IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA Jackline Njeri Murimi, Chuo Kikuu cha Tom Mboya na Solomon Muli, Chuo Kikuu cha Mount Kenya IKISIRI Suala la imani katika Mungu ni nyeti na linatiliwa maanani na binadamu katika tamaduni mbalimbali kote duniani kama njia mojawapo ya kujaribu kutafuta majibu ya changamoto anazokubana nazo kila uchao. Katika jamii nyingi za kiafrika,dini ni mfumo wa maisha (Mbithi 2011 )ambapo kila mwana jamii alihitajika kushiriki. Hata hivyo, suala hili la kidini linaonekana kuwatamausha vijana wengi na kufifisha imani yao katika dini. Hivyo ,utafiti huu ulinuia kuchanganua baadhi ya athari za udhanaishi wa dini kwa vijana kwa kurejelea riwaya ya Paradiso na Kidagaa Kimemwozea zilizoandikwa na John Habwe na Ken Walibora mtawalia kwa kuchunguza jinsi John Habwe na Ken Walibora wanavyoangazia udhanaishi wa kidini katika jamii . Katika kulizamia suala hili makala hii iliongozwa na nadharia ya udhanaishi iliyoasisiwa na Mwanathiolojia kutoka Denmaki(1813-1855),Fredrick Nietzsche,Martin Heidegger,Gabriel Marcel na Karl Jaspers waliotokea karne ya 20 na Jean Paul Satre Mfaransa aliyetokea baada ya vita vya pili vya dunia. Mihimili yake ilisaidia kufikia malengo ya yetu. Mihimili mikuu ya nadharia ya udhanaishi ni pamoja na;kutilia mkazo matatizo halisi yanayomsibu mwanadamu na kuwa na imani ya kijozi juu ya imani ya kuishi, inapalilia kutokuwepo kwa mungu na uumbaji wake wa ulimwengu,inatilia mkazo kuwa juhudi za mtu kujisaka au kujaribu kupambana na maisha huishia katika mauti, maudhui yake ni kama vile uhuru wa mtu binafsi kuweza kufikiri halafu kutoa jawabu lake. Nadharia husimulia taabu na kuchoka na hali ambazo husumbua yanayotatiza mwana wa adamu, nadharia hii inajadili mkengeuko,nadharia hii inachora taswira ya mateso anayopitia mwanadamu duniani, nadharia hii inatilia mkazo kuwa maisha yamejawa na utupu na kihoro hasa kuhusu siku za kesho.Maisha yamejawa na ubwege na huhakikisha binadamu kuwa mwisho wa maisha ni kifo.Nadharia hii ilifaa utafiti kwani ilitumika kueleza jinsi baadhi ya vijana waumini wavavyoyaona maisha jambo ambalo linawafanya watamaushwe na dini kila uchao. Nadharia hii ilitumika kupambanua ukweli wa je ni lipi ambalo baadhi ya vijana katika jamii wamejua hivi karibuni ambalo mababu zao hawakufahamu hapo awali?Utafiti ulifanyika maktabani kuliko na vitabu, majarida,matini na magazeti na wa mtandaoni ambapo data ilipatikana kutokana na tasnifu zilizoandikwa kuhusu mkengeuko wa imani za kidini.Sampuli ya kimaksudi ilitumika katika kuteua riwaya ya Paradisona Kidagaa Kimemwozea. Mbinu anuwai za kimaelezo zilitumika katika kuchambua data na kuiwasilisha kwa lugha ya nadhari kuambatana na lengo la utafiti. Maarifa yaliyopatikana katika utafiti huu yatakuwa na mchango mkubwa katika maarifa yaliyopo kuhusu vijana na masuala ya dini katika jamii. IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 20 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA Utangulizi Kulingana na Cames (1984), udhanaishi ni falsafa inayoshughulikia maswali kuhusu maisha ya mwanadamu. Kwa jumla, ni mtazamo unaokagua kwa mapana mwanya alio nao mwanadamu kwenye ulimwengu anamoishi. Vile vile, ni falsafa inayoelezea mahusiano yaliyomo kati ya mwanadamu na Mungu na ikiwa mwanadamu huyu anapaswa kuamini kuwepo kwa Mungu au la. Taabu na matatizo anazokutana nazo mwanadamu zinamfanya kuwa na maswali chungu nzima kuhusu maisha haswa juu ya maswala ya uwepo wa maadili na kiroho. Kwa mujibu wa Mark Sanchez (2021), dini ni mfumo wa imani, mila na alama zilizoanzishwa karibu na wazo la uungu au kutoka takatifu. Dini ni mafundisho yaliyoundwa na seti ya kanuni, imani na mazoea anazoenzi binadamu anapokosa suluhu mwafaka kuhusu hali nyeti anazokutana nazo maishani. Baada ya zama za giza, mwanadamu alianza kujisatiti kutafuta suluhu la