa na baba yake (uk 93). 

Chandachema anatelekezwa na wazazi wake mwalimu Fumba na Rehema.Chandachema 
analelewa na nyanya yake baada ya baba yake Fumba, kumtelekezea huko.Katika usimulizi 
wake,Chandachema anasema kuwa maisha yake yalijaa shubiri tangu utotoni.Hakumbuki 
akimwona mama yake (uk 102|).Kutokana na maelezo anayopewa na Katini,Fumba alimtunga 
mimba Rehema, mama yake Chandachema akiwa kidato cha tatu.Wazazi wa Rehema wanapinga 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May  2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 9



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI 

 

 

 

 

ndoa kati ya Rehema na Fumba na kumletea Fumba mtoto wake alee.Fumba anamwacha 
Chandachema alelewe na nyanya hadi kifo cha nyanya yake. 

Vilevile,katika riwaya ya  Nguu za Jadi,Mrima anawatelekeza wanawe wawili Sayore na 
Kajewa.Haya yanatokea baada ya Sagilu kumnyemelea na kumzuga Mrima kwa kutumia pesa 
kiasi kwamba Mrima anaisahau familia yake huku Mangwasha mkewe anaangaika na wanawe 
peke yake bila baba yao (uk 1).Riwayani tunajuzwa kuwa,Sagilu anamtaka Mangwasha 
kimapenzi licha ya kujua kwamba msichana huyu alikuwa na mchumba na baada ya kukataliwa 
anaweka kisasi dhidi yake.Mrima anazugwa pesa na Sagilu jambo lilnalomfanya kuingilia ulevi 
hadi kuisahau familia yake.Riwayani,tunajuzwa kuwa wana hawa hawakuwa na habari kuhusu 
baba yao(uk.1).Pia,Mangwasha mkewe Mrima anamweleza rafiki yake Mbungulu yote 
yaliyomsibu.Alimweleza jinsi anavyojitwika jukumu la kuwasomesha,kuwalisha na kuwavisha 
watoto hawa peke yake (uk 29).Hivyo,kutokana na utafiti huu,ni wazi kwamba Mrima haonekani 
kujitwika majukumu yake ya unyumba.Anakesha na kuamkia ulevini.Hana habari tena kuhusu 
familia yake. 

Kutokana na visa hivi vya kuwatelekeza watoto,ukweli ni kwamba watoto wanaozaliwa nje au 
ndani ya ndoa wana haki sawa.Wazazi wote wanajukumu la kuwashughulikia na kuwatunza 
wanao iwe wameona au la. 

Ubaguzi wa watoto 
Kumbagua mtu au mtoto kuna maana ya kumtendea mtu huyo kwa njia ambayo haifai au kwa 
njia tofauti kwa sababu fulani.Kulingana na katiba ya kenya ilioidhinishwa 2010 katika kifungu 
cha 27; kila mtu ni sawa mbele ya sheria na ana haki ya kulindwa na kupata manufaa sawa ya 
sheria.Usawa unajumuisha kupata haki na uhuru wote wa kimsingi kwa njia iliyo kamili na 
sawa.Kutokana na kifungu hiki, mtu hatakuwa na ubaguzi dhidi ya mwingine kwa njia ya moja 
kwa moja au vinginevyo. 

Vilevile, kifungu cha tano cha sheria ya watoto kinasema kwamba hakuna mtoto anayepaswa 
kubaguliwa kwa misingi ya asili,jinsia,dini,imani,desturi,lugha,maoni,dhamira,rangi,kuzaliwa 
kijamii,kisiasa,kiuchumi au hali nyingine.Riwayani, Pete anabaguliwa na mama na wajomba 
zake pale ambapo wanamwoza kwa lazima kwa mzee Fungo kama mke wa nne.Wanafanya hivi 
ili wapewe mahari itakayotumiwa kuwaelimisha ndugu zake watano wa kiume.Hili linadhihirika 
kupitia kauli ya mzee Fungo anapomwuliza Pete,”Utawezaje kujitunza wewe na mtoto wako na 
hali bibi yako ndiye huyo,hana hanani,na wazazi wako walafi walikuuza kwangu ili wapate pesa 
za kuwasomesha ndugu wako watano wa kiume?” (uk 149). 

Ubaguzi huu kwa Pete una msingi wake katika tamaduni ambazo zinamwona mtoto wa kiume 
kama mrithi wa familia.Kitendo anachofanyiwa Pete kinatokana na imani ya kitamaduni 
kwamba watoto wa jinsia moja ni bora kuliko wengine.Tamaduni zinazombagua mtoto wa kike 
zimepitwa na wakati na zinafaa kutupiliwa mbali.  

