

































IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA  RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA 

 

 

 

 

ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA  RIWAYAZA 
PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA 

Jackline Njeri Murimi, Chuo Kikuu cha Tom Mboya 

na 

Solomon Muli, Chuo Kikuu cha Mount Kenya 

IKISIRI 
Suala la imani katika Mungu ni nyeti na linatiliwa maanani na binadamu katika tamaduni 
mbalimbali kote duniani kama njia mojawapo  ya kujaribu kutafuta majibu ya changamoto 
anazokubana nazo kila uchao. Katika jamii nyingi za kiafrika,dini ni mfumo wa maisha (Mbithi 
2011 )ambapo kila mwana jamii alihitajika kushiriki. Hata hivyo, suala hili la kidini linaonekana 
kuwatamausha vijana wengi na kufifisha imani yao katika dini.                                                                
Hivyo ,utafiti huu ulinuia kuchanganua  baadhi ya athari za udhanaishi  wa dini kwa vijana kwa 
kurejelea riwaya ya Paradiso na Kidagaa Kimemwozea  zilizoandikwa na  John Habwe na Ken 
Walibora mtawalia kwa kuchunguza jinsi John Habwe na Ken Walibora wanavyoangazia 
udhanaishi wa kidini katika jamii .  
Katika kulizamia suala hili makala hii iliongozwa na nadharia ya udhanaishi iliyoasisiwa na 
Mwanathiolojia kutoka Denmaki(1813-1855),Fredrick Nietzsche,Martin Heidegger,Gabriel 
Marcel na Karl Jaspers waliotokea karne ya 20 na Jean Paul Satre Mfaransa aliyetokea baada ya 
vita vya pili vya dunia.  Mihimili yake ilisaidia kufikia malengo ya yetu. Mihimili mikuu ya 
nadharia ya udhanaishi ni pamoja na;kutilia mkazo matatizo halisi yanayomsibu mwanadamu na 
kuwa na imani ya kijozi juu ya imani ya kuishi, inapalilia kutokuwepo kwa mungu na uumbaji 
wake wa ulimwengu,inatilia mkazo kuwa juhudi za mtu kujisaka au kujaribu kupambana na 
maisha huishia katika mauti,  maudhui yake ni kama vile uhuru wa mtu binafsi kuweza kufikiri 
halafu kutoa jawabu lake. Nadharia husimulia taabu na kuchoka na hali ambazo husumbua 
yanayotatiza mwana wa adamu,  nadharia hii inajadili mkengeuko,nadharia hii inachora taswira 
ya mateso anayopitia mwanadamu duniani,  nadharia hii inatilia mkazo kuwa maisha yamejawa 
na utupu na kihoro hasa kuhusu siku za kesho.Maisha yamejawa na ubwege na huhakikisha 
binadamu kuwa mwisho wa maisha ni kifo.Nadharia hii ilifaa utafiti kwani ilitumika kueleza 
jinsi baadhi ya vijana waumini wavavyoyaona maisha jambo ambalo linawafanya watamaushwe 
na dini kila uchao. Nadharia hii ilitumika kupambanua ukweli wa je ni lipi ambalo baadhi ya 
vijana katika jamii wamejua hivi karibuni ambalo mababu zao hawakufahamu hapo awali?Utafiti 
ulifanyika maktabani kuliko na vitabu, majarida,matini na magazeti na wa mtandaoni ambapo 
data ilipatikana  kutokana na tasnifu zilizoandikwa kuhusu mkengeuko wa imani za 
kidini.Sampuli ya kimaksudi ilitumika  katika kuteua riwaya ya Paradisona Kidagaa 
Kimemwozea. Mbinu anuwai za kimaelezo zilitumika katika kuchambua data na kuiwasilisha 
kwa lugha ya nadhari kuambatana na lengo la utafiti. Maarifa yaliyopatikana katika utafiti huu 
yatakuwa na mchango mkubwa katika maarifa yaliyopo kuhusu vijana na  masuala ya dini katika 
jamii. 
 
 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 20



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA  RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA 

 

 

 

 

Utangulizi 
Kulingana na Cames (1984), udhanaishi ni falsafa inayoshughulikia maswali kuhusu maisha ya 
mwanadamu. Kwa jumla, ni mtazamo unaokagua kwa mapana mwanya alio nao mwanadamu 
kwenye    ulimwengu anamoishi. Vile vile, ni falsafa inayoelezea mahusiano yaliyomo kati ya 
mwanadamu na Mungu na ikiwa mwanadamu huyu anapaswa kuamini kuwepo kwa Mungu au 
la. Taabu na matatizo anazokutana nazo mwanadamu zinamfanya kuwa na maswali chungu 
nzima kuhusu maisha haswa juu ya maswala ya uwepo wa maadili na kiroho. Kwa mujibu wa 
Mark Sanchez (2021), dini ni mfumo wa imani, mila na alama zilizoanzishwa karibu na wazo la 
uungu au kutoka takatifu. Dini ni mafundisho  yaliyoundwa na seti ya kanuni, imani na mazoea 
anazoenzi binadamu anapokosa suluhu mwafaka kuhusu hali nyeti anazokutana nazo maishani. 
Baada ya zama za giza, mwanadamu alianza kujisatiti kutafuta suluhu la maisha kwa nyanja 
tofauti ikiwepo dini.  
Dini ni neno linalopatikana uarabuni  ‘Diin’ linalomaanisha ‘imani ya umoja wa mweyenzi 
Mungu’ desturi,tabia au mazoea. Kwa jumla neno hili husisitiza maana ya mwanadamu 
kuitambua nguvu kubwa kumliko na ambayo inautawala ulimwengu mzima na hasa Mungu au 
Miungu ya mtu binafsi kama mwongozo wa kiroho, kiimani  na kiibada. Dini ndio mafundisho 
ambayo huunganisha sana mwanadamu na Mungu au Miungu, yaani ni hatua na athari za 
kuunganisha tena Mungu na wanadamu. Neno dini linaweza kutumika kiishara kuashiria  kama 
shughuli au wajibu unafanywa kila wakati na kwa ukali.Mifano ya dini duniani ni ile ya Ukristo 
iliyo na waumini bilioni 2.1, ile ya Uisilamu yenye waumini bilioni 1.9 na ile ya Ubudha iliyo na 
waumini bilioni 1.6. Kulingana na vitabu vya kihistoria vya dini, dini zilizoimarika zilizionekana 
kwa mara ya kwanza baada ya  wa kazi, ukuzaji wa kilimo ambapo wakati mwingi ulitumiwa 
kutazama maumbile. Dini za Neolithic ziliundwa karibu na vitu vitatu; hekalu, kuhani na 
dhabihu(matoleo) ambayo pia ni kielelezo cha utambuzi wa takatifu na unajisi. 
Kazi ya dini ni kuimarisha mfumo wa maadili yanayohusu mshikamano wa kikundi cha jamii 
kulingana na mradi wa kawaida na kuunda kiwango fulani cha kuridhika kiroho kupitia imani 
kushida kuteseka na kufikia furaha.Dini zote zina misingi ya kihistoria zilizoitwa hadithi za 
uwongo zikieleweka kama hadithi zinazoelezea asili ya maisha, kuhalalisha hali yake na 
makadirio yake ya baadaye. Dini zote zinaungwa mkono na mikondo tofauti ya mawazo ambayo 
hujaribu kueleza sisi ni kina nani na kwa nini tumekuja ulimwenguni. Katika tamaduni zilizo na 
maandishi, dini zinategemea maandishi ya asili takatifu ambayo huleta wafuasi wao karibu na 
jamii moja ya kiroho.Kwa mujibu wa vitabu vya kihistoria, dini za kigeni zilisambazwa maeneo 
mengi ya dunia na Wazungu kutoka Bara la Ulaya na Waarabu kutoka Mashariki ya mbali kabla 
na baada ya zama za giza.. 