maisha kwa nyanja tofauti ikiwepo dini. Dini ni neno linalopatikana uarabuni ‘Diin’ linalomaanisha ‘imani ya umoja wa mweyenzi Mungu’ desturi,tabia au mazoea. Kwa jumla neno hili husisitiza maana ya mwanadamu kuitambua nguvu kubwa kumliko na ambayo inautawala ulimwengu mzima na hasa Mungu au Miungu ya mtu binafsi kama mwongozo wa kiroho, kiimani na kiibada. Dini ndio mafundisho ambayo huunganisha sana mwanadamu na Mungu au Miungu, yaani ni hatua na athari za kuunganisha tena Mungu na wanadamu. Neno dini linaweza kutumika kiishara kuashiria kama shughuli au wajibu unafanywa kila wakati na kwa ukali.Mifano ya dini duniani ni ile ya Ukristo iliyo na waumini bilioni 2.1, ile ya Uisilamu yenye waumini bilioni 1.9 na ile ya Ubudha iliyo na waumini bilioni 1.6. Kulingana na vitabu vya kihistoria vya dini, dini zilizoimarika zilizionekana kwa mara ya kwanza baada ya wa kazi, ukuzaji wa kilimo ambapo wakati mwingi ulitumiwa kutazama maumbile. Dini za Neolithic ziliundwa karibu na vitu vitatu; hekalu, kuhani na dhabihu(matoleo) ambayo pia ni kielelezo cha utambuzi wa takatifu na unajisi. Kazi ya dini ni kuimarisha mfumo wa maadili yanayohusu mshikamano wa kikundi cha jamii kulingana na mradi wa kawaida na kuunda kiwango fulani cha kuridhika kiroho kupitia imani kushida kuteseka na kufikia furaha.Dini zote zina misingi ya kihistoria zilizoitwa hadithi za uwongo zikieleweka kama hadithi zinazoelezea asili ya maisha, kuhalalisha hali yake na makadirio yake ya baadaye. Dini zote zinaungwa mkono na mikondo tofauti ya mawazo ambayo hujaribu kueleza sisi ni kina nani na kwa nini tumekuja ulimwenguni. Katika tamaduni zilizo na maandishi, dini zinategemea maandishi ya asili takatifu ambayo huleta wafuasi wao karibu na jamii moja ya kiroho.Kwa mujibu wa vitabu vya kihistoria, dini za kigeni zilisambazwa maeneo mengi ya dunia na Wazungu kutoka Bara la Ulaya na Waarabu kutoka Mashariki ya mbali kabla na baada ya zama za giza.. Yaliyoandikwa Kuhusu Mada Makoyo (2014),katika tasnifu yake anajadili jinsi elimu ya Kenya inavyotamausha wasomi kwa kuegemea kwenye dini ya Kikristo ambayo inaamini msomi kuwa na imani ya kila kitu bila ya kuuliza swali lolote. Kulingana na Makoyo ,kuamini huku kunawafanya watu washindwe kujitegemea kwa sababu wanahofia kufanya maamuzi muhimu maishani mwao kwa hofu ya kupata ghadhabu kutoka kwa Mungu. Hali hii inamfanya mwanadamu kujiona kama kiumbe kisicho na akili ya kufanya maamuzi yoyote na hivyo kumkatisha tamaa zaidi. Kazi hii ya Makoyo ni muhimu kwa mtafiti kwani inarejelea jinsi elimu ya taifa la Kenya inavyowakatisha IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 21 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA wasomi tamaa. Tofauti ya kazi hii na ya mtafiti ni kuwa kazi yake iliepuka utamaushi unaosababishwa na elimu na kujikita kwa sababu za kidini zinazotamausha vijana, athari za utamaushi huu na njia zinazoweza kuangaziwa kuleta suluhu mwafaka za utamaushi huu miongoni mwa vijana. Nyamemba,R( 2016 ) Anasema kuwa , vijana wanapokosa kupata matarajio waliyokuwa nayo kwa nyanja mbalimbali kama vile elimu na ajira ,wengi wao hutamauka na kuamua kujitosa kwenye dawa za kulevya za kila aina zikiwemo bangi,ugoro na singara. Hali hii imewafanya wengi wao kukosa faida katika jamii. Kazi hii ya nyamemba inafafanua kuwa vijana wengi hukatishwa tamaa na ukosefu wa masuala ya kiuchumi kama vile elimu na ajira. Masuala yaliyoko kwenye kazi hii yalifaa mtafiti kwani yamejikita kwenye udhanaishi kama yake tu ila ni tofauti na utafiti wake ambao uliepuka masuala ya uchumi na badala yake kuegemea tamaa inayokatishwa na masuala ya imani za kidini miongoni mwa vijana huku sababu,athari na mapendekezo mwafaka ya hali hii zikiangaziwa. Matundura(2019)huku akimnukuu mwalimu wake wa chuo kikuu Bw.Crispine Isaboke,anasema kuwa pindi mtu anapozaliwa,moyo