Utafiti huu unaendana sawia na ule wa Dauda (2008), anaposema kwamba ufaulu wa elimu ya 
mtoto wa kike ni mdogo kwani tafiti zimeonyesha kuwa wasichana wachache wanaenda shuleni 
kuliko wavulana.Alibainisha kuwa hii ni kwa sababu mtoto wa kike hajabahatika kuenziwa, 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May  2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 10



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI 

 

 

 

 

kulindwa na kupendwa katika jamii kutokana na mila fulani, imani potofu za kitamaduni na 
kidini ambazo zinamweka katika hatari ya kunyanyaswa na kutelekezwa. 

Uavyaji mimba 
Uavyaji mimba ni kitendo cha hiari cha kuua mimba kabla ya kijusi kuwa na uwezo wa 
kuishi.Lewis na Tamparo (2007) wanadai kuwa, kulingana na kamati ya kitaifa ya kuzuia 
unyanyasaji wa watoto, zaidi ya watoto elfu moja wanaavywa kila kuchao.Dkt.Richard Krugman 
wa kituo cha kitaifa cha kuzuia unyanyasaji  na utelekezwaji wa watoto wa Denver Kempe, 
anaweka idadi hiyo kuwa kubwa zaidi ya mimba zinazoavywa ambayo ni kutoka mimba elfu 
mbili hadi elfu tano kwa mwaka.Tunaweza kujua kwamba, thamani ya nafsi ni kuu machoni pa 
mungu lakini hali za kisasa na shinikizo za jamii zimepofusha watu wengi kutokana na ujuzi huu 
wa kina.Kwa sababu hiyo, chaguzi zinafanywa ulimwenguni kote ambazo zinapuuza thamani ya 
uhai wa mwanadamu na mojawapo ni utoaji mimba. 

Vilevile, kulingana na katiba ya kenya kifungu cha 26, kila mtu anahaki ya kuishi.Maisha ya mtu 
huanza baada ya mimba kutungwa.Uavyaji mimba hauruhusiwi isipokuwa kwa maoni ya 
mtaalamu wa masuala ya afya.Riwayani, mamake Sauna anamsaidia kuavya kitoto 
chake.Anafanya hivi kwa kumwogopa Bw.Maya ambaye ni baba wa kambo wa Sauna 
aliyemnajisi Sauna.Jambo hili linadhihirika kupitia dondoo ifuatayo;”...sikuweza kuamini 
kwamba mama yangu angekuwa amrijeshi wa mauaji.Maskini kitoto changu kilitunguliwa kabla 
hata hakijaumbika” (uk 155). 

Kutokana na suala hili ni wazi kwamba watoto wa kike wananyanyaswa na wazazi wao haswa 
kina baba wa kambo jambo ambalo linapelekea wao kuwa na ujauzito katika umri mdogo kisha 
kutafuta suluhu ya ujauzito hule ambayo ni kutungua ile mimba. 

 Wizi wa watoto 

Wizi wa watoto  ni hatua au desturi ya kupata na kuhamisha watoto kutoka mazingira yao salama 
kinyume cha sheria kwa madhumuni ya kazi za kuwalazimisha au unyanyasaji wa kingono.Wizi 
wa watoto umekuwa suala la ulimwengu mzima katika miaka michache iliyopita.Ingawa hakuna 
takwimu sahihi zilizopo, mkataba wa ILO(mwaka wa 2005) ulikadiria kuwa watoto 980,000 hadi 
1,225,000 wavulana na wasichana wako katika hali ya kulazimishwa kufanya kazi.Aina hizi za 
kazi ni pamoja na usafirishaji wa dawa za kulevya,ajira ya watoto nyumbani,kuhusisha watoto 
katika ukahaba na zingine nyingi jambo ambalo ni kinyume cha sheria.Kulingana na katiba ya 
kenya, iliyoidhinishwa mwaka wa 2010 katika kifungu cha 30, mtu hatahitajika kufanya kazi ya 
kulazimishwa. 

Riwayani, Assumpta K.Matei amelishughulikia suala hili kwa kupitia mhusika Sauna na 
Bi.Kangara.Sauna aliyekuwa kijakazi nyumbani mwa Lunga na Naomi anawaiba Dick na 
Mwaliko.Hii ni baada ya Naomi mkewe Lunga kumwacha Lunga na watoto wake baada ya 
Lunga kufilisika.Hali hii inamfanya Lunga augue shinikizo la damu na hatimaye kufa huku 
akiwaacha wanawe chini ya ulinzi wa kijakazi yao Sauna.Sauna anapata upenyu wa kuwaiba 
Dick na Mwaliko.Sauna anamuuza Dick kwa Buda pale ambapo Buda anamwigiza Dick katika 
matumizi na ulanguzi wa dawa za kulevya.Haya yanadhihirika kupitia dondoo ifuatayo;”siku ile 
baada ya kuibwa na kijakazi Sauna,Dickson alipelekewa baba mmoja tajiri ambaye alijitia 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May  2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 11



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI 

 

 

 

 

kumpeleka shuleni.Kumbe alikuwa kapelekwa katika chuo cha kuhitimu kama mvunja 
sheria!...Tajiri wake huyu, kwa lakabu Buda,alimfunza mbinu za kujikimu,akamwingiza katika 
biashara hii (uk 120). 