Yaliyoandikwa Kuhusu Mada 
 
Makoyo (2014),katika tasnifu yake anajadili jinsi elimu ya Kenya inavyotamausha wasomi kwa 
kuegemea kwenye dini ya Kikristo ambayo inaamini msomi kuwa na imani ya kila kitu bila ya 
kuuliza swali lolote. Kulingana na Makoyo ,kuamini huku kunawafanya watu washindwe 
kujitegemea kwa sababu wanahofia kufanya maamuzi muhimu maishani mwao kwa hofu ya 
kupata ghadhabu kutoka kwa Mungu. Hali hii inamfanya mwanadamu kujiona kama kiumbe 
kisicho na akili ya kufanya maamuzi yoyote na hivyo kumkatisha tamaa zaidi. Kazi hii ya 
Makoyo ni muhimu kwa mtafiti kwani inarejelea jinsi elimu ya taifa la Kenya inavyowakatisha 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 21



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA  RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA 

 

 

 

 

wasomi tamaa. Tofauti ya kazi hii na ya mtafiti ni kuwa kazi yake iliepuka utamaushi 
unaosababishwa na elimu na kujikita kwa sababu za kidini  zinazotamausha vijana, athari za 
utamaushi huu na njia zinazoweza kuangaziwa kuleta suluhu mwafaka za utamaushi huu 
miongoni mwa vijana. 
 
Nyamemba,R( 2016 ) Anasema kuwa , vijana wanapokosa kupata matarajio waliyokuwa nayo 
kwa nyanja mbalimbali kama vile elimu na ajira ,wengi wao hutamauka na kuamua kujitosa 
kwenye dawa za kulevya za kila aina zikiwemo bangi,ugoro na singara. Hali hii imewafanya 
wengi wao kukosa faida katika jamii. Kazi hii ya nyamemba inafafanua kuwa vijana wengi 
hukatishwa tamaa na ukosefu wa masuala ya kiuchumi kama vile elimu na ajira. Masuala 
yaliyoko kwenye kazi hii yalifaa mtafiti kwani yamejikita kwenye udhanaishi kama yake tu ila ni 
tofauti na utafiti wake ambao uliepuka masuala ya uchumi na badala yake kuegemea tamaa 
inayokatishwa na masuala ya imani za kidini miongoni mwa vijana huku sababu,athari na 
mapendekezo mwafaka ya hali hii zikiangaziwa. 
Matundura(2019)huku akimnukuu mwalimu wake wa chuo kikuu Bw.Crispine Isaboke,anasema 
kuwa pindi mtu anapozaliwa,moyo wake huwa kana kwamba umetiwa majira mithili ya saa na 
hajui hatima yake ila inajulikana na Mungu. Anadai kuwa chochote anachoamua mwanadamu 
kilipangwa pindi tu alipozaliwa na kuwa maamuzi yake yote hudhibitiwa na jaala jambo ambalo 
linatamausha kiumbe huyu zaidi.  Kazi hii inaangazia mwanadamu ambaye ametamaushwa na 
hali ya kufahamu kuwa maisha yake yote. hudhibitiwa na jaala na yashaapangwa tangu 
mwanzoni na kuwa hana uwezo wa kubadili chochote maishani kwani lililopangwa kwake ndilo 
humkuta maishani. Utafiti wa mtafiti uliangazia sababu za  masuala ya kidini zinavyotamausha 
vijana, athari zake kwa vijana hawa pamoja na mapendekezo ya kushughulikia utamaushi huu 
ambapo masuala mengi husababishwa na binadamu  mbali sio jaala. 

Wasike, K (2020) huku akinukuu riwaya ya Ua la Faraja katika tawasifu yake , mhusika 0molo 
alitamaushwa na maisha kiasi cha kuishi kwa muda mrefu bila kuoa. Omolo aliishi kwa kujiuliza 
maswali mengi kuhusu maisha,” Alishangaa kwa nini hata yule mwenye maisha ya shida 
anapoungua na kukaribia kifo ili hafurahi kuisha kwa shida zake akifa bali huhangaika kujitibu 
ili apone aendelee na shida zake (uk23) vile vile mhusika Queen haoni faida ya kuishi na hakuna 
haja kwa kutia bidii maishani kisha afe. Hili linakazwa na hali yake kuwa alikuwa na ugonjwa 
wa UKIMWI. Mtafiti wa kazi hii amezingatia utamaushi wa maisha kwa jumla unaowafanya 
wahusika wengine kukosa tamaa ya kufanya lolote maishani kwani mwishoni mna kifo. Kazi 
yenyewe itafaa mtafiti kwani  ina misingi ya mathara yanayosababishwa na utamaushi. Kazi ya 
mtafiti ilifafanua mathara haya kwa upana kwenye kipengele cha  utamaushi wa kidini huku 
yakiegemezwa kwa sababu zake na kisha kuangazia mapendekezo ya kukabiliana na hali hii tata. 
 
Abdallah,M.(2021) Anasema kuwa baada ya vita vya pili vya dunia,maisha yalionekana 
kutokuwa na maana kwa jinsi vita hivyo vilivyoangamiza mamilioni ya watu. Aidha maisha 
yalikuwa magumu kwa kuwa uchumi uliporomoka. Hali hii ya taabu ya kisaikolojia ,ilifanya 
watu wengi na hasa kutoka magharibi wadai kuwa Mungu amekufa kwa sababu kama angekuwa 
hai asingewaruhusu kuteseka na kuacha wengi waangamie kama ilivyotokea. Kazi ya Abdallah 
inaangazia utamaushi uliosababishwa na vita ambao uliathiri watu wa vitengo tofauti barani 
Ulaya.kazi hii itafaa mtafiti sana kwani inajadili kwa mapana suala la utamaushi. Tofauti na kazi 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 22



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA  RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA 

 

 

 

 

yake ni kuwa upande wake aliangazia utamaushi unaosababishwa na imani za kidini kwa vijana 
pekee katika jamii badala ya kuangazia wanaumri wote kwa jumla,sababu za hali hii 
kutokea,athari zake na kisha mapendekezo mwafaka ya kukabiliana na hali yenyewe. 
 
Adria Fuluge (2022) huku akiangazia riwaya ya Rosa Mistika katika jarida lake ,anajadili jinsi 
wahusika mbalimbali wanavyotamaushwa na maisha na kukosa suluhu kwa vitengo vyote 
ikiwemo dini hadi kufikia maamuzi ya kujiua. Ingawa kwa mkondo  na mchakato mrefu, Rosa 
anapitia hali nzito ya maisha akitafuta maana ya maisha na anapoona kuwa hakuna suluhu 
atakalopata anatamauka na kuamua kujitoa uhai. Rosa anafuraia kifo chake kwa sababu kwake 
huo ndio uhuru aliokuwa anautafuta kama suluhisho la taabu zake.(uk 161). Adria amejikita 
kwenye utamaushi wa wahusika wa umri tofauti na hasa wa jinsia ya kike.  
Kwa upande wa mtafiti alinuia kushughulikia utamaushi wa kidini miongoni mwa wahusika  
vijana wa jinsia zote huku akizamia kinachosababisha utamaushi huu, athari zake kwa vijana 
hawa pamoja na njia mwafaka zinazoweza kutumiwa kukabiliana na hali hii nyeti katika karne 
ya 21. 
 
Hivyo kutokana na kazi hizi zote bado kuna mwanya uliojitokeza na ndio maana utafiti huu 
ulinuia kuuziba kwa kuzingatia suala la utamaushi wa kidini na athari zake kwa vijana kwa 
mujibu wa riwaya ya Paradiso ya John Habwe na KidagaaKimemwozea ya Ken Walibora               

Muhtasari wa Riwaya ya Paradiso 
Riwaya ya Paradiso iliandikwa na John Habwe na kuchapishwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 
2005. Kulingana na TUKI 2013:451,neno ‘paradiso’ lina maana ya edeni,pepo au firdausi. 
Kulingana na TUKI 2013:458,neno ‘pepo’ lina maana ya mahali patukufu panapoaminiwa kuwa 
baada ya kufufuliwa na kulipwa matendo yao  mazuri walioishi kulingana na amri za Mungu 
wataishi milele.  Ingawa Paradiso ni riwaya yenye mkusanyiko mwingi wa maudhui,maudhui 
makuu kwenye riwaya hii ni yale ya Unafiki wa kidini unaoendelezwa na viongozi wa dini 
pamoja na waumini wake katika matukio mbalimbali yanayopatikana kwenye riwaya hii. Unafiki 
huu wa kidini unaotokea unaendelezwa na wahusika tofauti na kudhihirika kwa matendo kama 
vile ya;ufisadi,mipango ya kando,vita baina ya  waumini,chuki,anasa,biashara kwa jina la Mungu 
na kujitajirisha kwa kutumia Neno la Mungu miongoni mwa vitendo vingine. Matendo haya ni 
kinyume na mafundisho ya dini.  

