IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI Jackline Njeri Murimi, Chuo Kikuu cha Tom Mboya na Jude Muli Mukuta, Chuo Kikuu cha Mount Kenya IKISIRI Masuala ibuka ni mambo yanayoangaziwa na kupewa kipau mbele katika jamii ya leo na aghalabu yalipuuzwa katika miaka ya zamani. Fasihi kama zao la wakati hubadilika jinsi jamii inavyobadilika ili iyamulike masuala mapya yanayoibuka katika jamii husika. Masuala haya ni pamoja na usawa katika jamii, haki za binadamu na mengine mengi. Utafiti huu umelenga kuonyesha jinsi haki za watoto zinavyokiukwa katika fasihi kupitia riwaya mbili teule ambazo ni:Chozi la Heri (2017) ya Assumpta K.Matei na Nguu za jadi (2021) ya Clara Momanyi. Ili kukamilisha lengo hili kuu, malengo mahususi matatu yalizingatiwa.Malengo hayo ni pamoja na; Kujadili jinsi ukiukaji wa haki za watoto unavyojitokeza katika riwaya teule,kutathmini madhara yanayotokana na ukiukaji wa haki za watoto katika riwaya teule na kuchanganua njia mbadala zinazoweza kutumika ili kuondoa ukiukaji wa haki za watoto katika jamii. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhalisia ambapo mihimili ya nadharia hii ilitusaidia kufikia malengo ya utafiti huu.Utafiti huu ulichukua muundo wa kimaelezo. Data ilikusanywa kule maktabani pale ambapo riwaya teule zilisomwa pamoja na tasnifu mbalimbali ili kurutubisha utafiti. Data ilichanganuliwa kwa njia ya kimaelezo kwa kuzingatia malengo na maswali ya utafiti pamoja na nadharia ya uhalisia.Uteuzi wa kimakusudi ulitumika katika utafiti huu kuteua riwaya ya Chozi la Heri na Nguu za Jadi. Utafiti huu utasaidia katika kuibua mapendekezo ambayo yatasaidia watengenezaji sera wanaojihusisha na suala la ukiukaji wa haki dhidi ya watoto,vilevile,utafiti huu utakuwa na mchango mkubwa katika taaluma ya elimu kwani utaihamasisha jamii kuhusu dhima ya fasihi ikiwemo kuyamulika matatizo yanayotokea katika jamii na kuyatafutia suluhu. Zaidi ya hayo, utafiti huu utawanufaisha waandishi wa kazi za fasihi kwani utawasaidia katika kutambua masuala nyeti katika jamii na namna ya kuyatatua. Usuli wa mada Fasihi ni sanaa inayotumia lugha kwa ubunifu wa juu ili kuelezea ujuzi wa viwango mbalimbali vya wanajamii anamoishi msanii. Njogu na Chimerah (1999),wanadai kwamba,kazi za fasihi huwasilisha mivutano, mikinzano, hali na maingiliano mbalimbali ya maisha ya mwanadamu na mazingira anamoishi. Msanii yeyote wa kazi ya fasihi huchota jumla ya mawazo anayotaka kuangazia kulingana na hali halisi za kisasa zinazomzunguka kiteknolojia,kiuchumi na kitamaduni.Ni kupitia kazi hizi ambapo tunapata taswira kamili ya jamii.Kwa jumla,fasihi kama sanaa ni zao halisi la jamii na haiwezi ibuka kutoka ombwe tupu.Masuala yanayoibuliwa katika IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 1 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI Chozi la Heri ya Assumpta K. Matei na katika Nguu za jadi ya Clara Momanyi haswa suala la ukiukaji wa haki dhidi ya watoto ni taswira kamili ya jamii ya kisasa. Hunt (1994) anaeleza kuwa mtoto ni kiumbe ambaye bado hajakomaa kiakili na umri wake upo chini ya miaka kumi na minane.Mtoto anafaa kulindwa dhidi ya dhuluma za aina yoyote.Kulingana na katiba ya Kenya (2010) mtoto ni mwanadamu yeyote aliye na umri wa chini ya miaka kumi na minane.Vilevile,Shirika la Afya Duniani (WHO) linamsawiri mtoto kama mtu ambaye umri wake uko chini ya miaka kumi na tisa. Kila mtoto, bila kujali umri wake,rangi,jinsia au mahali alipozaliwa ana haki.Haki hizi zimewekwa katika sheria za kimataifa katika mkataba wa haki za mtoto (CRC).Mkataba huu unatambua kwamba watoto wote lazima watendewe haki kwa usawa na kwa utu.Sheria za mkataba wa haki za mtoto hazina ubaguzi na huwa kwa manufaa ya mtoto kila mara.Haki hizi zinajuimsha haki ya kujieleza na kutoa maoni,haki ya usawa,afya,elimu,mazingira safi,mahali salama pa kuishi na kulindwa dhidi ya kila aina ya madhara.Haki hizi zimeainishwa katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Mtoto wa 1989 (UNCRC), mkataba wa haki za binadamu ulioidhinishwa zaidi duniani. Haki za watoto ni mojawapo ya masuala ibuka ambayo yamekuwa wakishughulikiwa na waandishi mbalimbali haswa katika karne hii ya ishirini na moja.Kwa kipindi kirefu,watoto wamekuwa wakipuuzwa katika jamii na haki zao kukiukwa jambo ambalo limewapata waandishi mbalimbali hamu ya kumlika suala hili kupitia kazi zao za fasihi. Aries 1962 na Radbill 1968 wanadai kuwa ushahidi wa kihistoria unaonyesha kwamba,ukiukaji wa haki za watoto umekuwepo tangu mwanzo.Watoto wamekuwa wakidhulumiwa na asasi mbalimbali za jamii zikiwemo utamaduni na dini.Madai haja yanaungwa mkono na (Burges 1979) anayesema kwamba, wazazi wamekuwa wakiwadhulumu watoto wao kwa muda mrefu sana.Wakati wa zamani, nchini Roma na jamii nyingi za Kiafrika ziliwasawiri watoto kama mali ya wazazi wao pale ambapo watoto hawa waliweza kuuawa au kutendewa maovu na wazazi wao bila kuchukuliwa hatua yoyote ya sheria (Cicchetti 1980).Wazazi wengi hupata motisha ya kuwadhulumu watoto wao kwa madai kuwa Biblia inapendekeza adhabu kali itolewe kwa watoto kama njia ya kuwaokoa kutokana na moto (Methali 23:13-14). Ukiukaji wa haki dhidi ya watoto,limekuwa tatizo sugu ambalo limesababisha kukatizwa kwa ndoto za watoto wengi duniani haswa kutokana na mahusiano ya kimapenzi pale ambapo wengi wao haswa wasichana hupata ujauzito na kuishia kuwacha shule.Ripoti zimetolewa na mashirika mbalimbali kuhusu suala hili la mimba za mapema na mahusiano ya kimapenzi.Kwa mfano, kutokana na data ya utafiti ya Shirika la Afya Duniani (WHO, 2013) ni wazi kwamba, watoto wa kike hususan milioni kumi na sita ambao umri wao upo kati ya miaka kumi na tano hadi kumi na tisa na hata wengine ambao umri wao upo chini ya miaka kumi na mitano huathirika sana na mimba za mapema kila mwaka.Idadi hii ni kubwa zaidi,tatizo ambalo linafaa kutafutiwa suluhu. Kule Afrika Mashariki,ni wazi kwamba asilimia kubwa ya watoto hulazimishiwa ndoa za mapema.Kutokana na taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF,2017),Sudan Kusini iliongoza kwa idadi ya juu zaidi ikiwa na asilimia 52,ikifuatwa na Uganda ikiwa na asilimia 40,Tanzania asilimia 28 na Kenya asilimia 23.Kuozwa kwa mtoto wa IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 2 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI kike akiwa angali mdogo ni ukiukaji wa haki dhidi ya watoto tendo ambalo limechangia mimba za mapema. Vilevile,licha ya maendeleo mengi katika miongo ya hivi karibuni,mamilioni ya watoto bado wanaishi bila haki zao za kimsingi.Ulimwenguni, inakadiriwa kuwa watoto milioni mia nane wanaishi katika maeneo tete na yaliyoathiriwa na migogoro ambapo haki za watoto hukiukwa na watoto kuingizwa katika unyonyaji na utumwa(De Young, Kenardy na Cobham 2011).Kulingana na ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) iliyotolewa mwaka wa 2022, kati ya mwaka wa 2005 na 2020, visa zaidi ya elfu mia mbili sitini na sita vya ukiukaji wa haki za watoto viliripotiwa barani Afrika,Asia,Mashariki ya kati na Amerika kusini.Kutokana na ripoti hiyo, watoto laki moja walidhibitishwa kulemazwa, watoto elfu