Vilevile, Bi. Kangara kupitia kwa juhudi za Sauna na wengine, alifanikiwa kupata wasichana wa 
kuuza katika madanguro,wavulana wa kuwapelekea matajiri ambao walishiriki katika ulanguzi 
wa dawa za kulevya na wafanyakazi katika makasri ya matajiri na katika mashamba ya 
mikahawa na michai.Aidha, wengine walisafirishwa ughaibuni ambako waliahidiwa kazi na 
walipofika kule ughaibuni walipata kwamba kazi zenyewe ni za kujidhalilisha (uk 158). 

Watoto kunyimwa haki ya kujua usuli wao na kutagusana na baba zao. 

Taarifa kuhusu asili ya mtu inajumuisha utambulisho wa wazazi wake na hali yake ya kuzaliwa 
na hata malezi.Kila mtoto ana haki ya kupata maelezo kuhusu asili yake ambayo yanaweza 
kumwongoza kugundua ukweli kuhusu vipengele muhimu vya utambulisho wake wa kibinafsi 
na kifamilia.Katika mkataba wa haki za watoto (CRC) kila mtoto ana haki ya utambulisho wake 
mwenyewe,rekodi rasmi ya yeye ni nani ambayo inajumuisha jina lake,utaifa na mahusiano ya 
familia.Hakuna mtu anafaa kuichukua haki hii kutoka kwake na ikiwa hili litatokea,serikali 
lazima isaidie mtoto kurejesha utambulisho wake haraka. 

Katika riwaya ya Chozi La Heri,Kairu anaeleza kwamba alipokosa karo aliwahi kumwuliza 
mama yake kwa nini asimwombe baba,ambaye anasikia ni mwenye chake na lake,amlipie 
karo.Hata hivyo,mama yake huwa hamjibu,anachompa ni mtazamo unaouliza 
swali,’Nitamwambia vipi mtu mwenye familia yake kumkimu mtoto aliyezaliwa nje ya 
ndoa?’(uk.93).Hivyo,kutokana na usemi huu ni wazi kwamba mama yake anajaribu kumwambia 
Kairu kwamba hawezi kumwomba baba yake amlipie karo kwani yeye amezaliwa nje ya 
ndoa.Jmbo hili linamyima Kairu haki ya kumjua baba yake mzazi na hata kutagusana naye. 

Vilevile,katika Chozi la Heri,mama yake Kipanga hamwelezi wazi kwamba baba yake mlezi 
hakuwa baba.Katika masimulizi yake pale kituoni cha mwanzo mpya,Kipanga yu hospitalini 
anaponusurika kifo kutokana na kangara iliyowaua watu sabini kutokana na matumizi ya 
vileo.Kipanga anasema kwamba,alianza kuchovya vileo akiwa kidato cha pili baada ya 
aliyedhania kuwa baba yake kumkana, na kulazimika kuhama alikoita kwao,yeye,mama yake na 
mnuna wake ambaye alisemekana ndiye mwana halisi wa baba yake.Kipanga anasema kwamba 
lililomuuma zaidi ni kwamba alipomtaka mama yake kumwambia ukweli,mama mtu hakumpa 
jawabu la kuridhisha.Alichosema ni,’Yapo mambo ambayo mtu hawi na uso wa kumtazamia 
mwanawe kwayo.Aliyekulea ndiye mzazi wako,mradi tu akubali kuwajibikia ulezi’(uk.143). 

Kutokana na utafiti huu ni wazi kwamba watoto wananyimwa haki ya kujua usuli wao na hasa 
kutagusana na baba zao haswa wakati ambao wamezaliwa nje ndoa.Kuwanyima watoto haki hii 
kunaweza kuwasababishia matatizo ya kisaikolojia pale ambapo wengi wao huishia kutafuta 
mbinu mbaya za kukabiliana na tatizo hili kama vile Kipanga. 

Madhara yanayotokana na ukiukaji wa haki za watoto 
Ukiukaji wa haki za watoto husababisha anuwai ya athari mbaya kwa  mwathiriwa na jamii kwa 
ujumla. Madhara haya yanaweza kuwa ya kijamii na pia yanayoathiri maendeleo ya mtu binafsi. 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May  2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 12



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI 

 

 

 

 

Kukimbia nyumbani 
Watoto wote wanahitaji na wanastahili usalama na hali ya kuhusishwa.Kutoroka nyumbani ni 
ishara kwamba watoto hawapati mahitaji muhimu nyumbani.Ili kuepukana na dhuluma 
zinazomkosesha mtoto utulivu na amani, watoto wengi huonelea ni vyema kukimbia nyumbani 
na kwenda mahali pengine angalau penye usalama na utulivu.Hii ndiyo hatua ya mwisho ambayo 
mtoto huchukua baada ya juhudi zote za uvumilivu kugonga mwamba. 