Riwaya hii ya Paradiso imengawanyika katika sura kumi na nane zilizomo kwenye kurasa  230 
ambazo kila sura ina mvuto wake unaomfanya msomaji kuwa na ari ya kubukua kitabu 
chenyewe kujifahamisha zaidi kuhusu maudhui makuu ya unafiki wa kidini. Ingawa  dini 
hudhaniwa na jamii kama chombo cha usalama na afueni kwa ulimwengu 
uliovurugika,yanayojitokeza katika riwaya hii ni tofauti kabisa kwani baadhi ya viongozi wa dini 
na washirika wao wanatenda kinyume na matarajio na mafundisho ya dini. Maadili ya baadhi ya 
waumini yameoza kiasi cha kuwafanya vijana wanaozidi kuziduka kila uchao kukosa kuona 
maana ya kujihusisha na dini. Hata hivyo,riwaya hii ya Paradiso inadodoa maudhui mengine 
kama vile,Ndoa,Ukware,Nafasi ya kanisa kwenye jamii,Ufisadi, Tamaa, 
Elimu,Migogoro,Umaskini na Utabaka miongoni mwa maudhui mengine. Riwaya hii inaweza 
kuainishwa kama ya uhalisia kwani masuala yanayojadiliwa ndani ya kitabu yanalingana na yale 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 23



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA  RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA 

 

 

 

 

yanayoshuhudiwa kwenye ulimwengu wa kawaida tu. Maabadi zinawakilishwa na makanisa ya 
Bethany na lile la NewJerusalemu ilhali viongozi wakuu wa dini wanawakilishwa na Askofu 
Joshua na mkewe Kasisi Lona pamoja na Mhubiri Michael. 

 Muhtasari wa Riwaya ya KidagaaKimemwozea 
Riwaya ya KidagaaKimemwozea iliandikwa na Ken Walibora na kuchapishwa kwa mara ya 
kwanza mwaka wa 2012. Riwaya hii imegawanyika katika sura 10 zilizo kwenye kurasa 162. 
Ingawa riwaya hii ina masuala chungu nzima yanayojadiliwa na mwandishi,suala kuu lililopo 
kwenye kitabu hiki ni namna ndoto walizokuwa nazo Waafrika walipokuwa wakipigania uhuru 
zilipogeuka na kuwa jinamizi isiyotarajiwa.  Afrika inawakilishwa na taifa la Tomoko na eneo 
dogo la  Sokomoko linaloongozwa na Mtemi Nasaba Bora.Wazalendo na wanyonge waliokuwa 
mstari wa mbele kupigania uhuru na kumfukuza  mkoloni mweupe waligeukwa na viongozi wa 
kiafrika pindi tu uhuru ulipopatikana. Neno ‘Kidagaa Kimemwozea’ ni istilahi iliyotumika 
kuonyesha namna matarajio ya Waafrika yalivyotingwa na uongozi wa Waafrika wenzao kwa 
kukosa kutimiza ahadi zao na kutamausha nyoyo zilizokuwa na matarajio makuu baada ya 
uhuru. Kulikuwa na wanyonge waliowakilishwa na wahusika kama vile Imani,Amani,Matuko 
Weye,Uhuru na DJ miongoni mwa wengine ambao nyoyo zao zilitamauka kiasi cha kupatwa na 
msongo wa mawazo ulioathiri na kuvuruga akili zao. Familia za waliopigania uhuru kama vile 
Mwinyihatibu Mtembezi hazikuwa na chochote cha kujivunia ila kutaabikia kwenye nchi yao 
huru. Maudhui makuu kwenye riwaya hii ni yale ya Usaliti ambapo raia wanasalitiwa na 
viongozi wao kwa kupitishwa dhuluma za kila aina na hata wengine kuuawa pasipo na hatia. 
Raslimali zinazopaswa kuauni wananchi zinawakilishwa na maji ya Mto Kiberege ambapo 
badala ya maji haya kuleta uhai yanakisiwa kuwa ni maji ya mauti. Hadithi ya kitabu hiki 
inasawiriwa kupitia safari ya wahusika wawili Amani na Imani ambao wanaanza safari kutoka 
makwao kuelekea eneo la Sokomoko kusaka kazi ambazo labda zingeleta afueni kwa maisha 
yao. Wahusika hawa wanavunja mwiko kwa kunywa maji ya Mto Kiberege yaliyodhaniwa na 
wenyeji kuwa maji ya mauti. Kitendo cha kutoathiriwa na maji yale kinabadili dhana ya wakaaji 
wa Sokomoko na kuweka peupe kuwa hata haramu inaweza kuwa halali na halali kuwa haramu. 
Wanapofika katika kijiji cha Sokomoko, Amani na Imani wanaajiriwa na ndugu wawili;Mtemi 
Nasaba Bora na Mwalimu Majisifu mtawalia. Ingawa  waajiri hawa walikuwa dhalimu kwa 
Amani na Imani, vijana hawa wanafanya bidii za mchwa kwa kazi zao kwani nia yao ilikuwa 
kufanya upelelezi ili kugundua waliopoka mali ya familia zao. Inadhihirika kuwa jasho la 
wasomi hufaidi wengine kwani Mwalimu Majisifu ni mwizi wa miswada ya wasomi ambapo 
badala ya kuchapisha kazi za wasomi hawa,anawajulisha kuwa kazi zao ni chapwa na kisha 
kuzichapisha kwa jina lake na kuziuza. Hata hivyo,Amani na Imani wanaongoza umati wa watu 
na kuwazidua kuhusu haki zao walizonyimwa na viongozi wao. Kupitia kwao inadhihirika kuwa 
Mtemi Nasaba Bora ambaye anawakilisha viongozi wa Afrika baada ya uhuru ni mnyakuzi 
mkuu wa ardhi za wanyonge. Inadhihirika kuwa viongozi hubadili vyeti vya kumiliki ardhi na 
kuwapa wenyeji vyeti bandia kwa minajili ya kunyakua ardhi zao. Baada ya siri za Mtemi 
Nasaba Bora kuwekwa wazi anajiona ombwe tupu na asiyeweza kuishi kwa aibu miongoni mwa 
watu wake na kwa hivyo anaamua kujitoa uhai kwa kujitia kitanzi. Amani anayewakilisha 
wanamapinduzi anaongoza utawazaji wa mtemi mpya na kuahidi kuwa makosa yaliyotokea 
awali hayatarudiwa. Pia anawazidua raia kuwa macho kukabiliana na dhuluma yoyote ile 
ambayo ingezuka na kuendelezwa na kiongozi mwingine. Mabadiliko yanayoletwa Sokomoko 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 24



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA  RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA 

 

 

 

 

na Amani na Imani yanadhirisha kuwa hakuna jambo lisilowezekana Barani Afrika . wanyonge 
wakiungana pamoja wanaweza kuleta mageuzi makubwa na kubadilisha hali ya kiuchumi ya 
jamii zao. Riwaya hii pia ina maudhui mengine kama vile;ufisadi,unafiki wa 
kidini,dhuluma,ulevi,wizi na ukware miongoni mwa maudhui mengine. 