tisini wameajiriwa ili kutumikia jeshi,wengine kutekwa nyara,kubakwa na mengine mengi. Hata hivyo, waandishi wa kazi za fasihi wamelishughulikiwa suala hili kwa kiasi fulani.Katika kazi yake Kavuria (2008), dhuluma dhidi ya watoto katika riwaya za Kiswahili,alitoa maelezo kuhusu unyanyasaji wa kimapenzi kama aina moja ya dhuluma za watoto.Alielezea zaidi kuwa, watoto wanapodhulumiwa kimapenzi mara nyingi haki huwa haipatikani kwani kesi zao hutupiliwa mbali. Kwa mujibu wa Kiarie (2005), ukiukaji wa haki za watoto katika jamii ya leo husababishwa na tamaduni duni, msukumo wa wanarika na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii. Hivyo basi, fasihi ya kiswahili hutumiwa na waandishi mbalimbali kama kurunzi ili kuyamulika mambo jinsi yalivyo katika jamii.Kwa sababu hii, utafiti wetu ulijikita katika ukiukaji wa haki za watoto katika riwaya mbili kuu za kiswahili;Chozi la Heri (2017) ya Assumpta K. Matei na Nguu za Jadi (2021) ya Clara Momanyi. Tatizo la utafiti Ukiukaji wa haki za watoto limekuwa ni donda sugu katika jamii kwa muda mrefu sasa.Kila mtoto, bila kujali umri wake,rangi,jinsia au mahali alipozaliwa ana haki.Haki hizi zimewekwa katika sheria za kimataifa katika mkataba wa haki za mtoto (CRC).Mkataba huu unatambua kwamba watoto wote lazima watendewe haki kwa usawa na kwa utu.Sheria za mkataba wa haki za mtoto hazina ubaguzi na huwa kwa manufaa ya mtoto kila mara.Haki hizi zinajumuisha haki ya kujieleza na kutoa maoni,haki ya usawa,afya,elimu,mazingira safi,mahala salama pa kuishi na kulindwa dhidi ya kila aina ya madhara.Haki hizi zimeainishwa katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Mtoto wa 1989 (UNCRC), mkataba wa haki za binadamu ulioidhinishwa zaidi duniani. Kulingana na ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) iliyotolewa mwaka wa 2022, kati ya mwaka wa 2005 na 2020, visa zaidi ya elfu mia mbili sitini na sita vya ukiukaji wa haki za watoto viliripotiwa barani Afrika,Asia,Mashariki ya kati na Amerika Kusini.Kutokana na ripoti hiyo, watoto laki moja walidhibitishwa kulemazwa,watoto elfu tisini wameajiriwa ili kutumikia jeshi,wengine kutekwa nyara,kubakwa na mengine mengi.Watoto ni amali muhimu ya jamii na hivyo ni wahusika wakuu katika fasihi ambayo ni kioo cha jamii.Wanapoathirika bila shaka jamii kwa ujumla inaathirika.Utafiti huu hivyo basi unanuia kulizama tatizo hili kwa kuangazia ukiukaji wa haki dhidi ya watoto katika riwaya za kiswahili IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 3 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI mfano wa Chozi la Heri na Nguu za Jadi kama kipengele cha uhalisia, ambapo uhalisia katika maandishi ya kiubunifu hutumika kuendeleza maudhui mbalimbali Ukiukaji wa haki za watoto katika riwaya zaChozi la Heri na Nguu za Jadi Mauaji Kuua ni hali ya kutoa uhai wa kiumbe au mtu.Haki ya kuishi inatokana na imani kwamba kila binadamu ana haki ya kuishi na haswa,hapaswi kuuawa na mtu au kitu kingine,ikiwa pamoja na serikali.Kulingana na Cucchetti 1989, nchini Roma,wakati wa zamani pamoja na jamii nyingi za kiafrika, watoto walisawiriwa kama mali ya wazazi wao na wangeweza kuwatendea maovu mbalimbali na hata kuwaua bila kuchukuliwa hatua yoyote ya kisheria.Vilevile, katika Biblia, kuna visa mbalimbali vya mauaji ya watoto vilivyonakiliwa katika kitabu cha Mathayo 2:16 na Kutoka 1:15.Kutokana na vitabu hivi, kiongozi angetoa amri ya kuwaua watoto hata bila kupingwa na jamii. Riwayani, mauaji ya watoto yametokea pale ambapo mzee Kedi analiteketeza jumba la Ridhaa kutokana na tofauti zao za kisiasa.Hii ni baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya Mwekevu ambaye alipingwa na wengi ila Ridhaa alimuunga mkono.Wanaoangamia katika mkasa ule wa moto ni mjukuu wa Ridhaa kwa jina Becky,Tila na Mukeli bintize Ridhaa.Haya yanajitokeza kupitia kauli ifuatayo;”sasa Ridhaa anatazamana na majivu ambayo bila shaka ni miili ya wanawe wawili,mkewe, mkaza mwanawe na mjukuu wake, Becky” (uk 5).Utafiti huu unaendana sambamba na taarifa iliyochapishwa mnamo Januari 28,2008 na Jeffrey Gettleman.Kutokana na taarifa hiyo, vurugu za kikabila ziliongezeka nchini kenya baada ya kuchaguliwa kwa kiongozi mpya na maafisa wa polisi walisema takriban watu kumi na tisa wakiwemo watoto kumi na mmoja walichomwa hadi kufa ndani ya nyumba na kundi la watu.Hata jeshi la Kenya lililotumwa kwa mara ya kwanza kuzuia wapinzani kushambuliana, lilishindwa kusitisha wimbi la mauaji ya kulipiza kisasi. Vilevile, umati uliodai kuwa Lemi kamwibia mama mmoja simu unamteketeza Lemi vibaya.Haya yanadhihirika katika usimulizi wa Dick kisa ambacho anakitamba akilini mwake.Katika kisa hiki,Tindi dadake Lemi anakwenda naye katika sherehe ili kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Lemi.Sherehe ilianza vyema,mtoto akala shibe yake,kisha akamwambia dadake waende nyumbani kwani usiku ulikuwa mpevu ila Tindi alimwambia kuwa ilikuwa mapema na amwache asakate midundo miwili kisha waondoke.Lemi alipelekwa kwenye chumba cha kutazamia runinga ili kusetiriwa asione asiyostahili kuona.Binti yule aliingia uwanjani na kusakata midundo bila kujali mpito wa wakati,wala mtoto aliyekuwa chumbani peke yake.Asubuhi jua lilipotaka kuchomoza Tindi alimshika mnuna wake mkono wakaelekea nyumbani.Hatua chache kabla ya Lemi na dadake kufika kwao kulitokea vurumai pale ambapo mama mmoja ambaye alikuwa ameraukia matwana ya kumpeleka kazini alikuwa akipinga ukemi,amenyang’anywa rununu yake akawa anakimbia kuelekea walikokuwa Lemi na dadake kwa msaada pasi na kujua alikuwa akiwaelekezea balaa.Umati wa watu uliokuwa umesikia kamsa ya mama huyu uliwaelekea kina Lemi na kutaka kuwavaa mawe na tairi.Dadake alikimbia na kumwacha Lemi ambaye alisalimiwa kwa mawe na mateke.Baadaye alivikwa tairi kiunoni na kumwagiwa petroli na kutiwa moto (uk 120-122). Kutokana na utafiti huu ni wazi kwamba watoto wanadhulumiwa haswa kwa madai ya wizi yasiyokuwa na ushahidi kisha kuchomwa na kupokonywa haki yao ya kuishi. IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 4 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI Dhuluma za kimapenzi Kulingana na Sneddon (2003), unyanyasaji wa mapenzi hutokea wakati mtoto anashirikishwa ngono.Inaweza kujumuisha mtu mzima kutumia mtoto ili kujiridhisha kimapenzi.Baadhi ya tabia za kujihusisha kimapenzi kati ya mtoto na mtoto au kati ya mtoto na mtu mzima huzingatiwa kuwa unyanyasaji wa kimapenzi.Tabia hizi zinaweza kuhusisha mguso wa mwili na usio wa mwili kama vile kufichua sehemu za siri na matumizi ya maneno ya kushawishi mtoto kingono. Mfano wa dhuluma za kimapenzi ni ubakaji.Kubaka ni kitendo cha kushirikiana kimapaenzi au ngono na mtu bila hiari yake kwa kutumia nguvu.Watoto ambao ni mali ya taifa ya nchi yetu wanahitaji kutunzwa na kulindwa kwani kuna ongezeko kubwa la ukiukaji wa haki zao za msingi.Ubakaji au unyanyasaji wa kijinsi kwa watoto (CSA) ni miongoni mwa aina za kutisha za ukiukaji wa haki zao.Madhara ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto huacha kovu kubwa ndani yao pale ambapo ustawi wao katika utu uzima huweza kusumbuliwa pakubwa.Ripoti zinazotokana