Mhusika Zohali katika Chozi la Heri anakimbia nyumbani kwao baada ya baba yake 
kumdhalilisha baada ya kupata ujauzito akiwa kidato cha pili bila utetezi wowote wa mama 
yake.Zohali anapoona kwamba maisha nyumbani kwao yamekuwa magumu, anatorokea mtaani 
ambako anaishi maisha duni ya matumizi mabaya ya dawa za kulevya hadi pale ambapo 
wenzake wanapompeleka kwenye Wakfu wa Mama Paulina ambapo anapewa hifadhi na 
kujifungulia hapo.Zohali anamdanganya Mtawa Pacha kwamba ni yatima. 

Katika usimulizi wake, Zohali aliwaelezea wenzake madhila aliyoyapitia nyumbani kwao.Haya 
yanathihirika kupitia dondoo ifuatayo;”Baba alisema kwamba hakuwa na pesa za kumlipa 
kijakazi tena.Kazi za nyumbani ziliniangukia mimi.Si kufua,si kupiga deki,si kupika...almuradi 
kila siku ilikuwa na adha zake” (uk 101). 

Kutokana na utafiti huu ni wazi kwamba,madhila aliyopitia yalimtia Zohali uchungu na 
unyanyapaa ambao ulimfanya awafishe wazazi wake wakiwa wangali hai.Hata hivyo, kupitia 
usimulizi wake tunapata kujua baba yake alijawa na majuto baadaye na akaanza kumtafuta mara 
tu baada ya kugubdua ametoroka (uk 101). 

Kutatizika kimasomo 
Unyanyasaji na kutelekezwa kwa watoto huongeza hatari ya watoto kupata matatizo ya kielimu 
(Briere et al.,1996; Johnson-Reid et al;2004;Nikulina et al;2011).Watoto ni wanajamii ambao 
wanapenda kuona haki ikitekelezwa.Watoto huwa na imani kwamba,haki ikitekelezwa baadhi ya 
matatizo kama vile,ubaguzi,dhuluma na maonevu husuluhishwa.Aidha palipo na haki pana 
usawa na amani. 

Fasili kuhusu ndoa za utotoni inasisitiza kwamba, watoto wanapoolewa mapema,elimu yao rasmi 
mara nyingi hukatizwa.Kukatizwa kwa elimu hii huzuia kupata maarifa na ujuzi unaowapa 
nafasi ya ajira(Wiliamson 2012).Madhara mbalimbali ya ndoa za utotoni na kuachishwa shule 
yameonyeshwa pale ambapo waathiriwa wanapata nafasi ndogo za ushiriki na maamuzi na hata 
hatari ya kufanyiwa vurugu. 

Mhusika Pete katika Chozi la Heri anaozwa kwa mzee Fungo akiwa darasa la saba ili mahari 
itayopatikana iwasomeshe ndugu zake wa kiume tendo linaloashiria ubaguzi.Kutokana na ndoa 
hii ya lazima, masomo ya Pete yanafikia kikomo kwani  hakufaulu kuizima kiu yake ya elimu 
(uk 148).Katika ndoa yake, Pete hana amani kamwe kwani anasema kuwa,”ule unene wake mzee 
Fungo,lile kutuzi lililotoka kwenye makwapa yake makuza na kufudikiza kote chumbani,ule wivu 
wa mke mwenzangu wa pili,kule kukemewa na kuchekwa na wana wa mke wa kwanza...yote 
yalininyong’onyeza na kuniumbua” (uk 149). 

Tunaweza kusema kuwa,kama Pete hangelazimishwa kuolewa na mzee Fungo,angeizima kiu 
yake ya masomo kwani kutokana na kauli ya nyanya yake ni wazi kwamba Pete alikuwa na 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May  2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 13



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI 

 

 

 

 

hamu kuu ya kufuatilia elimu na wakati ambapo angetimiza azimio yake angejichagulia kijana 
mwenzake wafunge nakidi. 

Ukosefu wa mahitaji ya kimsingi 
Aina nyingine ya athari za ukiukaji wa haki za watoto ni ukosefu wa mahitaji ya kimsingi kwa 
watoto.Makuzi sahihi ya watoto,afya,elimu na ulinzi wa sheria ni mahitaji ya kimsingi ya 
watoto. 