 

Athari za Udhanaishi wa Kidini kwa Vijana 

 Vijana Kuchoshwa na Utaratibu wa Maabadani. 
Maabadi ni mahali popote pa kufanyia ibada kama vile hekalu, kanisa au msikiti. Pia ni sehemu 
au eneo maalumu lililojengwa ambalo mtu au kundi la watu hukutana kufanya ibada au kujifunza 
masomo ya dini. Hata hivyo mnamo miaka ya hivi karibuni kumeibuka madhehebu ambayo 
hayafuati utaratibu wowote wa kufanya ibada zao kwa tetezi kuwa ibada inapaswa kuongozwa 
na Roho Mtakatifu. Hali hii imechosha vijana wa karne ya 21 na baadhi yao kuacha kuhudhuria 
ibada zenyewe na badala yake kujihusisha na starehe zao siku zilizotengwa za ibada. Suala hili la 
vijana kuchoshwa na taratibu za ibada limekuwa likiangaziwa na waandishi tofauti waliobobea 
na wale chipukizi. 

 John Habwe Katika riwaya ya Paradiso, anamwangazia kijana Kyalo aliyeichukia dini tangia 
akiwa kijana, sala za dini zilimchosha na aliona tu watu wengi walijihusisha na dini tu kwa 
sababu ya dhiki. Kyalo alichukia dini kiasi kwamba hata baada ya kuoa mke wake Salome 
alimwona mjinga kwa kujishughulisha na hadaa za wahubiri. Madai ya Kyalo yanadhihirika 
kwenye dondoo ifuatayo ; 

‘…Kyalo hakupenda masuala ya dini. Tangu alipozaliwa hakuwa amekwenda kanisani. 
Hakuonahajayoyoteyakujidhikinasalandefuambazozilichosha. Hakupendahasasalazakelele. 
Alinonakuwamkewakealikuwamjingakwakujishughulishanahadaazawahubiri’ (uk49) 

Kutokana na utafiti huu ni dhahiri shahiri kuwa Kyalo, anayewakilisha baadhi ya vijana katika 
jamii hakupenda kelele nyingi zilizopigwa na waumini wakati wa ibada na hivyo basi akafanya 
maamuzi ya kujiepusha na masuala ya dini. Hata alipokua na kuwa na familia msimamo wake 
ulibaki pale pale ; masuala ya dini haikuwa moyoni mwake kamwe. 

 Vijana wa Kike Kukataa Kuolewa na Wahubiri. 
Ndoa ni muungano kati ya watu wawili au zaidi unaokubaliwa na kuheshimiwa na jamii. Tukio 
la kuanzisha ndoa linaitwa harusi. Kabla ya ndoa, kuna kipindi cha uchumba ambapo watu hao 
wawili waliokubaliana wanachunguzana tabia na kujifunza au kujuana zaidi. Katika tamaduni 
nyingi duniani, uhusiano huu huwa ni kati ya mwanamume na mwanamke ila miaka ya hivi 
karibuni kumekuwa na msukumo wa jamii fulani hasa kutoka Ulaya na Marekani kufanya ndoa 
ya watu wa jinsia moja. Katiba ya Kenya kifungucha 4 ibaraya 9 kila aliyefikisha miaka kumi na 
nane ana haki ya kuolewa au kuoa na kuwa na familia. Hata hivyo, ndoa haipaswi kuwa ya 
lazima na kila mmoja anapaswa kujichangulia mchumba amtakaye. Miaka ya hivi karibuni ndoa 
imekumbwa na nyufa ambazo zinatishia kusabaratisha taasisi hii iliyoasisiwa na mababu zetu 
kabla ya karne ya ishirini na moja. Linalotilia msumari moto kwenye kidonda ni kuwa hata ndoa 
za wahubiri na viongozi wa dini zimekuwa na atiati na migogoro isiyokoma jambo ambalo 
linawafanya vijana na hasa wa kike kuwa na hofu ya kuolewa na viongozi wa dini. Katika 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 25



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA  RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA 

 

 

 

 

riwaya ya Paradiso, kijana wa kike Nice ambaye pia ni bintiye Askofu Joshua na kasisi Lona wa 
kanisa la NewJerusalemu, anakataa katakata pendekezo la wazazi wao kuolewa na mhubiri 
Michael. Maisha ya unafiki wa kidini aliyoyaona na wazazi wake. Nice alikata kauli ya 
kutoolewa na mhubiri liwe liwalo kama inavyoelezwa na dondoo iliyo hapa chini ; 

‘… Joshua na Lona walikaa hapo kumkabili Nice kuhusu pendekezo lao la kuolewa na 
Michael.Bila kificho Nice aliwaeleza hawezi. ‘’kwa nini mnitafutie mama, mama ?’’. ‘’Hebu 
sikiliza mama, huyo mume ni kufu yako, ni mtu wa dini na ni rika lako’’ alisema Lona…’’ Najua 
ni mtu wa dini, lakini mimi mama si mtu wa dini’’ Nice alisema kwa maringo’. (.uk 73)  

Usiku mzima Askofu Joshua na mkewe walimkorofisha binti yao angalau abadili msimamo 
wake na kukubali matakwa yao lakini Nice alibakia kwenye msimamo wake wa kutoolewa na 
mtu wa dini tena mhubiri. Nice alitamani kuachiwa uhuru wa maamuzi yake kama ataolewa au 
la. Alihofia kuolewa na mtu wa dini kwani alikuwa ameshuhudia mengi kwenye ndoa ya wazazi 
wake licha ya kuwa watumishi wa Mungu. Hata baada ya wazazi wa Nice kuwa na hasira na 
kumtishia binti yao kutafuta wazazi wengine endapo angekataa pendekezo lao la kuolewa na 
mhubiri Michael, Nice alisimama kidete kuwa yeye sio mtu wa dini na hataki kuolewa na mtu 
wa dini. 

 Kwa vile fasihi ni kioo cha jamii, utafiti huu unatambua Nice ambaye ni kiwakilishi cha vijana 
wa kike kwenye jamii ya karne ya ishirini na moja wanaodinda kuolewa na wahubiri kwa hofu 
ya kutiwa pingu na dini licha ya kulelewa na jamii ya viongozi wa dini. Wao wangetaka kuwa 
huru kutafuta waume zao bila kulazimishwa na wazazi wao. 

 Vijana Kushuku Uwezo wa Mungu. 
Kila binadamu duniani huamini kuwa kuna kiumbe mwenye nguvu na uwezo kumliko. Kiumbe 
huyu ndiye mpaji wa uhai na ndiye ajuaye uhai huenda wapi baada ya viumbe kufikwa na mauti. 
Jamii nyingi humpa kiumbe huyu majina tofauti ikiwemo Mungu, Maulana, Mola, 
RabanaKarima miongoni mwa majina mengine. Kiumbe huyu hudhaniwa na jamii ya 
mwanadamu kuwa na nguvu nyingi na uwezo wa kuamua hali ya baadaye na hatima ya 
mwanadamu huyu na hivyo mwanadamu humcha na kumheshimu mara nyingi. Kwa imani, 
kiumbe huyu hukimbiliwa hasa wakati kuna ugumu wa hali kwa imani kuwa ataleta suluhu na 
hali ya utulivu. Kwenye vitabu vitakatifu, Mungu hutajwa kama ngome ya kukimbiliwa wakati 
wa haja. Hata hivyo, vituko na kashfa miongoni mwa viongozi wa kidini kwenye madhehebu 
tofauti miaka ya hivi karibuni, zimefanya waumini wengi kushuku uwezo wa’ Mungu’ wa 
kubadili hali zikiwa na utata. Vile vile, matatizo yanayozidi kuongezeka kila uchao yakiwemo 
magonjwa, ajali, mauti na majanga ya kila siku yanazidi kufanya waumini wengi kushuku uwezo 
wa ‘Mungu’ wa kutuliza hali hizi. Vile vile, jamii inatarajia maombi na ibada zinazofanywa na 
waumini kila siku zifanye Mungu atulize hali ya mizozo iliyomo kwenye madhehebu 
mbalimbali. 