na vyombo vya habari na mijadala kuhusu unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto zinaonyesha ongezeko la kitendo hiki kiovu ambacho kinahitaji kuchunguzwa kwa haraka.Kazi za fasihi pia zimetumika kulimulika jambo hili kupitia waandishi mbalimbali.Kwa mfano; Assumpta K.Matei katika riwaya yake Chozi la Heri amedhihirisha ubakaji katika dondoo hili;”Baadaye genge hili la la mabarobaro watano lilifululiza hadi walipokuwa maskini mabinti wangu wawili, Lime na Mwanaheri.Sikuweza kuvumilia kuona unyama waliotendewa.Nilijaribu kwa jino na ukucha kuwaokoa lakini likawa suala la mume nguvuze! Mahasimu hawa walitekeleza unyama wao na kuniacha bila kunigusa,niuguze majeraha ya moyo”(uk 25). Kutokana na dondoo hili,Lime na Mwanaheri ni wahadhiriwa wa kitendo hiki cha ubakaji.Wawili hawa ni wanawe Kaizari.Kaizari anamsimulia Ridhaa katika kambi ya wakimbizi jinsi wanawe walivyobakwa na mabarobaro watano baada ya nchi ya Wahafidhina kumtawaza kiongozi mwanamke.Uhafidhina unawafanya baadhi kutokubali uamuzi huu.Kaizari anaelezea kuwa, siku ya nane baada ya mapinduzi walisikia hodi mlangoni.Mkewe subira alisalimiwa kwa kofi kubwa kisha akaulizwa wapi kile kidume chako kijoga ambacho kimetuuza kwa kumpigia kura Mwekevu. Ubakaji huu wa Lime na Mwanaheri unaonyesha jinsi tamaa ya uongozi inavyosambaratisha mshikamano wa kijamii.Vijana wanatumiwa na viongozi kuendeleza njama zao ovu badala ya kuuwajibisha uongozi. Vilevile,Sauna anabakwa na Bwana Maya, baba yake wa kambo.Kitendo hiki kinadhihirika kupitia dondoo lifuatalo;”Mlaani shetani” Sauna aliumbia moyo wake... “Fikiria wewe, u kigoli, kifua ndio kinaanza kuvuvumka, kisha unaamka usiku kumpata baba yako, ba-ba-ya-ko, kwenye chumba chako cha malazi.Anakutenda ya kutendwa.Asubuhi huna hata uso wa kumtazamia yeyote,wala kinywa cha kumwambia mama yako kuhusu feli uliyotendewa”(uk 154). Katika dondoo hili, Sauna anazungumza moja kwa moja na moyo wake kana kwamba ni binadamu mwazake.Sauna anaulalamikia moyo wake kuonyesha masikitiko aliyonayo baada ya kuvunjiwa heshima na baba yake wa kambo.Kupitia maneno haya, ni wazi kwamba kitendo hiki cha ubakaji kinamsababishia Sauna uchungu moyoni kitendo ambacho anakikashifu.Kubakwa kwa Sauna kunaonyesha jinsi kinababa wa kambo wanavyowadhulumu wanao wa kike badala ya IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 5 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI kuwalinda.Kauli hii inaendana moja kwa moja na utafiti wa Sara Scott,2023 Septemba anapodai kuwa baba na baba wa kambo ndio jamaa wanaopatikana na hatia zaidi ya unyanyasaji wa kingono wa watoto katika familia.Anaeleza kuwa,kutokana na kesi nyingi zinazoripotiwa ni wazi kwamba, wahalifu waliohukimiwa kwa kosa la ubakaji wa watoto asilimia kubwa ya wahalifu hao ni watu wa familia haswa kina baba wa kambo. Vilevile,mwalimu Fumba anamdhulumu mwanafunzi wake Rehema kimapenzi.Fumba anahusiana kimapenzi na mwanafunzi wake Rehema kisha kumtunga mimba (uk 102- 103).Pia,mwanaharakati analalamikia kulawitiwa kwa wavulana.Katika usemi anauliza kuwa “lakini ni wangapi wanaokumbuka kuwa hata maghulamu wanalawitiwa?”(uk.17).Vilevile,katika Nguu Za Jadi,wasichana wadogo wanazalishwa wakiwa bado hawajatimiza umri wa kujitwika majukumu kama hayo (uk.137-138).Hili linajitokeza kupitia taswira anayochora mwandishi kuhusu watoto wenye umri mdogo. Ndoa za mapema na za lazima Ndoa ya mapema ni ndoa ya kulazimishwa ya mtoto, ambaye kwa kawaida hufafanuliwa kama mtu aliye chini ya umri wa miaka kumi na minane (Encyclopedia of Violence,Peace & Conflict Toleo la tatu, 2022).Ndoa za mapema hutokana na ukosefu wa usawa wa jinsia pale ambapo mtoto wa kike ndiye huathirika zaidi ikilinganishwa na yule wa kiume.Vilevile, ndoa za mapema zimethihirishwa katika Chozi la Heri kupitia mhusika Pete ambaye alilazimishwa kuolewa kama mke wa nne kwa mzee Fungo.Licha ya rai za nyanya yake kwamba aachwe afuatilie elimu, maneno hayo yaliangukia masikio yaliyotiwa uziwi kwani mama na ndugu zake Pete walikuwa wameamua kumuoza Pete kwani waliamini kuwa alikuwa ashaingia utuuzima baada ya kupashwa tohara.Haya yanathihirika kupitia dondoo lifuatalo; “Maisha yangu yalichukua mkondo mwingine nilipojiunga na darasa la saba.Katika jamii yangu, inaamiwa kuwa msichana akiisha kupashwa tohara, ameingia utuuzima, hivyo ataipaka familia yake tope ikiwa ataendelea kuozea kwao bila mume.Wajomba zangu hawakuchelea kupokea posa na baadaye mahari kutoka kwa buda mmoja ambaye alinioa kama mke wa nne” (148). Kutokana na dondoo hili,tunagundua kwamba, Pete anaozwa akiwa na umri mdogo kwani alikuwa katika darasa la saba.Pete anaozwa kama mke wa nne kwa mzee Fungo.Ndoa hii ya Pete kwa mzee Fungo inasababishwa na imani potovu za jamii ile pale ambapo wanaamini kwamba wakati msichana anapashwa tohara anafaa kuolewa. Kukatizwa elimu Kila mtoto ana haki ya kupata elimu.Elimu ni taaluma inayomsaidia mwanadamu kujiendeleza kimaarifa na kiutafiti.Kwa mujibu wa Meyer (1977), elimu ni asasi iliyo na athari ya kuendeleza mitagusano ya watu katika jamii.Elimu huwafanya watu kujitegemea na kujikomboa kimawazo.Elimu huwapa vijana maadili na maarifa ifaayo katika jamii kwani baadae vijana hawa huweza kuajiriwa au kujiajiri.Elimu ni suala muhimu sana miongoni mwa vijana kwani huwatoa katika hali duni ya maisha.Kulingana na Taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF 2023) kila mtoto ana haki ya kupata elimu bila kujali asili yake,jinsia au kabila. IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 6 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI Vilevile, waandishi mbalimbali wa kazi za fasihi za kiswahili wameliangazia suala hili.Kwa mfano,Assumpta K Matei ameliwasilisha suala hili kupitia mhusika Pete.Pete anakatiziwa elimu yake akiwa darasa la saba.Pete analazimishwa kuolewa na mzee Fungo kwa hofu kuwa ataipaka familia yake tope ikiwa ataendelea kuozea kwao bila mume licha ya nyanya yake kupinga kitendo cha mama na wajomba wake kumwoza kabla ya kukamilisha elimu. Hili linathihirika kupitia dondoo lifuatalo; “Huyu mtoto ni mbichi mno,”...’hatuwezi kumkabidhi mzee wetu huyu kifaranga kiteketeke hivi, tutakuwa tunampangaza ulezi.Isitoshe, Pete mwenyewe ana hamu kuu ya kufuatilia elimu, tumwache aizime kiu yake.Akiisha kutimiza maazimio yake,atajichagulia kijana mwenzake wafunge nakidi’ (Uk 148). Kutokana na dondoo hili, elimu ya Pete inakatizwa ili aozwe kwa mzee Fungo.Ingawa Pete ana hamu kuu ya kufuatilia elimu, tamaduni na imani potovu zinamfanya kukatiziwa elimu yake akiwa darasa la saba.Mara nyingi, ndoa huthaminiwa sana kuliko elimu.Elimu kwa wasichana hupewa thamani ya chini . Vilevile, mhusika Zohali analazishwa kuacha masomo yake baada ya kupata ujauzito akiwa katika kidato cha pili.Katika masimulizi yake anaeleza kuwa, maisha yake yalianza kwenda tenge alipojiunga na kidato cha pili.Anazidi kueleza kwamba, hali ya mtafaruku wa hisia iliyowapata vijana katika umri huo aliikumbatia kwa papara za ujana ndipo akajipata ameambulia ujauzito.Mwalimu mkuu alitoa hukumu kwamba Zohali arejeshwe nyumbani na baada ya kujifungua wazazi wake