Riwayani,Pete anakosa mahitaji ya kimsingi baada ya mama yake kumtelekezea kwa nyanya 
yake.Katika masimulizi yake,Pete anaeleza kuwa hakudiriki kuonja tamu ya kupendwa na 
wazazi wake.Anaendelea na kusema kuwa, hakumbuki hata siku moja akiulizwa kuhusu neema 
na mashaka yake shuleni.Hata baada ya mamake kuona kwamba bibi anamtaka kununua sare 
nyingine kila baada ya miezi michache,haikumpa kuwaza kuwa kima cha mwanawe kimeanza 
kuwanda,nayo maumbile yameanza kufanya kazi yake (uk 147). 

Vilevile,Pete anakosa sodo baada ya kupata hedhi.Anaelezea kwamba, anapata hedhi yake ya 
kwanza baada ya kuingia darasa la sita.Tatizo ni kwamba, hakuwa na mama wala dada wa 
kumjuza ya kufanya litokeapo la kutokea jambo ambalo linamfanya kumwendea ajuza wake 
ambaye amejiinamia kwa uzee.Kutokana na yale mazoea yao ya jadi, ajuza huyu alimtafutia 
tambara la blanketi alitumie kama sodo.Anazidi kueleza kuwa, tambara lile halikufaa kitu kwani 
alihitajika kutafuta njia nyingine ya kujikuna ajipatapo. Zaidi ya hayo, kutokana na 
mahangaiko hayo,juma zima lilikuwa limepita kama darasa halijakilimbuka hata kivuli chake (uk 
148). 

Vilevile,katika masimulizi yake Chandachema ni wazi kwamba baba yake hakuwa akituma 
mahitaji ya mwanae Chandachema baada ya kumtelekeza kwa nyanyake jambo ambalo 
linamlazimu nyanyake Chandachema kutumia kidogo alichokuwa analetewa na dada zake 
kumtunza yule mtoto (uk 102). 

Hivyo basi, hali ya watoto kukosa mahitaji ya kimsingi ni jambo la kihalisia kulingana na 
nadharia ya uhalisia.Jambo hili hufanyika katika ulimwengu halisi na ulimwengu wa 
kawaida.Watoto waliotelekezwa huteseka sana kutokana na mapuuza ya mahitaji yao.Utafiti huu 
unaenda sambamba na ule wa Abashula,Jibat na Ayele (2014) nchini Ethiopia unaobaini kuwa 
watoto waliotelekezwa na wazazi wao hukumbana na matatizo mengi kama vile kukosa 
mavazi,elimu,chakula na mahitaji mengine ya kimsingi na ukosefu wa mapenzi ya wazazi 
huwasababishia msongo wa mawazo. 

Watoto kuishi katika mazingira yasiyokuwa na amani na hatarishi 
Mkataba wa watoto (2001) huwalinda watoto ambao umri wao upo chini ya miaka kumi na 
minane.Watoto hupata haki ya kulindwa na hali ambazo zinayaweka maisha yao hatarini kutoka 
kwa mkataba huu.Watoto waliotelekezwa na wazazi wao huishi katika mazingira ambayo 
yamejaa changamoto.Riwayani,baada ya nyanya yake Chandachema kufariki,Chandachema 
analazimika kuhamia kwa jirani yao Satua.Satua alimwonyesha waziwazi kwamba hamtaki.Hali 
hii inadhihirika zaidi mwandishi anapoeleza kuwa,baada ya Chandachema kuishi kwa Satua kwa 
miezi miwili alianza kuona mabadiliko.Uchangamfu aliokuwa nao Satua uliyeyuka ghafla kwani 
alianza kulalamikia kuisha haraka kwa sukari,alilalamikia matumizi kiholela ya sabuni ya 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May  2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 14



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI 

 

 

 

 

kuogea na pia alinung’unika kuhusu kubanana kwa jeshi la watoto kwenye chumba cha malazi 
(uk103).Chandachema alichukizwa na malamishi hayo na kulazimika kufunganya kidogo 
alichokuwa nacho na kuondoka. 

Vilevile, baada ya Chandachema kuondoka kutoka kwa jirani yao Satua,alipewa hifadhi na 
Bw.Tenge na Bi.Kimai pale ambapo alilelewa pamoja na watoto wao watano.Katika masimulizi 
yake,Chandachema anaeleza kuwa chumba cha wafadhili wake kilikuwa kimoja;ndicho cha 
malazi,ndicho cha mapokezi,ndicho jikoni.Sebule na chumba cha malazi viligawanywa na shuka 
moja nyepesi.Usiku  watoto walilala juu ya vigodoro ambavyo ni kama viliwekwa mvunguni 
mwa kitanda cha wazazi.Zaidi ya hayo,wakati Bi.Kimai alienda mashambani,chumba kile 
kiligeuka na kuwa danguro.Bw.Tenge alikuwa akimleta mwanamke mmoja baada ya mwingine 
hapo hapo mbele ya wanawe.Kitendo hiki cha ukware cha Bw.Tenge kilimpa Chandachema 
dhiki za kisaikolojia (uk 106). 