 Ken Walibora katika riwaya yake ya KidagaaKimemwozea, anamrejelea kijana wa kike Imani 
ambaye anashuku uwezo wa Mungu aliyeruhusu kufikwa na dhiki iliyompata pale nyumbani 
aliponusurika kuchomwa na wenye wivu. Madai ya Amani yanadhihirika kwenye dondoo hii; 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 26



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA  RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA 

 

 

 

 

‘Basiniliponusurikakuteketezwanilitokanikatazamambingunakuwazasana. 
KwaniniMungualiruhusudhikikamahiyokunikusa?’ (uk58-59)  

Maneno ya Imani ni kuwa Mungu mwenyewe hakuwa na uwezo wa kumlinda na hali ya maadui 
kutaka kumteketeza kwani hangekuwa na uwezo angemlinda kutokana na wahuni waliochoma 
nyumba yao na hangeruhusu wafike kwa boma lao. 

John habwe katika riwaya yake ya paradiso anamrejelea kijana wa kike lydia ambaye aliamini 
kuwa ana uwezo wa kufanya mambo mengi na kuwa mungu yuko tu anapokuwa hajiwezi. Haya 
yote yanajitokeza katika dondoo ifuatayo; 

’’Lydia haya ya dini yalimfutu. Hakuyafuatilia kwa karibu. Angewezaje huku mama yake ndiye 
huyo? Au ni kweli walivyosema mwana huiga kisogo cha nina. Lydia alijua kuwa Mungu yuko 
anapokuwa hajiwezi. Pale unapoweza unayafanya mwenyewe’’(uk97)  

 Utafiti huu unatambua kuwa kwenye mawazo ya Lydia ni kuwa Mungu anapaswa kuingililia 
kwa maisha ya mtu tu pale ambapo mtu huyo amelemewa na pale ambapo mtu huyo anaona 
anaweza basi anapaswa kujishughulikia. Yaani sio lazima mtu kutegemea Mungu kwa kila 
jambo. 

 Vijana Kukataa ‘Kuokoka’ na Kuingia kwa Anasa. 
Kuokoka ni kitendo cha kutoka sehemu moja iliyo na hatari na kwenda sehemu nyingine ambayo 
ni salama. Kulingana na SamuelMtimbike (2022), kwa dini ya Kikristo, kuokoka ni kuitii injili ya 
Bwana Yesu na kisha kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni wa maji mengi na kwa jina la 
Yesu na kupokea kipawa cha Roho mtakatifu na kisha kuishi maisha matakatifu kwa kufanya 
mapenzi ya Mungu. Kulingana na dini ya Kiisilamu, waliomkubali Mohamad na kufuata amri 
zake wamekwisha okoka na watapata Bustani zipitazo mito kati yake. Humo watadumu milele. 
Huku ndiko kufuzu kukubwa. Kulingana na mafundisho ya dini, wokovu ndio zawadi kubwa 
anayoweza kupata mwanadamu kwani inamhakikishia uzima wa milele Paradiso. Wokovu huu 
unahitaji kila muumini kuishi maisha ya utakatifu yasiyo na dhambi kulingana na mafundisho ya 
dini yake. Hata hivyo, jinsi siku zinavyosonga ndivyo waumini wengi na haswa vijana 
wanavyozidi kukaidi injili ya wokovu na badala yake kujiingiza kwenye ‘’dhambi’’ za kila aina 
zikiwemo ulevi, ukware, utovu wa maadili, anasa na starehe za kila aina kinyume na mafundisho 
ya dini zao. Kisa na maana, wanaowaongoza kwenye mafundisho haya ya kidini wanayatenda 
maovu haya wazi bila woga wa adhabu ya Muumba wao.  

Katika riwaya ya Paradiso, John Habwe anamrejelea kijana wa kike Nice bintiye Askofu Joshua 
na kasisi Lona aliyetoshwa na wokovu wa wazazi wake na kuzamia starehe zake za maisha kule 
NewYork. Salamu za Nice zililetwa nyumbani na Bwana Njenga aliyekutana naye kule NewYork 
katika shughuli zake za ukasisi. Bwana Njenga alipojaribu kumpa Nice habari za Yesu, Nice 
alimkumbusha kuwa baba yake ni mhubiri na kuwa hakuweza kumuokoa. Mwandishi anasema 
kuwa Nice alikuwa amejizika zii katika ulevi na matembezi. Ithibati ya utafiti huu imo katika 
nukuu ifuatayo ambayo ni mazungumzo ya Bwana Njenga na kijana wa kike Nice bintiye 
Askofu Joshua na Kasisi Lona; 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 27



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA  RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA 

 

 

 

 

‘Nice alikuwa amesahau kisomo chake. Alijizika ziii katika ulevi na matembezi…. 
Well,nilitakakukuulizaunakaawapi? Unaa…YaaninilitakaumkubaliYesu’’…’’Sikiza. 
Babayangunimhubiri. Hakufaulukuniokoa. Wewehutafaulu. 
Ninakoishinanikifanyachoyakuhusuvipi?’’BaadayamjadalahuukatiyaNicenaBwanaNjenga, 
Nicealichomokanjebilakuaganasuruariyakeyakubanaambayokuivuakwakealikuwalazimaangesai
diwa’. (uk128) 

Utafiti huu ulitambua kuwakijana wa kike Nice, alikuwa amechoshwa na ukosefu wa uaminifu 
kwa wazazi wake licha ya kuwa wao walikuwa watumishi wa Mungu na badala yake akazamia 
kuhamia NewYork alikoishi maisha ya ulevi na starehe alizotaka mwenyewe. Huu ndio uhuru 
alioutafuta maishani mbali za wazazi wake waliookoka. 

Vijana Kuzinduka na Kuuliza Maswali Kuhusu Dini Hadharani. 
Kuzinduka ni kitendo cha kutoka katika bumbuazi au kutoka katika hali ya kutoelewa jambo. 
Mtu yeyote anaweza kuzinduka kimawazo na kuwa na falsafa mpya kuliko aliyokuwa nayo hapo 
awali. Katika kipindi cha zama za giza, binadamu aliacha hali ya kimaumbile na jaala kuchukua 
mkondo wake bila kutia juhudi zozote za kudhibiti changamoto zilizotesa kiumbe huyu. Hata 
hivyo, baada ya kipindi cha ufufuo, binadamu alianza harakati za kujikomboa kutoka sirisiri za 
utumwa zilizomfunga kwa miaka nyingi zikiwemo zile za kidini, uchumi, teknolojia na ujinga 
wa kutosoma. Kiumbe huyu alianza kutafuta maarifa na ujuzi ambazo zingempunguzia taabu 
alizokubana nazo siku nenda siku rudi. Upande wa kidini, watu walifundishwa mafunzo na 
itikadi kali kwamba ili kumfikia Mungu ni lazima muumini yeyote apitie kwa Papamtakatifu. 
Kulingana na Ellen G. White (2023), mwanzo wa utawala wa KanisalaRumi ulikuwa mwanzo 
wa utawala wa giza na jinsi uwezo wa kanisa ulivyoogezeka ndivyo pia hali ya giza 
ilivyoongezeka. Anasema kuwa Imani ya wengi kuwa Yesu mwana wa Mungu ndiye mwazilishi 
wa kanisa iligeuzwa na badala yake papa na maasikofu aliowapa mamlaka kuadhimishwa.  

John Habwe kwenye riwaya yake ya Paradiso, anarejelea kiongozi wa kikundi cha vijana pale 
kwenye kanisa la Bethany lililoongozwa na kasisi Michael. Uhusiano wa Michael na Patricia na 
kukosa kuwa mwaminifu katika ndoa yake na Lydia, kuliwapa vijana nafasi ya kuzinduka na 
kuuliza hadharani kuhusu matumizi ya misaada iliyotoka ng’ambo na usimamizi wa nasari 
iliyokuwa chini ya kanisa jinsi inavyojitokeza kwenye nukuu iliyo hapa; 

‘TayarimwanyauliingiaBethany. Kuna kikundi kilichoona hakikufaidi vizuri pale Bethany. 
Kikundi hiki kiliongozwa na Kariuki. Kariuki alikuwa kiongozi wa vijana kaika kanisa la 
Bethany. Kikundi cha vijana 
kilidaimisaadayoteiliyotokang’amboilikuwakatikamikonoyawachache. 
PiausimamiziwashuleyanasariyaBethanypiaulifaidiwachachesana. 
Ummamkubwauliodundulizakuijengahaupatichochote. 
Walimuwashuleyanasariwaliopaswakutokahumokanisanihawajuisikuhiziwanatokawapi?’ 
(uk153.) 