wamtafutie shule nyingine.Hili linathihirika kupitia dondoo ifuatayo; “Dadake Zohali,samahani sana lakini uchunguzi unabainisha kwamba Zohali ni mjamzito.Nimekuita hapa ili uweze kumrejesha nyumbani.Akijifungua wazazi wake wanaweza kumtafutia shule nyingine” (uk 99). Kutokana na dondoo hili, mwalimu mkuu alitoa hukuma kwa Zohali kurejeshwa nyumbani baada ya kuambulia ujauzito na baadaye kutafutiwa shule nyingine akishaajifungua.Kutokana na hukumu hii ya mwalimu mkuu ni wazi kwamba Zohali anakatiziwa masomo yake.Vilevile, ami za Lucia na Akelo wanapinga elimu yao na kudai kuwa kuwaelimisha wasichana ni kufisidi rasilimali.Hili linathihirika kupitia kauli ifuatayo; “...si nyinyi mliokuwa hata mkipinga elimu ya mabinti hawa? Hamkusema kwamba kuwapeleka shuleni ni kufisidi rasilimali?” (uk 66) Kutokana na kauli hii ni wazi kuwa, Ami za Lucia na Akelo hawamthamini mtoto wa kike na elimu yake.Kwao kumsomesha msichana ni kuifisidi rasilimali Ajira kwa watoto Ajira kwa watoto hurejelea unyonyaji wa watoto kupitia aina yoyote ya kazi ambayo inawanyima utoto wao,inaingilia uwezo wao wa kuhudhuria shule ya kawaida na inawadhuru kimwili,kiakili,kimaadili na kijamii. Ripoti ya Shirika la Kazi Duniani ya mwaka 2021 inaonyesha jumla ya watoto milioni 3.3 wako katika hali ya kutumikishwa kwa IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 7 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI kulazimishwa.Vilevile, katika riwaya ya Chozi la Heri,ajira kwa watoto imeendelezwa kupitia wahusika kama vile Sauna pale ambapo mhusika huyu anaajiriwa kwenye machimbo ya mawe,kuuza maji na hata pombe baani.Hii ni baada ya kupoteza matumaini na hamu ya kuendeleza masomo yake baada ya kuhujumiwa kimapenzi na kihisia.Suala hili linathihirika kupitia dondoo ifuatayo; “Nimefanya kazi katika machimbo ya mawe, nimewahudumia waungwana kwa namna zote katika majumba ya kuuzia pombe, nimeuza maji ya mito na madimbwi yaliyotiwa kwenye chupa zenye vibandiko vya kuvutia, ati ni mineral water...” (uk 156). Vilevile Chandachema anahusishwa katika ujira wa uchunaji wa majani chai akiwa mtoto wa darasa la tano kwenye Shirika la chai la Tengenea.Chandachema alianza kuchuna majanichai kwa malipo kidogo ili kuwatua Bi.Kimai na Bw.Tenge mzigo wa kumnunulia sare na madaftari.Hili linathihirika kupitia kauli ifuatayo; “Nilianza kuchuna majanichai kwa malipo kidogo nikiwa katika darasa la tano.Wakati mwingine ningerauka alfajiri na mapema kufanya kazi kabla ya kwenda shuleni saa kumi na mbili asubuhi”(uk 106-107). Vilevile,katika Nguu za Jadi,ajira kwa watoto inadhihirika kupitia vitendo vya Sihaba.Sihaba anawaajiri wasichana wadogo kufanya biashara ya ukahaba ili ajinufaishe kifedha.Hili linadhihirika kupitia kauli ifuatayo;Sihaba alitupwa korokoroni asubiri mashtaka ya kuwaajiri watoto wadogo kufanya biashara ya ukahaba(uk 143).Sihaba aliendeleza biashara hii kwa muda mrefu jambo ambalo lilijulikana na wengi ila waliogopa kutoa habari hii kwani walimwogopa Sihaba sana.Hivyo, wakamwacha kuendeleza hujuma yake. Ni haki ya watoto kulindwa dhidi ya unyanyasaji wa kiuchumi na ajira ambayo inatatiza ukuaji wao kimaadili,kiakili na kiafya.Ni jukumu la serikali kutoa masharti ya kazi.Nchini Kenya, watoto wengi huajiriwa katika mashamba ya majani chai, kahawa, migodi na mikonge ambao umri wao upo chini ya miaka kumi na sita.Watoto hawa hupokea ujira mdogo usioweza kuyakidhi mahitaji yao licha ya kazi za sulubu wanazofanya. Watoto kutelekezwa na wazazi wao Kutelekeza mtoto hufafanuliwa kama kutofaulu kwa mzazi au mtu mwingine mwenye wajibu kwa mtoto kumpa chakula kinachohitajika,mavazi,makazi,matibabu na ustawi unaostahili (Benedictis na wengineo 2006).Kutowatelekeza watoto huwasaidia kukua vyema.Wajibu wa wazazi kuwafunza watoto wao maadili mema hutokea wakati huu.Watoto ambao hawatunzwi vyema katika utoto wao huishia kukosa maadili mema na wengi wao huingilia matendo maovu (Ciccheti 1983).Kuwaonyesha watoto mapenzi ili wahisi wako salama ni mojawapo ya utunzaji wa watoto. Katika riwaya ya Chozi la Heri, Pete anatelekezwa na mama yake mzazi.Pete analelewa na bibi mzaa mama yake baada ya mtafaruku kati ya baba na mama yake kutokea.Pete anapata kujua kuwa chanzo cha mama yake kumtelekeza kwa kwa nyanya yake ni kuwa hakuwa na mshabaha na baba yake.Katika usimulizi wake, Pete anasema; IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 8 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI “Mara tu macho yangu makinda yalipoanza kuutambua ulimwengu,nilijipata kwenye boma la bibi mzaa mama,kisa na maana, kumetokea mtafaruku fulani kati ya baba na mama.Sijui ni mtafaruku wa aina gani, ila katika pitapita zangu kijijini mwa bibi, alitokea domo kaya fulani akaninong’onezea kwamba sikuwa na mshabaha hata chembe na baba” (uk 147). Kutelekezwa kwa Pete na mamaye kunapelekea Pete kukosa vitu vya kimsingi.Kwa mfano, Pete anakosa sodo baada ya kukabiliana ana kwa ana na hedhi yake ya kwanza jambo ambalo linamfanya nyanya yake kumtafutia tambara la blanketi kwani ndilo lilikuwa fimbo ya karibu. Vilevile, Subira mkewe Kaizari anawatelekeza wanawe.Subira baada ya kutofautiana na mavyaa zake anaondoka na kuwaacha Lime na Mwanaheri bila kujali huzuni atakayowasababishia.Mwanaheri anaeleza kuwa,mama yake alitoka katika jamii ya Bamwezi jambo lililomsababishia mama yake kuchukuliwa kama mgeni katika boma yao na hata kijijini chao.Anaeleza kuwa, “haikuwa ibra kumsikia nyanya yao akimrejelea mama yao Subira kama múki,yaani ‘huyo wa kuja’na kusema kwamba msichana wa Bamwezi, hata akiwa na umri wa miaka tisini ni msichana wa Bamwezi tu”(uk 94).Maneno hayo ya nyanya yake Mwanaheri yalikuwa ya kumkumbusha Subira kwamba yeye hakuwa wa ukoo hule. Vilevile, riwayani, vitoto vidogo vinatelekezwa na mama zao baada ya kuzaliwa.Haya yanatokea pale ambapo baada ya kuzaliwa vitoto hivi vinatupwa.Neema anamwokoa mtoto aliyetupwa jalalani na kumpeleka kwenye kituo cha polisi.Neema anasimulia na kusema, “Nilipokaribia biwi hili, nilisikia sauti fulani dhaifu mawazoni mwangu, ‘Ng’aa! Ng’aa!’Niliipuuza sauti hii, nikidhani kuwa huu ni mwangwi wa sauti ya kitoto cha jirani yangu ambacho kilikuwa na mazoea ya kulia usiku kucha.Mara sauti hiyo ilisikika tena, ikanituma kutazama kando.Hapo hapo katikati mwa kilima hiki cha taka, niliona karatasi ya sandarusi ikifurukuta katikati ya fondogoo la kila aina.Kufurukuta huku kuliandamana na kilio kile hafifu...”