Hivyo basi, ni haki ya watoto kuishi katika mazingira ambayo hayaatarishi maisha yao.Ni 
jukumu la serikali na wazazi kuhakikisha kwamba mazingira ambayo watoto wanaishi yana 
utulivu na amani.Watoto huathirika kiakili na kitabia iwapo watalelewa katika mazingira 
yaliyojaa fujo na migogoro kwani wao huyaiga na kuyatilia maanani mambo ambayo 
wanatendewa na watu wazima. 

Matumizi ya dawa za kulevya 
Tatizo la dawa za kulevya linaendelea na limekuwa suala nyeti duniani.Kulingana na ripoti 
zilizopo ulimwenguni kuhusu dawa (2018),watu wengi wameadhiriwa sana na dawa za 
kulevya.Suala la matumizi ya vileo limechangiwa sana na utelekezwaji wa watoto.Watoto 
hutumia vileo hili kujisahaulisha na hali ngumu ya maisha inayowakabili. 

Watoto wanapokabiliana na changamoto katika maisha huanza kutumia dawa za kulevya ili tu 
wajiliwaze kutokana na madhila ambayo wanapitia.Katika riwaya ya Nguu Za Jadi,wasichana 
wadogo waliozalishwa wakiwa wadogo wanaonekana wakinusa gundi chini ya viambaza vya 
maduka(uk 137). 

Vilevile,katika riwaya ya Chozi la Heri,Dick analazimika kuzitumia dawa za kulevya wakati wa 
kuzilangua kwa miaka kumi baada ya kutekwa nyara na Sauna na kuuzwa kwa Mzee 
Buda.Pia,Kipanga anaishia kutumia vileo ili kujisahaulisha kusambaritika kwa familia 
yao.Kipanga alianza kuchovya kidogokidogo akiwa kidato cha pili baada ya aliyedhania kuwa 
baba yake kumkana (uk 143). 

Mapendekezoya kukabiliana na Ukiukaji wa Haki za Watoto 
Assumpta K.Matei na Clara Momanyi wanapendekeza baadhi ya hatua zinazoweza kutumika ili 
kutatua tatizo hili la ukiukaji wa haki za watoto.Kulingana na Goldstorm(1979:340), suluhisho la 
tatizo huwa bora katika kuimarisha maisha ya watoto katika jamii. 

Miongoni mwa mapendekezo yaliyotolewa na waandishi hawa wawili ni pamoja na nafasi ya 
maafisa wa polisi kukabiliana na wale ambao wanakiuka haki za watoto. Polisi wana wajibu wa 
kuchunguza makosa yote ya jinai.Makosa yanayotendewa watoto huwa nyeti sana na mara 
nyingi huhitaji polisi kufanya kazi na mashirika mengine katika kufanya uchunguzi.Hatua 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May  2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 15



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI 

 

 

 

 

inayochukuliwa na maafisi wa polisi ya kuwakamata Sauna na Bi.Kangara na kuwashtaki kwa 
ulanguzi wa binadamu kisha kufungwa jela miaka kadha na kazi ngumu inayaokoa maisha ya 
watoto waliodhulumiwa na wawili hao (uk.158).Pia,polisi wanamwokoa Mwaliko kutoka kwa 
Bi.Kangara na kumkabidhi kwenye kituo cha Benefactor (uk.159).Vilevile,katika Nguu Za 
Jadi,polisi wanamkamata Sihaba kwa kuwahusisha wasichana wadogo katika biashara ya 
ukahaba kwa manufaa yake.Vilevile,maafisa wa polisi wanawaandama wazazi wa wasichana 
waliotumika katika ukahaba ili kuchukuliwa hatua za kisheria. 

Pili,ni wajibu wa wanajamii kuwasaidia watoto wanaodhulumiwa.Hatua iliyochukuliwa na 
Bi.Kimai na Bw.Tenge katika Chozi La Heri ya kumchukua Chandachema kama mwana wao 
baada ya kukosa hisani kwa Satua inamsaidia sana kwani anapata kuishi na wawili hawa na 
kulelewa kama mwanao.Pia,Neema anachukua wajibu wa kukiokota kitoto kilichokuwa 
kimetupwa kwenye jaa la taka,anakipeleka katika kituo cha polisi na baadaye katika makao ya 
watoto mayatima ya Benefactor (uk.161). 