Utafiti huu unatambua kuwa vijana wa jana ni tofauti na wale wa sasa kwani wale wa sasa 
hawana woga tena na pindi waonapo jambo lenye utata wanalikashfu moja kwa moja. Ndio 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 28



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA  RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA 

 

 

 

 

maana Kariuki, kiongozi wa vijana katika kanisa la Bethany anaongoza vijana wenzake kuuliza 
maswali peupe bila woga wowote kinyume na ilivyokuwa hapo awali. 

 Vijana Kuacha Kuhudhuria Ibada. 
Ibada ni kitendo chochote kinachofanywa kuonyesha unyenyekevu wa hali ya juu, utiifu, 
heshima, shukrani na utukufu aidha kwa Mungu au kitu kilicho na mamlaka makuu kuliko 
binadamu. Dini zote duniani huwa na ibada zinazofanyiwa mahala teule labda kwenye majengo 
ya kifahari au kachara, chini ya miti, mapangoni, juu ya miamba au hata misituni. Maabadi haya 
huheshimiwa na huwa muhari kila mmoja katika jamii ahudhurie ibada kulingana na muda na 
wakati uliotengwa. Hata hivyo, vijana wa karne ya ishirini na moja wamekuwa na mahudhurio 
duni ya ibada kwa tetesi kuwa matakwa yao hayatiliwi maanani na viongozi wa maabadi na 
haswa wazee.  

 John Habwe katika riwaya yake ya Paradiso, anarejelea mahudhurio duni ya vijana katika 
kanisa la Bethany baada ya kiongozi wa kanisa hili Michael kupatikana na kashfa ya uhusiano 
wa nje ya ndoa na Patricia licha ya kuwa na mke wake mwanadini Lydia. Haya yanadhihirika 
katika maneno yafuatayo; 

‘’JapobadokulikuwanawauminilukukiBethanyhasawalewaliofuatamiujiza, 
kundikubwalilinyofoanakujiondokea. Ahadizilipotolewabilamafanikiohapakuwanasababu 
yakuendeleakuning’iniaBethany.Kundilavijanatayarililijibambuakamagomelagogo.’’(uk160).  

Utafiti huu unadhibitisha madai kuwa vijana wanazidi kuchoshwa na masuala ya dini na 
wanazidi kuyakimbia na kujipa shughuli zao. Hii ni baada ya vijana hawa kutambua kuwa 
viongozi wa kidini wanaowaongoza wamejawa na kashfa chungu nzima. Wanaamua kujiondoa 
mmoja baada ya mwingine. 

 Vijana Kuwa na Ukakamavu wa Kudharau Watumishi wa Mungu Peupe. 
Watumishi wa Mungu ni viongozi waliotwikwa mamlaka ya kuongoza ibada katika madhabau 
ya waumini. Kila dhehebu duniani huwa na viongozi wake wanaopaswa kuheshimiwa na 
kusikizwa kwani ndio hutwikwa jukumu la kufundisha mafunzo ya kidini kulingana na mila na 
itikadi za dini husika. Vile vile, watumishi hawa wa Mungu wanapaswa kujiheshimu na kuwa 
waangalifu kwa maneno na matendo yao kwani chochote wanachosema au kutenda hadharani 
hutiwa kwenye mizani na waumini walio chini yao. 

Hata hivyo, watumishi hawa wa Mungu wanazidi kujihusisha na vituko vya kila aina ikiwemo 
kulaghai waumini kwa jina la Mungu, kufanya miujiza bandia, kuwa na mipango ya kando na 
kashfa za pesa miongoni mwa kashfa zingine. Vituko vyao vinazidi kuwapunguzia heshima na 
kufanya waumini na haswa vijana waliozinduka kuwadharau hadharani. 

John Habwe katika riwaya yake ya Paradiso, anawarejelea vijana wanafunzi wa shule ya upili ya 
Alliance Girls wanaodharau mtumishi wa mungu na mke wake Michael, Lydia. Hii ni baada ya 
vijana hawa kughudua kuwa Patricia analea mimba ya mhubiri na mume wake mwalimu wao. 
Walianzisha dharau kwa mwalimu wao kwa kutupa vijikaratasi hapa na pale kukashfu vitendo 
vya mume wa mwalimu wao aliye mtumishi wa Mungu kwenye kanisa la Bethany. Idhibati ya 
dharau hili ipo kwenye dondoo ifuatayo; 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 29



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA  RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA 

 

 

 

 

‘HatailipojulikanawazikuwaPatriciaanaleamimba, shulenzimahatawanafunziwalijua. 
Lydiaamebakiapalenarafikiwachache. Walimuwenginiwakumsengenyaakipita. 
Sasayeyeameamuaakaekando. 
KamahanajambolamnopaleshulenialikwendaBethanykusaidianakazi. 
Wanafunziwameandikavikaratasikusambazailikumkashfukuhusuvitendovyamumewe. 
LabdahilindilolililomtepuaLydiatenamoyowake. 
SasaaliposikiakuwaPatriciaamelazwaakaonawenzakewataendelezakashfanakumsemaovyoovyo.’ 
(uk204) 

Utafiti huu unakumbana na ukweli kuwa mtumishi wa Mungu na pia mwalimu Lydia 
anakumbana na hali nzito pale shuleni kwani hana uso wa kutazama wanafunzi hawa wanaosema 
ukweli wa jinsi hali ilivyo kuhusu ndoa yake na mume wake Michael. Anapunguza maneno yake 
na kuondoka shuleni pindi tu vipindi vyake vya masomo vinapokamilika. 

Vijana Kukataa Kazi ya Mungu Peupe. 

Kazi ya Mungu ni kitendo cha kutoa huduma iliyo au isiyo na malipo kufanya kazi ya Mungu. 
Kila dhehebu huwa na nafasi yake ya utumishi wa kazi ya Mungu kulingana na kanuni zao. Kwa 
yeyote kuwa na nafasi ya utumishi huu anapaswa kuwa na elimu fulani ya kithiolojia kulingana 
na kitengo ambacho angependa kuegemea. Ili kupata nafasi ya kutoa huduma husika ni lazima 
kufuata masharti fulani yaliyowekwa kulingana na kanuni za dhehebu husika. Katika karne ya 
21, idadi ya vijana katika utumishi wa Mungu imepungua jambo ambalo linazidi kutia wazee na 
viongozi wa madhehebu kiwewe kila uchao. Tafiti na maandishi mengi kwenye masuala ya dini 
zinadhirihisha kuwa vijana wanazidi kukataa utumishi wa Mungu na kuwa washirika tu 
wasiodhibitiwa kikamilifu na dini. 

Ken Walibora katika riwaya yake ya KidagaaKimemwozea, anamrejelea kijana Mwalimu 
Majisifu Majimarefu aliyefadhiliwa na Misheni kwenda ng’ambo kusomea ukasisi ili kurithi 
viatu vya baba yake ya ukasisi. Majisifu anapoenda ng’ambo anaghairi mtazamo huu wa kazi ya 
Mungu na kuamua kuishi maisha yake yasiyo na uhusiano na kazi ya Mungu jinsi inavyojitokeza 
katika nukuu hapa chini; 

‘Mwalimu majisifu alitarajiwa kusomea ukasisi ili aandame nyayo za babake. Lakini alipofika 
huko lipo lilimchusha akatoshwa na dini. Dini kwake ilikuwa kasumba iliyoulewesha umma 
ukalewa chakari na kupepesuka…. Aliona kwamba ingawa dini zote huhubiri Amani, udugu, na 
rehema, ila maovu na makuruhu mengi katika historia ya mwanadamu mathalan husuda, uongo, 
usongombwingo na vita yametendwa katika jina la Mungu. Kwa hivyo akaghairi nia ya kuwa 
kasisi’. (uk27). 