(uk 161).Aidha, Mtawa Cizarina anasema kwamba “kuna mtoto aliyetupwa langoni mwa kituo cha watoto cha Benefactor akiwa amefungwa kijiblanketi kikuukuu” (uk 162). Kutokana na suala hili, ni wazi kwamba binadamu amezika hadhi na utakatifu wa maisha ya mja katika kaburi la sahau.Utafiti huu unaenda sambamba na ule wa (Kalume 2014) anapoeleza kwamba kitoto cha siku moja kilipatikana katika biwi la taka kule Lamu.Anayefanya kitendo kile anashtumiwa na wananchi.Kitoto kile kinapelekwa katika kituo cha kuvilea vitoto vilivyotelekezwa. Vilevile, babake Kairu anamtelekeza Kairu kwani hamsaidii mkewe katika malezi jambo ambalo halimpi amani Kairu katika masomo yake.Hili linatokea baada ya mama yake Kairu kuhusiana kimapenzi na baba yake Kairu japo ana familia nyingine.Kairu anazaliwa nje ya ndoa na kunyimwa nafasi ya kutunzwa na baba yake (uk 93). Chandachema anatelekezwa na wazazi wake mwalimu Fumba na Rehema.Chandachema analelewa na nyanya yake baada ya baba yake Fumba, kumtelekezea huko.Katika usimulizi wake,Chandachema anasema kuwa maisha yake yalijaa shubiri tangu utotoni.Hakumbuki akimwona mama yake (uk 102|).Kutokana na maelezo anayopewa na Katini,Fumba alimtunga mimba Rehema, mama yake Chandachema akiwa kidato cha tatu.Wazazi wa Rehema wanapinga IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 9 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI ndoa kati ya Rehema na Fumba na kumletea Fumba mtoto wake alee.Fumba anamwacha Chandachema alelewe na nyanya hadi kifo cha nyanya yake. Vilevile,katika riwaya ya Nguu za Jadi,Mrima anawatelekeza wanawe wawili Sayore na Kajewa.Haya yanatokea baada ya Sagilu kumnyemelea na kumzuga Mrima kwa kutumia pesa kiasi kwamba Mrima anaisahau familia yake huku Mangwasha mkewe anaangaika na wanawe peke yake bila baba yao (uk 1).Riwayani tunajuzwa kuwa,Sagilu anamtaka Mangwasha kimapenzi licha ya kujua kwamba msichana huyu alikuwa na mchumba na baada ya kukataliwa anaweka kisasi dhidi yake.Mrima anazugwa pesa na Sagilu jambo lilnalomfanya kuingilia ulevi hadi kuisahau familia yake.Riwayani,tunajuzwa kuwa wana hawa hawakuwa na habari kuhusu baba yao(uk.1).Pia,Mangwasha mkewe Mrima anamweleza rafiki yake Mbungulu yote yaliyomsibu.Alimweleza jinsi anavyojitwika jukumu la kuwasomesha,kuwalisha na kuwavisha watoto hawa peke yake (uk 29).Hivyo,kutokana na utafiti huu,ni wazi kwamba Mrima haonekani kujitwika majukumu yake ya unyumba.Anakesha na kuamkia ulevini.Hana habari tena kuhusu familia yake. Kutokana na visa hivi vya kuwatelekeza watoto,ukweli ni kwamba watoto wanaozaliwa nje au ndani ya ndoa wana haki sawa.Wazazi wote wanajukumu la kuwashughulikia na kuwatunza wanao iwe wameona au la. Ubaguzi wa watoto Kumbagua mtu au mtoto kuna maana ya kumtendea mtu huyo kwa njia ambayo haifai au kwa njia tofauti kwa sababu fulani.Kulingana na katiba ya kenya ilioidhinishwa 2010 katika kifungu cha 27; kila mtu ni sawa mbele ya sheria na ana haki ya kulindwa na kupata manufaa sawa ya sheria.Usawa unajumuisha kupata haki na uhuru wote wa kimsingi kwa njia iliyo kamili na sawa.Kutokana na kifungu hiki, mtu hatakuwa na ubaguzi dhidi ya mwingine kwa njia ya moja kwa moja au vinginevyo. Vilevile, kifungu cha tano cha sheria ya watoto kinasema kwamba hakuna mtoto anayepaswa kubaguliwa kwa misingi ya asili,jinsia,dini,imani,desturi,lugha,maoni,dhamira,rangi,kuzaliwa kijamii,kisiasa,kiuchumi au hali nyingine.Riwayani, Pete anabaguliwa na mama na wajomba zake pale ambapo wanamwoza kwa lazima kwa mzee Fungo kama mke wa nne.Wanafanya hivi ili wapewe mahari itakayotumiwa kuwaelimisha ndugu zake watano wa kiume.Hili linadhihirika kupitia kauli ya mzee Fungo anapomwuliza Pete,”Utawezaje kujitunza wewe na mtoto wako na hali bibi yako ndiye huyo,hana hanani,na wazazi wako walafi walikuuza kwangu ili wapate pesa za kuwasomesha ndugu wako watano wa kiume?” (uk 149). Ubaguzi huu kwa Pete una msingi wake katika tamaduni ambazo zinamwona mtoto wa kiume kama mrithi wa familia.Kitendo anachofanyiwa Pete kinatokana na imani ya kitamaduni kwamba watoto wa jinsia moja ni bora kuliko wengine.Tamaduni zinazombagua mtoto wa kike zimepitwa na wakati na zinafaa kutupiliwa mbali. Utafiti huu unaendana sawia na ule wa Dauda (2008), anaposema kwamba ufaulu wa elimu ya mtoto wa kike ni mdogo kwani tafiti zimeonyesha kuwa wasichana wachache wanaenda shuleni kuliko wavulana.Alibainisha kuwa hii ni kwa sababu mtoto wa kike hajabahatika kuenziwa, IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 10 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI kulindwa na kupendwa katika jamii kutokana na mila fulani, imani potofu za kitamaduni na kidini ambazo zinamweka katika hatari ya kunyanyaswa na kutelekezwa. Uavyaji mimba Uavyaji mimba ni kitendo cha hiari cha kuua mimba kabla ya kijusi kuwa na uwezo wa kuishi.Lewis na Tamparo (2007) wanadai kuwa, kulingana na kamati ya kitaifa ya kuzuia unyanyasaji wa watoto, zaidi ya watoto elfu moja wanaavywa kila kuchao.Dkt.Richard Krugman wa kituo cha kitaifa cha kuzuia unyanyasaji na utelekezwaji wa watoto wa Denver Kempe, anaweka idadi hiyo kuwa kubwa zaidi ya mimba zinazoavywa ambayo ni kutoka mimba elfu mbili hadi elfu tano kwa mwaka.Tunaweza kujua kwamba, thamani ya nafsi ni kuu machoni pa mungu lakini hali za kisasa na shinikizo za jamii zimepofusha watu wengi kutokana na ujuzi huu wa kina.Kwa sababu hiyo, chaguzi zinafanywa ulimwenguni kote ambazo zinapuuza thamani ya uhai wa mwanadamu na mojawapo ni utoaji mimba. Vilevile, kulingana na katiba ya kenya kifungu cha 26, kila mtu anahaki ya kuishi.Maisha ya mtu huanza baada ya mimba kutungwa.Uavyaji mimba hauruhusiwi isipokuwa kwa maoni ya mtaalamu wa masuala ya afya.Riwayani, mamake Sauna anamsaidia kuavya kitoto chake.Anafanya hivi kwa kumwogopa Bw.Maya ambaye ni baba wa kambo wa Sauna aliyemnajisi Sauna.Jambo hili linadhihirika kupitia dondoo ifuatayo;”...sikuweza kuamini kwamba mama yangu angekuwa amrijeshi wa mauaji.Maskini kitoto changu kilitunguliwa kabla hata hakijaumbika” (uk 155). Kutokana na suala hili ni wazi kwamba watoto wa kike wananyanyaswa na wazazi wao haswa kina baba wa kambo jambo ambalo linapelekea wao kuwa na ujauzito katika umri mdogo kisha kutafuta suluhu ya ujauzito hule ambayo ni kutungua ile mimba. Wizi wa watoto Wizi wa watoto ni hatua au desturi ya kupata na kuhamisha watoto kutoka mazingira yao salama kinyume cha sheria kwa madhumuni ya kazi za kuwalazimisha au unyanyasaji wa kingono.Wizi wa watoto umekuwa suala la ulimwengu mzima katika miaka michache iliyopita.Ingawa hakuna takwimu sahihi zilizopo, mkataba wa ILO(mwaka wa 2005) ulikadiria kuwa watoto 980,000 hadi 1,225,000 wavulana na wasichana wako katika hali ya kulazimishwa kufanya kazi.Aina hizi za kazi ni pamoja na usafirishaji wa dawa za kulevya,ajira ya watoto nyumbani,kuhusisha watoto katika ukahaba na zingine nyingi jambo ambalo ni kinyume cha sheria.Kulingana na katiba ya kenya, iliyoidhinishwa mwaka wa 2010 katika kifungu cha 30, mtu hatahitajika kufanya kazi ya kulazimishwa. Riwayani, Assumpta K.Matei amelishughulikia suala hili kwa kupitia mhusika Sauna na Bi.Kangara.Sauna aliyekuwa kijakazi nyumbani mwa Lunga na Naomi anawaiba Dick na Mwaliko.Hii ni baada ya Naomi mkewe Lunga kumwacha Lunga na watoto wake baada ya Lunga kufilisika.Hali hii inamfanya Lunga augue shinikizo la damu na hatimaye kufa huku akiwaacha wanawe chini ya ulinzi wa kijakazi yao Sauna.Sauna anapata upenyu wa kuwaiba Dick na Mwaliko.Sauna anamuuza Dick kwa Buda pale ambapo Buda anamwigiza Dick katika matumizi na ulanguzi wa dawa za kulevya.Haya yanadhihirika kupitia dondoo ifuatayo;”siku ile baada ya kuibwa na kijakazi Sauna,Dickson alipelekewa baba mmoja tajiri ambaye alijitia IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 11 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI kumpeleka shuleni.Kumbe alikuwa kapelekwa katika chuo cha kuhitimu kama mvunja sheria!...Tajiri wake huyu, kwa lakabu Buda,alimfunza mbinu za kujikimu,akamwingiza katika biashara hii (uk 120). Vilevile, Bi. Kangara kupitia kwa juhudi za Sauna na wengine, alifanikiwa kupata wasichana wa kuuza katika madanguro,wavulana wa kuwapelekea matajiri ambao walishiriki katika ulanguzi wa dawa za kulevya na wafanyakazi katika makasri ya matajiri na katika mashamba ya mikahawa na michai.Aidha, wengine walisafirishwa ughaibuni ambako waliahidiwa kazi na walipofika kule ughaibuni walipata kwamba kazi zenyewe ni za kujidhalilisha (uk 158). Watoto kunyimwa haki ya kujua usuli wao na kutagusana na baba zao. Taarifa kuhusu asili ya mtu inajumuisha utambulisho wa wazazi wake na hali yake ya kuzaliwa na hata malezi.Kila mtoto ana haki ya kupata maelezo kuhusu asili yake ambayo yanaweza kumwongoza kugundua ukweli kuhusu vipengele muhimu vya utambulisho wake wa kibinafsi na kifamilia.Katika mkataba wa haki za watoto (CRC) kila mtoto ana haki ya utambulisho wake mwenyewe,rekodi rasmi ya yeye ni nani ambayo inajumuisha jina lake,utaifa na mahusiano ya familia.Hakuna mtu anafaa kuichukua haki hii kutoka kwake na ikiwa hili litatokea,serikali lazima isaidie mtoto kurejesha utambulisho wake haraka. Katika riwaya ya Chozi La Heri,Kairu anaeleza kwamba alipokosa karo aliwahi kumwuliza mama yake kwa nini asimwombe baba,ambaye anasikia ni mwenye chake na lake,amlipie karo.Hata hivyo,mama yake huwa hamjibu,anachompa ni mtazamo unaouliza swali,’Nitamwambia vipi mtu mwenye familia yake kumkimu mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa?’(uk.93).Hivyo,kutokana na usemi huu ni wazi kwamba mama yake anajaribu kumwambia Kairu kwamba hawezi kumwomba baba yake amlipie karo kwani yeye amezaliwa nje ya ndoa.Jmbo hili linamyima Kairu haki ya kumjua baba yake mzazi na hata kutagusana naye. Vilevile,katika Chozi la Heri,mama yake Kipanga hamwelezi wazi kwamba baba yake mlezi hakuwa baba.Katika masimulizi yake pale kituoni cha mwanzo mpya,Kipanga yu hospitalini anaponusurika kifo kutokana na kangara iliyowaua watu sabini kutokana na matumizi ya vileo.Kipanga anasema kwamba,alianza kuchovya vileo akiwa kidato cha pili baada ya aliyedhania kuwa baba yake kumkana, na kulazimika kuhama alikoita kwao,yeye,mama yake na mnuna wake ambaye alisemekana ndiye mwana halisi wa baba yake.Kipanga anasema kwamba lililomuuma zaidi ni kwamba alipomtaka mama yake kumwambia ukweli,mama mtu hakumpa jawabu la kuridhisha.Alichosema ni,’Yapo mambo ambayo mtu hawi na uso wa kumtazamia mwanawe kwayo.Aliyekulea ndiye mzazi wako,mradi tu akubali kuwajibikia ulezi’(uk.143). Kutokana na utafiti huu ni wazi kwamba watoto wananyimwa haki ya kujua usuli wao na hasa kutagusana na baba zao haswa wakati ambao wamezaliwa nje ndoa.Kuwanyima watoto haki hii kunaweza kuwasababishia matatizo ya kisaikolojia pale ambapo wengi wao huishia kutafuta mbinu mbaya za kukabiliana na tatizo hili kama vile Kipanga. Madhara yanayotokana na ukiukaji wa haki za watoto Ukiukaji wa haki za watoto husababisha anuwai ya athari mbaya kwa mwathiriwa na jamii kwa ujumla. Madhara haya yanaweza kuwa ya kijamii na pia yanayoathiri maendeleo ya mtu binafsi. IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 12 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI Kukimbia nyumbani Watoto wote wanahitaji na wanastahili usalama na hali ya kuhusishwa.Kutoroka nyumbani ni ishara kwamba watoto hawapati mahitaji muhimu nyumbani.Ili kuepukana na dhuluma zinazomkosesha mtoto utulivu na amani, watoto wengi huonelea ni vyema kukimbia nyumbani na kwenda mahali pengine angalau penye usalama na utulivu.Hii ndiyo hatua ya mwisho ambayo mtoto huchukua baada ya juhudi zote za uvumilivu kugonga mwamba. Mhusika Zohali katika Chozi la Heri anakimbia nyumbani kwao baada ya baba yake kumdhalilisha baada ya kupata ujauzito akiwa kidato cha pili bila utetezi wowote wa mama yake.Zohali anapoona kwamba maisha nyumbani kwao yamekuwa magumu, anatorokea mtaani ambako anaishi maisha duni ya matumizi mabaya ya dawa za kulevya hadi pale ambapo wenzake wanapompeleka kwenye Wakfu wa Mama Paulina ambapo anapewa hifadhi na kujifungulia hapo.Zohali anamdanganya Mtawa Pacha kwamba ni yatima. Katika usimulizi wake, Zohali aliwaelezea wenzake madhila aliyoyapitia nyumbani kwao.Haya yanathihirika kupitia dondoo ifuatayo;”Baba alisema kwamba hakuwa na pesa za kumlipa kijakazi tena.Kazi za nyumbani ziliniangukia mimi.Si kufua,si kupiga deki,si kupika...almuradi kila siku ilikuwa na adha zake” (uk 101). Kutokana na utafiti huu ni wazi kwamba,madhila aliyopitia yalimtia Zohali uchungu na unyanyapaa ambao ulimfanya awafishe wazazi wake wakiwa wangali hai.Hata hivyo, kupitia usimulizi wake tunapata kujua baba yake alijawa na majuto baadaye na akaanza kumtafuta mara tu baada ya kugubdua ametoroka (uk 101). Kutatizika kimasomo Unyanyasaji na kutelekezwa kwa watoto huongeza hatari ya watoto kupata matatizo ya kielimu (Briere et al.,1996; Johnson-Reid et al;2004;Nikulina et al;2011).Watoto ni wanajamii ambao wanapenda kuona haki ikitekelezwa.Watoto huwa na imani kwamba,haki ikitekelezwa baadhi ya matatizo kama vile,ubaguzi,dhuluma na maonevu husuluhishwa.Aidha palipo na haki pana usawa na amani. Fasili kuhusu ndoa za utotoni inasisitiza kwamba, watoto wanapoolewa mapema,elimu yao rasmi mara nyingi hukatizwa.Kukatizwa kwa elimu hii huzuia kupata maarifa na ujuzi unaowapa nafasi ya ajira(Wiliamson 2012).Madhara mbalimbali ya ndoa za utotoni na kuachishwa shule yameonyeshwa pale ambapo waathiriwa wanapata nafasi ndogo za ushiriki na maamuzi na hata hatari ya kufanyiwa vurugu. Mhusika Pete katika Chozi la Heri anaozwa kwa mzee Fungo akiwa darasa la saba ili mahari itayopatikana iwasomeshe ndugu zake wa kiume tendo linaloashiria ubaguzi.Kutokana na ndoa hii ya lazima, masomo ya Pete yanafikia kikomo kwani hakufaulu kuizima kiu yake ya elimu (uk 148).Katika ndoa yake, Pete hana amani kamwe kwani anasema kuwa,”ule unene wake mzee Fungo,lile kutuzi lililotoka kwenye makwapa yake makuza na kufudikiza kote chumbani,ule wivu wa mke mwenzangu wa pili,kule kukemewa na kuchekwa na wana wa mke wa kwanza...yote yalininyong’onyeza na kuniumbua” (uk 149). Tunaweza kusema kuwa,kama Pete hangelazimishwa kuolewa na mzee Fungo,angeizima kiu yake ya masomo kwani kutokana na kauli ya nyanya yake ni wazi kwamba Pete alikuwa na IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 13 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI hamu kuu ya kufuatilia elimu na wakati ambapo angetimiza azimio yake angejichagulia kijana mwenzake wafunge nakidi. Ukosefu wa mahitaji ya kimsingi Aina nyingine ya athari za ukiukaji wa haki za watoto ni ukosefu wa mahitaji ya kimsingi kwa watoto.Makuzi sahihi ya watoto,afya,elimu na ulinzi wa sheria ni mahitaji ya kimsingi ya watoto. Riwayani,Pete anakosa mahitaji ya kimsingi baada ya mama yake kumtelekezea kwa nyanya yake.Katika masimulizi yake,Pete anaeleza kuwa hakudiriki kuonja tamu ya kupendwa na wazazi wake.Anaendelea na kusema kuwa, hakumbuki hata siku moja akiulizwa