Tatu,waandishi wanapendekeza kuwepo kwa vituo vya watoto.Vituo hivi vikiwepo huweza 
kuwaokoa watoto kutokana na vitendo viovu.Katika Chozi La Heri,mwandishi amefaulu kutumia 
kituo cha Benefactor katika kuendeleza hoja hii.Watoto wanaookolewa kutokana dhuluma 
wanazozipitia kama vile Mwaliko kutekwa nyara na Sauna kisha kuokolewa na maafisa wa 
polisi anapelekwa katika kituo hiki (uk.159).Vilevile,kitoto kilichookotwa na Neema kutoka 
jaani la taka anakipeleka katika kituo hiki cha Benefactor (uk.161) ambacho ni makao ya watoto 
wa mayatima.Vilevile,katika Nguu Za Jadi,watoto waliookolewa baada ya  kutoroka shuleni ili 
kufanya biashara ya ukahaba na kukosa mahali pa kwenda waliwekwa kwenye makao ya watoto 
(uk.143). 

Nne,ni wajibu wa Mashirika ya Kidini kuwasaidia watoto wanaodhulumiwa.Hatua 
inayochukuliwa na Shirika la Kidini la Hakikisho la Haki na Utulivu ya kumpeleka 
Chandachema kwenye makao ya watoto mayatima ya Jeshi La Wajane wa Kristu inamsaidia 
sana.Chandachema anapata kuishi kule kama vile nyumbani kwao huku akiendelea na masomo 
katika shule ya Tangamano (uk.108). 

Tano,ni wajibu wa jamii kuvipinga vitendo vya ukiukaji wa haki za watoto.Wajibu huu 
unahusisha wakubwa na wadogo.Assumpta K.Matei katika Chozi La Heri anatoa mfano wa bibi 
yake Pete anapojaribu kupinga kuozwa kwa Pete kwa mzee Fungo kwa kumwona bado mtoto 
anayestahili nafasi ya kukua,kupata masomo na baadaye kujichagulia mchumba (uk.148),japo 
bado Pete anaozwa na mama na wajomba wake. 

Sita,waandishi wanapendekeza kuwa ni jukumu la watoto kuzipinga dhuluma 
zinazowakabili.Assumpta K.Matei anamtumia mtoto Dick anayeamua kuyabadilisha maisha 
yake.Baada ya miaka mitano ya kulangua dawa za kulevya.Dick anafanya uamuzi wa kuacha 
biashara hii haramu na kufungua biashara ya kuuza vifaa vya simu (uk.110). 

Hatimaye,waandishi wanapendekeza kuwa ni wajibu wa serikali kuwasaidia watoto ambao haki 
zao zinakiukwa.Clara Momanyi anatoa mfano wa serikali ikihimizwa kuwasaidia wasichana 
ambao walihusishwa katika biashara ya ukahaba na Sihaba ili warudi shuleni (uk. 143) 

 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May  2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 16



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI 

 

 

 

 

Hitimisho 
Kwa ujumla, ukiukaji wa haki za watoto una athari mbaya kwa ustawi miongoni mwa jamii.Ni 
muhimu kutambua kuwa,watoto ni amali ya jamii na wanapaswa kulindwa dhidi ya dhuluma 
zozote zile. Kutokana na mapendekezo yaliyotolewa,wanajamii,maafisa wa usalama na 
mashirika mbalimbali yana wajibu wa kuzilinda haki za watoto.Vilevile,watoto wana jukumu la 
kupinga dhuluma ambazo wanatendewa. 

 

MAREJELEO 
Amulenga, C.M. na Amulenga, A.V. (2009) Solving Problems Occuring in Early Marriages. 

Nairobi: Focus Publishers 

Atieno, W. (2014) ‘Mama ajifungua ndani ya TukTuk’. Taifa Leo, Septemba 9, kur.1,2 

Bakize, L.. (2014). Utangulizi wa Fasihi ya Watoto. Dar es Salaam: Maccony Printing Press. 

Behnam, N. (2008) ‘Kikanda, jamii na watoto’:Ripoti ya Kikanda ya kuanza 

kujifunza:Kuwawezesha jamii kuhusu ustawi wa watoto.Washington,DC. 

Boss, P. (1998) Family Stress Management. Newbury Park, California: Sage Publications. 

Burke, C. (1999) Covenanted Happiness, Love and Commitment in Mariage, 2nd Ed. New 

Jersey: Screptree Publishers. 

Bronfenbrenner,U.(1979).’Elimu ya ustawi na uhusiano wa binadamu na mazingira’.Asili na 

desturi ya kutathmini vijiji kushiriki.Cambridge,MA:Uandishi wa Chuo Kikuu cha Harvard. 

Cancer Global Statistics (2014).www.int/media centre/factsheets/fs297/en/. 

Chambers,R. (1994).’Asili na desturi ya kutathmini vijiji kushiriki’.Maendeleo Duniani, 22.953-

969’. 

Chapman, R. (1982) The Language of English Literature. London: Edward Arnold Publishers. 

De Genors, M.K (2008) Inmate, Relationship, Marriage and Families. Seventh edition.New 

York:Mc Grace Hill. 