Utafiti huu unatambua kuwa ingawa watumishi wa Mungu wana nia nzuri ya kurithisha utumishi 
huu kwa watoto wao, kuna mambo nyeti yanayotinga hamu ya vijana hawa kuendeleza azma ya 
wazazi wao. Licha ya kuwa kasisi na baba yake Mwalimu Majisifu angetamani mtoto wake 
aiendeleze kazi ya Mungu kwa kufuata nyayo zake, kijana huyu alighairi nia hii kwa kutambua 
kuwa dini imejawa na unafiki mwingi na matendo mengi maovu yanafanyika kwa jina la Mungu. 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 30



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA  RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA 

 

 

 

 

Vijana Kutafuta Miungu na Ibada Zingine. 
Miungu ni jina linalojumlisha wahusika wanaoabudiwa katika dini mbalimbali kama wenye 
nguvu na enzi juu ya maisha ya mwanadamu. Tangu kipindi cha Neolithic, binadamu katika 
dunia wamekuwa wakifanya ibada za miungi tofauti kulingana na kipindi fulani cha mwaka. 
Kulikuwa na miungu ya wakati wa mavuno, wakati wa kiangazi, wakati wa mafuriko, baada ya 
majanga kutokea na kadhalika. Hata hivyo jinsi siku zilivyosonga ndivyo akili za waumini 
zilivyobadilika na kuelekeza ibada zao kwa Mungu mmoja kulingana na makubaliano. 
Kulingana na GasperMadumla (2014), jinsi dunia ilivyosonga ndivyo ongezeko la dhambi 
lilivyozidi na kumfanya mwanadamu kugeukia katika aina mbali mbali za ibada na hapo 
kukatengenezwa aina kubwa tatu za ibada ambazo ni; ibada kwa Mungu aliye hai, ibada kwa 
miungu ya jadi, mizimu, matambiko na mashetani na ibada kwa mwanadamu, vitu, fedha na 
mali. Katika karne ya 21, baadhi ya wanajamii na haswa vijana wamejikita katika uhuru wa 
kuabudu chochote watakavyo zikiwemo anasa na starehe zao. Waandishi tofauti wamekuwa 
wakiangazia waumini wanaoamua kuabudu vitu tofauti na kutumia mitindo tofauti ya maisha 
kulingana na matakwa yao. 

 Ken Walibora kwenye riwaya yake ya KidagaaKimemwozea, anamrejelea Mwalimu Majisifu 
ambaye baada ya kuchoshwa na Mungu na ibada za maabadi aliamua kuwa na mungu wake 
‘pombe’ na ibada yake ikawa ‘ulevi. Madai hayo yanajitokeza kwenye dondoo iliyo hapa; 

‘‘…lakinihatimayealikuwamwalimutuwashuleyaupili. 
Nalauasingekuwanawanaomjuawenyesatua, asingalikuwahatanaualimuhuo. 
Mamboyakeyalikuwataibuhadialipoanzakuabudu ‘Mungu’mwinginekwahimdinatwaa. 
Pombeilikuwamunguwakenaulevindioibadaaliyoipendakwadhatiya moyo’’. (Uk28). 

Utafiti huu uling’amua kuwa hata baada ya kijana mwalimu majisifu kukua na kuoa mke wake 
Dora, alizidi tu na ibada yake bila hofu kwani aliamini kuwa huu ndio uhuru aliopaswa kuwa nao 
binadamu yeyote wa kuachiwa mwanya wa kufuata sera zake bila kuingililiwa na yeyote.  

Mwalimu Majisifu anakosa kuhudhuria mkutano wa kusherehekea uhuru wa taifa la Tomoko 
kwenye uwanja wa Sokomoko kisa na maana alikuwa ameenda ibada jinsi ilivyo kwenye 
maneno yafuatayo; 

‘Majisifumbonasikukuonamkutanoni?’’ 
BwanaMtemialimuulizanduguyehatimayebaadayakimyachakitambokirefu…’’Nilikuwanimekwen
daibadakaka.’’ ‘’Temboitakuuanduguyangu. Punguzaulevibwana. 
Unautukanishaukoowetumtukufu. Sikuhizihatanaonaaibukukuitanduguyangu. 
Niliambiwajanakwambaulilalamtaronisikuileyashereheusikukucha. Hiiniaibubwana. 
Kumbukamarehemubabayetualikuwakasisinduguyangu. 
Alikuwaakisemakwambawalevihawataingiakatikaufalmewambinguni’’ (uk93.) 

Utafiti huu ulitambua kuwa Mwalimu Majisifu alikuwa tayari akeshajitafutia ibada yake ya ulevi 
tangia ujanani wake licha ya baba yake kumtaka awe kasisi kama yeye. Hivyo basi akahasi 
Mungu na Ibada za babake na kufanya maamuzi kuwa pombe ndiyo mungu wake na ulevi ndio 
ibada yake daima. 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 31



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA  RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA 

 

 

 

 

 

Njia Mbadala ya Kukabiliana na hali hii ya Udhanaishi  
John Habwe na Ken Walibora wanapendekeza baadhi ya njia zinazoweza kutumika ili kujenga 
imani katika mioyo ya vijana kuhusu masuala ya dini kwa lengo la kupunguza ukataji wa tamaa 
unaojengekeka kwao kila uchao.  Baadhi ya mapendekezo yaliyomlikwa na waandishi hawa ni 
pamoja na shughuli za ibada kuendeshwa kwa utaratibu wa pole pole na uungwana. katika 
riwaya ya Paradiso, baada ya mhubiri Michael kutoka Marekani, alifika na maoni kuwa 
shughuli za kanisa zilifaa kuendeshwa kwa utaratibu wa pole pole na uungwana bila kelele na 
kucheza kwingi kama kwamba leo dini ni disko. (uk 97-98) 

 Pili ni kutumia maafisa wa polisi na askari kwenye sehemu za maabadi ili kutuliza ghasia 
zinapozuka miongoni mwa washirika. Hii ni kwa sababu uwepo wa maafisa hawa utawafanya 
vijana kuwa na imani kuwa wanaoazimia kuleta fujo kwenye sehemu hizi za maabadi watakuwa 
na hofu na hivyo kufanya ibada kwa utaratibu. Katika riwaya ya Paradiso, maafisa wa polisi 
wanafika kuzima fujo na kutenganisha vikundi vilivyokuwa vikipigana katika kanisa la 
NewJerusalemu ambapo watu kadhaa walikuwa wameumizwa kwenye vurumai zilizotokea. 
(uk77). Maafisa hawa hawa wa polisi ndio waliotumiwa kuchunguza kashfa ya biashara ya 
mihadarati na madini iliyoendeshwa katika kanisa la NewJerusalemu (uk 198).  

  Vile vile, katika riwaya ya KidagaaKimemwozea, askari wa Mtemi Nasaba Bora wanalazimika 
kuzima ghasia zilizokuwa na vita baina ya makanisa mawili yaliyopigana kadamnasi sokoni juu 
ya uwanja wa kujenga maabadi ambapo kama haingekuwa askari hao wanamakundi hawa 
wangeuana waangamizane (uk 93). 