kuhusu neema na mashaka yake shuleni.Hata baada ya mamake kuona kwamba bibi anamtaka kununua sare nyingine kila baada ya miezi michache,haikumpa kuwaza kuwa kima cha mwanawe kimeanza kuwanda,nayo maumbile yameanza kufanya kazi yake (uk 147). Vilevile,Pete anakosa sodo baada ya kupata hedhi.Anaelezea kwamba, anapata hedhi yake ya kwanza baada ya kuingia darasa la sita.Tatizo ni kwamba, hakuwa na mama wala dada wa kumjuza ya kufanya litokeapo la kutokea jambo ambalo linamfanya kumwendea ajuza wake ambaye amejiinamia kwa uzee.Kutokana na yale mazoea yao ya jadi, ajuza huyu alimtafutia tambara la blanketi alitumie kama sodo.Anazidi kueleza kuwa, tambara lile halikufaa kitu kwani alihitajika kutafuta njia nyingine ya kujikuna ajipatapo. Zaidi ya hayo, kutokana na mahangaiko hayo,juma zima lilikuwa limepita kama darasa halijakilimbuka hata kivuli chake (uk 148). Vilevile,katika masimulizi yake Chandachema ni wazi kwamba baba yake hakuwa akituma mahitaji ya mwanae Chandachema baada ya kumtelekeza kwa nyanyake jambo ambalo linamlazimu nyanyake Chandachema kutumia kidogo alichokuwa analetewa na dada zake kumtunza yule mtoto (uk 102). Hivyo basi, hali ya watoto kukosa mahitaji ya kimsingi ni jambo la kihalisia kulingana na nadharia ya uhalisia.Jambo hili hufanyika katika ulimwengu halisi na ulimwengu wa kawaida.Watoto waliotelekezwa huteseka sana kutokana na mapuuza ya mahitaji yao.Utafiti huu unaenda sambamba na ule wa Abashula,Jibat na Ayele (2014) nchini Ethiopia unaobaini kuwa watoto waliotelekezwa na wazazi wao hukumbana na matatizo mengi kama vile kukosa mavazi,elimu,chakula na mahitaji mengine ya kimsingi na ukosefu wa mapenzi ya wazazi huwasababishia msongo wa mawazo. Watoto kuishi katika mazingira yasiyokuwa na amani na hatarishi Mkataba wa watoto (2001) huwalinda watoto ambao umri wao upo chini ya miaka kumi na minane.Watoto hupata haki ya kulindwa na hali ambazo zinayaweka maisha yao hatarini kutoka kwa mkataba huu.Watoto waliotelekezwa na wazazi wao huishi katika mazingira ambayo yamejaa changamoto.Riwayani,baada ya nyanya yake Chandachema kufariki,Chandachema analazimika kuhamia kwa jirani yao Satua.Satua alimwonyesha waziwazi kwamba hamtaki.Hali hii inadhihirika zaidi mwandishi anapoeleza kuwa,baada ya Chandachema kuishi kwa Satua kwa miezi miwili alianza kuona mabadiliko.Uchangamfu aliokuwa nao Satua uliyeyuka ghafla kwani alianza kulalamikia kuisha haraka kwa sukari,alilalamikia matumizi kiholela ya sabuni ya IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 14 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI kuogea na pia alinung’unika kuhusu kubanana kwa jeshi la watoto kwenye chumba cha malazi (uk103).Chandachema alichukizwa na malamishi hayo na kulazimika kufunganya kidogo alichokuwa nacho na kuondoka. Vilevile, baada ya Chandachema kuondoka kutoka kwa jirani yao Satua,alipewa hifadhi na Bw.Tenge na Bi.Kimai pale ambapo alilelewa pamoja na watoto wao watano.Katika masimulizi yake,Chandachema anaeleza kuwa chumba cha wafadhili wake kilikuwa kimoja;ndicho cha malazi,ndicho cha mapokezi,ndicho jikoni.Sebule na chumba cha malazi viligawanywa na shuka moja nyepesi.Usiku watoto walilala juu ya vigodoro ambavyo ni kama viliwekwa mvunguni mwa kitanda cha wazazi.Zaidi ya hayo,wakati Bi.Kimai alienda mashambani,chumba kile kiligeuka na kuwa danguro.Bw.Tenge alikuwa akimleta mwanamke mmoja baada ya mwingine hapo hapo mbele ya wanawe.Kitendo hiki cha ukware cha Bw.Tenge kilimpa Chandachema dhiki za kisaikolojia (uk 106). Hivyo basi, ni haki ya watoto kuishi katika mazingira ambayo hayaatarishi maisha yao.Ni jukumu la serikali na wazazi kuhakikisha kwamba mazingira ambayo watoto wanaishi yana utulivu na amani.Watoto huathirika kiakili na kitabia iwapo watalelewa katika mazingira yaliyojaa fujo na migogoro kwani wao huyaiga na kuyatilia maanani mambo ambayo wanatendewa na watu wazima. Matumizi ya dawa za kulevya Tatizo la dawa za kulevya linaendelea na limekuwa suala nyeti duniani.Kulingana na ripoti zilizopo ulimwenguni kuhusu dawa (2018),watu wengi wameadhiriwa sana na dawa za kulevya.Suala la matumizi ya vileo limechangiwa sana na utelekezwaji wa watoto.Watoto hutumia vileo hili kujisahaulisha na hali ngumu ya maisha inayowakabili. Watoto wanapokabiliana na changamoto katika maisha huanza kutumia dawa za kulevya ili tu wajiliwaze kutokana na madhila ambayo wanapitia.Katika riwaya ya Nguu Za Jadi,wasichana wadogo waliozalishwa wakiwa wadogo wanaonekana wakinusa gundi chini ya viambaza vya maduka(uk 137). Vilevile,katika riwaya ya Chozi la Heri,Dick analazimika kuzitumia dawa za kulevya wakati wa kuzilangua kwa miaka kumi baada ya kutekwa nyara na Sauna na kuuzwa kwa Mzee Buda.Pia,Kipanga anaishia kutumia vileo ili kujisahaulisha kusambaritika kwa familia yao.Kipanga alianza kuchovya kidogokidogo akiwa kidato cha pili baada ya aliyedhania kuwa baba yake kumkana (uk 143). Mapendekezoya kukabiliana na Ukiukaji wa Haki za Watoto Assumpta K.Matei na Clara Momanyi wanapendekeza baadhi ya hatua zinazoweza kutumika ili kutatua tatizo hili la ukiukaji wa haki za watoto.Kulingana na Goldstorm(1979:340), suluhisho la tatizo huwa bora katika kuimarisha maisha ya watoto katika jamii. Miongoni mwa mapendekezo yaliyotolewa na waandishi hawa wawili ni pamoja na nafasi ya maafisa wa polisi kukabiliana na wale ambao wanakiuka haki za watoto. Polisi wana wajibu wa kuchunguza makosa yote ya jinai.Makosa yanayotendewa watoto huwa nyeti sana na mara nyingi huhitaji polisi kufanya kazi na mashirika mengine katika kufanya uchunguzi.Hatua IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 15 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI inayochukuliwa na maafisi wa polisi ya kuwakamata Sauna na Bi.Kangara na kuwashtaki kwa ulanguzi wa binadamu kisha kufungwa jela miaka kadha na kazi ngumu inayaokoa maisha ya watoto waliodhulumiwa na wawili hao (uk.158).Pia,polisi wanamwokoa Mwaliko kutoka kwa Bi.Kangara na kumkabidhi kwenye kituo cha Benefactor (uk.159).Vilevile,katika Nguu Za Jadi,polisi wanamkamata Sihaba kwa kuwahusisha wasichana wadogo katika biashara ya ukahaba kwa manufaa yake.Vilevile,maafisa wa polisi wanawaandama wazazi wa wasichana waliotumika katika ukahaba ili kuchukuliwa hatua za kisheria. Pili,ni wajibu wa wanajamii kuwasaidia watoto wanaodhulumiwa.Hatua iliyochukuliwa na Bi.Kimai na Bw.Tenge katika Chozi La Heri ya kumchukua Chandachema kama mwana wao baada ya kukosa hisani kwa Satua inamsaidia sana kwani anapata kuishi na wawili hawa na kulelewa kama mwanao.Pia,Neema anachukua wajibu wa kukiokota kitoto kilichokuwa kimetupwa kwenye jaa la taka,anakipeleka katika kituo cha polisi na baadaye katika makao ya watoto mayatima ya Benefactor (uk.161). Tatu,waandishi wanapendekeza kuwepo kwa vituo vya watoto.Vituo hivi vikiwepo huweza kuwaokoa watoto kutokana na vitendo viovu.Katika Chozi La Heri,mwandishi amefaulu kutumia kituo cha Benefactor katika kuendeleza hoja hii.Watoto wanaookolewa kutokana dhuluma wanazozipitia kama vile Mwaliko kutekwa nyara na Sauna kisha kuokolewa na maafisa wa polisi anapelekwa katika kituo hiki (uk.159).Vilevile,kitoto kilichookotwa na Neema kutoka jaani la taka anakipeleka katika kituo hiki cha Benefactor (uk.161) ambacho ni makao ya watoto wa mayatima.Vilevile,katika Nguu Za Jadi,watoto waliookolewa baada ya kutoroka shuleni ili kufanya biashara ya ukahaba na kukosa mahali pa kwenda waliwekwa kwenye makao ya watoto (uk.143). Nne,ni wajibu wa Mashirika ya Kidini kuwasaidia watoto wanaodhulumiwa.Hatua inayochukuliwa na Shirika la Kidini la Hakikisho la Haki na Utulivu ya kumpeleka Chandachema kwenye makao ya watoto mayatima ya Jeshi La Wajane wa Kristu inamsaidia sana.Chandachema anapata kuishi kule kama vile nyumbani kwao huku akiendelea na masomo katika shule ya Tangamano (uk.108). Tano,ni wajibu wa jamii kuvipinga vitendo vya ukiukaji wa haki za watoto.Wajibu huu unahusisha wakubwa na wadogo.Assumpta K.Matei katika Chozi La Heri anatoa mfano wa bibi yake Pete anapojaribu kupinga kuozwa kwa Pete kwa mzee Fungo kwa kumwona bado mtoto anayestahili nafasi ya kukua,kupata masomo na baadaye kujichagulia mchumba (uk.148),japo bado Pete anaozwa na mama na wajomba wake. Sita,waandishi wanapendekeza kuwa ni jukumu la watoto kuzipinga dhuluma zinazowakabili.Assumpta K.Matei anamtumia mtoto Dick anayeamua kuyabadilisha maisha yake.Baada ya miaka mitano ya kulangua dawa za kulevya.Dick anafanya uamuzi wa kuacha biashara hii haramu na kufungua biashara ya kuuza vifaa vya simu (uk.110). Hatimaye,waandishi wanapendekeza kuwa ni wajibu wa serikali kuwasaidia watoto ambao haki zao zinakiukwa.Clara Momanyi anatoa mfano wa serikali ikihimizwa kuwasaidia wasichana ambao walihusishwa katika biashara ya ukahaba na Sihaba ili warudi shuleni (uk. 143) IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 16 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI Hitimisho Kwa ujumla, ukiukaji wa haki za watoto una athari mbaya kwa ustawi miongoni mwa jamii.Ni muhimu kutambua kuwa,watoto ni amali ya jamii na wanapaswa kulindwa dhidi ya dhuluma zozote zile. Kutokana na mapendekezo yaliyotolewa,wanajamii,maafisa wa usalama na mashirika mbalimbali yana wajibu wa kuzilinda haki za watoto.Vilevile,watoto wana jukumu la kupinga dhuluma ambazo wanatendewa. MAREJELEO Amulenga, C.M. na Amulenga, A.V. (2009) Solving Problems Occuring in Early Marriages. Nairobi: Focus Publishers Atieno, W. (2014) ‘Mama ajifungua ndani ya TukTuk’. Taifa Leo, Septemba 9, kur.1,2 Bakize, L.. (2014). Utangulizi wa Fasihi ya Watoto. Dar es Salaam: Maccony Printing Press. Behnam, N. (2008) ‘Kikanda, jamii na watoto’:Ripoti ya Kikanda ya kuanza kujifunza:Kuwawezesha jamii kuhusu ustawi wa watoto.Washington,DC. Boss, P. (1998) Family Stress Management. Newbury Park, California: Sage Publications. Burke, C. (1999) Covenanted Happiness, Love and Commitment in Mariage, 2nd Ed. New Jersey: Screptree Publishers. Bronfenbrenner,U.(1979).’Elimu ya ustawi na uhusiano wa binadamu na mazingira’.Asili na desturi ya kutathmini vijiji kushiriki.Cambridge,MA:Uandishi wa Chuo Kikuu cha Harvard. Cancer Global Statistics (2014).www.int/media centre/factsheets/fs297/en/. Chambers,R. (1994).’Asili na desturi ya kutathmini vijiji kushiriki’.Maendeleo Duniani, 22.953- 969’. Chapman, R. (1982) The Language of English Literature. London: Edward Arnold Publishers. De Genors, M.K (2008) Inmate, Relationship, Marriage and Families. Seventh edition.New York:Mc Grace Hill. Drabble, M. (1995) The Oxford Companion to English Literature.New York: Oxford University Press. Farouk, M.T. (1974) Uchambuzi wa Maandishi ya Kiswahili. Nairobi: Oxford University press. Gitau, E. (2014) ‘Unyanyasaji Dhidi ya Wanaume katika Fasihi Andishi ya Kiswahili’.Tasnifu ya uzamili Chuo kikuu Cha Kenyatta. Habwe, J.H. (2005) Paradiso. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation. IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 17 http://www.int/media centre/factsheets/fs297/en/ IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI Johnson, T. (2002) “ Violence and Abuse of Women and Girls in Kenya, Population Communication Africa.Nairobi: New World Printers. Karanja, D.W. (2008). Usawiri wa Masuala-Ibuka katika hadithi za watoto.Tasnifu ya uzamili. Chuo kikuu cha Kenyatta. Khamis, S.A. (2012) “ Riwaya Mpya ya Kiswahili. Utandawazi au Utandawizi? Lugha ya Riwaya Mpya Ya Kiswahili Inavyodai”. Bayreuth University. Krueger, A. Thompson, G. na Crispin, V. (2013).’Kufijunza kutoka kwa mifumo ramani ya kulinda watoto na uchambuzi katika Afrika Magharibi’: Maana ya Utafiti na Sera.Sera za Kimataifa,5,47-55. McKay, S., na Mazurana, D. (2004).’Wako wapi wasichana?’ Montreal, Canada: Kituo cha Kimataifa kwa Haki za Binadamu na maendeleo ya Kidemokrasia. Panter-Brick, C., na Leckman, J. (2013). Tangazo mfululizo la Mhariri: Kuimarisha kwa ustawi wa mtoto –Njia zilizounganika kwa hali njema.Jarida la Saikolojia na Taaluma,Tiba ya Ugonjwa wa Akili kwa Watoto, 54,333-336. Thompstone, G. (2010). Mapping na Uchambuzi wa mfumo wa kulinda watoto nchini Sierra Leone.Hong Kong,China: Watoto wa mpakani (Child Frontiers). UNPD. (2013) Dalili za Umaskini na Maendeleo, Sierra Leone.Imepatikana kutoka hdstats.undp.org UNICEF. (2013). Ukeketaji na Kutahiri wanawake : Maelezo ya takwimu na ugunduzi wa mienendo ya mabadiliko.New York, NY: Mwandishi. UNICEF,UNHCR,Kulinda Watoto (Save the Children), na Maono Duniani (Maono ya Dunia).(2013).Njia bora ya kuwalinda watoto wote: Nadharia na Mazoea ya mfumo ya kulinda watoto,ripoti ya mkutano.New Delhi, India: Mwandishi. Wessells, M.G. (2006). Wanajeshi watoto: Kutoka kwa Vurugu hadi Kulindwa. Cambridge, MA: Uandishi wa Chuo Kikuu cha Harvard. Wessells, M.G. (2009a). Je, tunajifunza nini kuhusu kulinda watoto katika jamii? Kikanda cha mapitio ya ushahidi juu ya jamii kuhusu utaratibu wa kulinda watoto katika mazingira ya kibinadamu na maendeleo.London, England: Kulinda Watoto (Save the Children). IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 18 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || UKIUKAJI WA HAKI ZA WATOTO KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:MFANO WA CHOZI LA HERI NA NGUU ZA JADI Whitney,S.D., Tajima, E.A.,Herrenkohl,T.I.,& Huang, B. (2006). Defining child abuse: Exploring variations in ratings of discipline severity among child welfare practotioners. Child and Adolescent Social Work Journal, 23, 316-342. Yeo.L.S., & Choi, P.M. (2011). Cognitive-behavioural therapy for children with behavioural difficulties in the Singapore mainstream school setting. School Psychology International,32,616- 631. IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 19 Jackline Njeri Murimi, Chuo Kikuu cha Tom Mboya IKISIRI Usuli wa mada Tatizo la utafiti Ukiukaji wa haki za watoto katika riwaya zaChozi la Heri na Nguu za Jadi Mauaji Ndoa za mapema na za lazima Kukatizwa elimu Ubaguzi wa watoto Uavyaji mimba Madhara yanayotokana na ukiukaji wa haki za watoto Kukimbia nyumbani Kutatizika kimasomo Ukosefu wa mahitaji ya kimsingi Watoto kuishi katika mazingira yasiyokuwa na amani na hatarishi Matumizi ya dawa za kulevya Mapendekezoya kukabiliana na Ukiukaji wa Haki za Watoto Hitimisho MAREJELEO