Drabble, M. (1995) The Oxford Companion to English Literature.New York: Oxford University 

Press. 

Farouk, M.T. (1974) Uchambuzi wa Maandishi ya Kiswahili. Nairobi: Oxford University press. 

Gitau, E. (2014) ‘Unyanyasaji Dhidi ya Wanaume katika Fasihi Andishi ya Kiswahili’.Tasnifu 

ya uzamili Chuo kikuu Cha Kenyatta. 

Habwe, J.H. (2005) Paradiso. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation. 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May  2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 17

http://www.int/media centre/factsheets/fs297/en/


IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI 

 

 

 

 

Johnson, T. (2002) “ Violence and Abuse of Women and Girls in Kenya, Population 

Communication Africa.Nairobi: New World Printers. 

Karanja, D.W. (2008). Usawiri wa Masuala-Ibuka katika hadithi za watoto.Tasnifu ya uzamili. 

Chuo kikuu cha Kenyatta. 

Khamis, S.A. (2012) “ Riwaya Mpya ya Kiswahili. Utandawazi au Utandawizi? Lugha ya 

Riwaya Mpya Ya Kiswahili Inavyodai”. Bayreuth University. 

Krueger, A. Thompson, G. na Crispin, V. (2013).’Kufijunza kutoka kwa mifumo ramani ya 

kulinda watoto na uchambuzi katika Afrika Magharibi’: Maana ya Utafiti na Sera.Sera za 

Kimataifa,5,47-55. 

McKay, S., na Mazurana, D. (2004).’Wako wapi wasichana?’ Montreal, Canada: Kituo cha 

Kimataifa kwa Haki za Binadamu na maendeleo ya Kidemokrasia. 

Panter-Brick, C., na Leckman, J. (2013). Tangazo mfululizo la Mhariri: Kuimarisha kwa ustawi 

wa mtoto –Njia zilizounganika kwa hali njema.Jarida la Saikolojia na Taaluma,Tiba ya Ugonjwa 

wa Akili kwa Watoto, 54,333-336. 

Thompstone, G. (2010). Mapping na Uchambuzi wa mfumo wa kulinda watoto nchini Sierra 

Leone.Hong Kong,China: Watoto wa mpakani (Child Frontiers). 

UNPD. (2013) Dalili za Umaskini na Maendeleo, Sierra Leone.Imepatikana kutoka 

hdstats.undp.org 

UNICEF. (2013). Ukeketaji na Kutahiri wanawake : Maelezo ya takwimu na ugunduzi wa 

mienendo ya mabadiliko.New York, NY: Mwandishi. 

UNICEF,UNHCR,Kulinda Watoto (Save the Children), na Maono Duniani (Maono ya 

Dunia).(2013).Njia bora ya kuwalinda watoto wote: Nadharia na Mazoea ya mfumo ya kulinda 

watoto,ripoti ya mkutano.New Delhi, India: Mwandishi. 

Wessells, M.G. (2006). Wanajeshi watoto: Kutoka kwa Vurugu hadi Kulindwa. Cambridge, MA: 

Uandishi wa Chuo Kikuu cha Harvard. 

Wessells, M.G. (2009a). Je, tunajifunza nini kuhusu kulinda watoto katika jamii? Kikanda cha 

mapitio ya ushahidi juu ya jamii kuhusu utaratibu wa kulinda watoto katika mazingira ya 

kibinadamu na maendeleo.London, England: Kulinda Watoto (Save the Children). 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May  2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 18



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI 

 

 

 

 

Whitney,S.D., Tajima, E.A.,Herrenkohl,T.I.,& Huang, B. (2006). Defining child abuse: 

Exploring variations in ratings of discipline severity among child welfare practotioners. Child 

and Adolescent Social Work Journal, 23, 316-342. 

Yeo.L.S., & Choi, P.M. (2011). Cognitive-behavioural therapy for children with behavioural 

difficulties in the Singapore mainstream school setting. School Psychology International,32,616-

631. 

 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May  2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 19


	Jackline Njeri Murimi, Chuo Kikuu cha Tom Mboya
	IKISIRI
	Usuli wa mada
	Tatizo la utafiti
	Ukiukaji wa haki za watoto katika riwaya zaChozi la Heri na Nguu za Jadi
	Mauaji
	Ndoa za mapema na za lazima
	Kukatizwa elimu
	Ubaguzi wa watoto
	Uavyaji mimba

	Madhara yanayotokana na ukiukaji wa haki za watoto
	Kukimbia nyumbani
	Kutatizika kimasomo
	Ukosefu wa mahitaji ya kimsingi
	Watoto kuishi katika mazingira yasiyokuwa na amani na hatarishi
	Matumizi ya dawa za kulevya


	Mapendekezoya kukabiliana na Ukiukaji wa Haki za Watoto
	Hitimisho
	MAREJELEO