Njia ya tatu ni kutumia mahakama kutoa maamuzi ya ni wapi palipo na makosa vurugu 
zinapotokea. Katika riwaya ya Paradiso, ilibidi kanisa la NewJerusalemu kufungwa miezi minne 
kungojea mahakama kuamua ni nani anamiliki nini katika majengo ya maabadi(uk77). 
Mahakama pia inatumika kusikiza kesi kuhusu biashara ya ulanguzi wa mihadarati 
inayoongozwa na wa kanisa la mhubiri Boribori pale New Jerusalemu.Mahakama hii inatumika 
kumfunga Boribori na mkewe Judy kwa nia ya kusafisha magugu maabadani ili kujenga imani 
mpya kwa washiriki. (uk 217) 

Njia nyingine ya kujenga imani ya kidini miongoni mwa vijana ni kurekebisha tabia na 
mienendo ya washirika iwapo wangeendelea kumhubiri Bwana na kumfanyia kazi. katika riwaya 
ya Paradiso, Mhubiri Michael anasisitiza kuwa endapo wanaodai kuwa wameokoka 
wangejitayarisha katika ulimwengu kwa maisha ya ahera hawana budi kurekebisha na kubadili 
mienendo yao kwa kuhasi mauaji, ubakaji, wizi, ufisadi na kashfa zingine zilizoitanishwa na 
waumini la sivyo walio nje watazidi kuambaa masuala ya dini. (uk 56) 

Vile vile, waandishi hawa wanapendekeza kupunguza muda unaotumika kufanya ibada na 
kutumia lugha inayoeleweka na kila mwanaibada. Vijana wengi huchoshwa na muda mwingi 
unaotumika katika ibada haswa mahubiri. Kwenye riwaya ya Paradiso, mhubiri Michael wa 
kanisa la Bethany, alipunguza mahubiri yake kutoka saa moja hadi dakika kumi na tano. 
Anapoamua kutumia kiingereza, Bwana Kitwana huwa mkalimani wake ili kuwafikia watoto, 
wanawake, wanaume, vizee, wagonjwa na wazima walioujaa ukumbi wa Bethany. (uk 160) Pia, 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 32



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA  RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA 

 

 

 

 

wazazi wanapaswa kuwaasa watoto wao wakiwa wadogo na kuwaadilisha njia ambazo 
wangefuata ili kukua kwa uangalifu usioterereka. Hii ni kwa sababu mwalimu wa kwanza wa 
mtoto ni mzazi au mlezi wake na kuwa kwa asilimia pana mtoto hukua kulingana na mienendo 
ya mazingira aliyolelewa. Katika riwaya ya Paradiso, Patricia alikumbuka maneno alomweleza 
mamake Wanjiro alipopata mtoto wa pili. Patricia alionywa na mamake vikali dhidi ya kumvulia 
mtu yeyote nguo mpaka atakapoingia katika ndoa halali. Mama huyu alimfundisha bintiye kuwa 
asijipendekeze kwa mume yeyote kwani kujipendekeza kwa mwanamume ndiko kufukuzwa 
huko. (uk171-172) Mama huyu alimkumbusha bintiye kuwa yeye bado ni mtoto kwani hakuwa 
na uwezo wa kutenganisha haramu na halali. ‘Kwanguhutakuwamtumzima. Mtu mzima ni mimi 
mama yako niliyekuzaa na unayepagaza. Kama ungekuwa mtu mzima ungejua uharamu ulioko 
kutembea na mtu asiyekupenda akakutia mimba na kisha…’’ Wanjiro alighafilika kumaliza’. 
(uk176) 

Wosiakamahuu kwa vijana ungewaadilisha na kujenga misingi yao katika mafundisho ya kidini 
na hivyo basi kupunguza anasa, mipango ya kando na unafiki wa kidini miongoni mwa 
washirika na hivyo kuvutia vijana kwenye Imani yake.  Viongozi wa kidini na wahubiri 
wanapaswa kubadilisha mkondo wa injili kutoka kwa matoleo ya kila siku na badala yake 
kuhubiri jinsi binadamu anapaswa kuishi na binadamu mwenzake.                                                    

Hii ni kwa sababu pasipo na haki na umoja wa washirika hata maabadi yenyewe hayataweza 
kusimama imara. Katika riwaya ya Paradiso, baada ya Mchungaji Boribori kufungwa jela, Nana 
aliyechukua mahali pake aliweka mkondo mpya wa injili. Injili yake ilitoka kwenye ‘zaka na 
maendeleo’ hadi kwenye ‘kwenenda kwa haki na kupendana kwa majirani’. Kulingana na Nana, 
subira ilikuwa muhimu ili kupata ahadi za Bwana maanake Bwana Mungu alikuwa na saa yake 
na mikakati yake ya kufanyia mambo ambayo haikuwa lazima kwenda sambamba na ya 
wanadamu. Baadaye waumini walianza kuona ukweli katika injili ya Nana na baadhi ya 
waliokuwa wamegura walirejea na wageni kutoka ulimwengu na makanisa jirani wakaanza 
kufurika kwenye kanisa la NewJerusalemu. (uk 226) Hii ina maana kuwa waumini vijana wengi 
hukosa imani kwenye dini kutokana na matoleo ya mara kwa mara na endapo mkondo wa injili 
utabadilishwa watarejea maabadani kwa moyo wa dhati. 

Hitimisho 
Kulingana na utafiti uliofanywa ni ukweli usiofichika kuwa kuna masuala chungu nzima 
yanayofanya vijana watamaushwe na masuala ya kidini kila uchao. Kwa vile hamna lolote lisilo 
na athari zake, utamaushi huu una athari maridhawa kwa vijana hawa hali ambayo ikikosa 
kutafutiwa suluhu mwafaka itakuwa na athari mbaya kwa masuala ya ibada za siku za 
kesho.Mapendekezo yaliyo hapo juu yanaweza kutumika kupiga hatua kujitahidi kushughulikia 
kiwewe cha vijana kutamaushwa na mafundisho ya dini yanayojikita katika mafundisho ya 
maadili katika jamii. 

 

 

 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 33



IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH  
 ( ISSN 2811-2466 )                                                                Jackline Njeri Murimi* 
https://ijojournals.com/                                        Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || 

ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA  RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA 

 

 

 

 

MAREJELEO 

Camus, A(1984). The Rebel: Hamish Hamilton, Loudon. 
 
------------(1961)Resistance, RebellionandDeath.Translated by Justin O’Brien. New York:Knopf 
 
Habwe, J. (2000). MaishaKitendawili.Nairobi.Jomo Kenyatta Foundation 
 
-------- (.2005).Paradiso.Nairobi; The Jomo Kenyatta Foundation. 
 
International Bible Society (1973). HolyBible:New International Version.New York. 
 
Katiba ya Kenya (2010).GovermentPrinters.Nairobi 
 
Makoyo,M.S. (2014). ‘‘A Critique of Christian Education for Self Reliance in Kenya i light of 
Existentialism’’.Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Nairobi.(Haijachapishwa) 
 
Mbithi,J. (1969). .AfricanReligionsandPhilosophy.London:Heinman Education Books Ltd. 
 
Mohamed S.A. (1995). Amezidi. East African Educational publishers. Nairobi. 
Nkonge,G.(2006). “ Athari za Udhanaishi katika KichwaMaji na NguvuzaSala” Tasnifu ya 
Uzamili, Chuo Kikuu cha Nairobi( Haijachapishwa) 
 
Nyamemba,(2012).‘Uchanganuzi Linganishi wa jinsi waandishi katika TunuyaUshairi 
wanavyoshughulikia masuala ya vijana”  Tasnifu ya Uzamili ,Chuo Kikuu cha Nairobi  
( Haijachapishwa) 
 
TUKI, (2012). Kamusi ya Kiswahili Sanifu (Toleo la 3)Nairobi. Oxford University. 
 
Walibora,K .(.2012). KidagaaKimemwozea,Nairobi;Target Publication Limited 
 
----------------(2006). KufaKuzikana .Nai robi;Target Publications 
 
 

IJO JOURNALS

Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 34


	IKISIRI
	Utangulizi
	Yaliyoandikwa Kuhusu Mada
	Muhtasari wa Riwaya ya Paradiso
	Muhtasari wa Riwaya ya KidagaaKimemwozea
	Athari za Udhanaishi wa Kidini kwa Vijana
	Vijana Kuchoshwa na Utaratibu wa Maabadani.
	Vijana wa Kike Kukataa Kuolewa na Wahubiri.
	Vijana Kushuku Uwezo wa Mungu.
	Vijana Kukataa ‘Kuokoka’ na Kuingia kwa Anasa.
	Vijana Kuzinduka na Kuuliza Maswali Kuhusu Dini Hadharani.
	Vijana Kuacha Kuhudhuria Ibada.
	Vijana Kuwa na Ukakamavu wa Kudharau Watumishi wa Mungu Peupe.
	Vijana Kutafuta Miungu na Ibada Zingine.

	Njia Mbadala ya Kukabiliana na hali hii ya Udhanaishi 
	Hitimisho

	MAREJELEO