wake huwa kana kwamba umetiwa majira mithili ya saa na hajui hatima yake ila inajulikana na Mungu. Anadai kuwa chochote anachoamua mwanadamu kilipangwa pindi tu alipozaliwa na kuwa maamuzi yake yote hudhibitiwa na jaala jambo ambalo linatamausha kiumbe huyu zaidi. Kazi hii inaangazia mwanadamu ambaye ametamaushwa na hali ya kufahamu kuwa maisha yake yote. hudhibitiwa na jaala na yashaapangwa tangu mwanzoni na kuwa hana uwezo wa kubadili chochote maishani kwani lililopangwa kwake ndilo humkuta maishani. Utafiti wa mtafiti uliangazia sababu za masuala ya kidini zinavyotamausha vijana, athari zake kwa vijana hawa pamoja na mapendekezo ya kushughulikia utamaushi huu ambapo masuala mengi husababishwa na binadamu mbali sio jaala. Wasike, K (2020) huku akinukuu riwaya ya Ua la Faraja katika tawasifu yake , mhusika 0molo alitamaushwa na maisha kiasi cha kuishi kwa muda mrefu bila kuoa. Omolo aliishi kwa kujiuliza maswali mengi kuhusu maisha,” Alishangaa kwa nini hata yule mwenye maisha ya shida anapoungua na kukaribia kifo ili hafurahi kuisha kwa shida zake akifa bali huhangaika kujitibu ili apone aendelee na shida zake (uk23) vile vile mhusika Queen haoni faida ya kuishi na hakuna haja kwa kutia bidii maishani kisha afe. Hili linakazwa na hali yake kuwa alikuwa na ugonjwa wa UKIMWI. Mtafiti wa kazi hii amezingatia utamaushi wa maisha kwa jumla unaowafanya wahusika wengine kukosa tamaa ya kufanya lolote maishani kwani mwishoni mna kifo. Kazi yenyewe itafaa mtafiti kwani ina misingi ya mathara yanayosababishwa na utamaushi. Kazi ya mtafiti ilifafanua mathara haya kwa upana kwenye kipengele cha utamaushi wa kidini huku yakiegemezwa kwa sababu zake na kisha kuangazia mapendekezo ya kukabiliana na hali hii tata. Abdallah,M.(2021) Anasema kuwa baada ya vita vya pili vya dunia,maisha yalionekana kutokuwa na maana kwa jinsi vita hivyo vilivyoangamiza mamilioni ya watu. Aidha maisha yalikuwa magumu kwa kuwa uchumi uliporomoka. Hali hii ya taabu ya kisaikolojia ,ilifanya watu wengi na hasa kutoka magharibi wadai kuwa Mungu amekufa kwa sababu kama angekuwa hai asingewaruhusu kuteseka na kuacha wengi waangamie kama ilivyotokea. Kazi ya Abdallah inaangazia utamaushi uliosababishwa na vita ambao uliathiri watu wa vitengo tofauti barani Ulaya.kazi hii itafaa mtafiti sana kwani inajadili kwa mapana suala la utamaushi. Tofauti na kazi IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 22 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA yake ni kuwa upande wake aliangazia utamaushi unaosababishwa na imani za kidini kwa vijana pekee katika jamii badala ya kuangazia wanaumri wote kwa jumla,sababu za hali hii kutokea,athari zake na kisha mapendekezo mwafaka ya kukabiliana na hali yenyewe. Adria Fuluge (2022) huku akiangazia riwaya ya Rosa Mistika katika jarida lake ,anajadili jinsi wahusika mbalimbali wanavyotamaushwa na maisha na kukosa suluhu kwa vitengo vyote ikiwemo dini hadi kufikia maamuzi ya kujiua. Ingawa kwa mkondo na mchakato mrefu, Rosa anapitia hali nzito ya maisha akitafuta maana ya maisha na anapoona kuwa hakuna suluhu atakalopata anatamauka na kuamua kujitoa uhai. Rosa anafuraia kifo chake kwa sababu kwake huo ndio uhuru aliokuwa anautafuta kama suluhisho la taabu zake.(uk 161). Adria amejikita kwenye utamaushi wa wahusika wa umri tofauti na hasa wa jinsia ya kike. Kwa upande wa mtafiti alinuia kushughulikia utamaushi wa kidini miongoni mwa wahusika vijana wa jinsia zote huku akizamia kinachosababisha utamaushi huu, athari zake kwa vijana hawa pamoja na njia mwafaka zinazoweza kutumiwa kukabiliana na hali hii nyeti katika karne ya 21. Hivyo kutokana na kazi hizi zote bado kuna mwanya uliojitokeza na ndio maana utafiti huu ulinuia kuuziba kwa kuzingatia suala la utamaushi wa kidini na athari zake kwa vijana kwa mujibu wa riwaya ya Paradiso ya John Habwe na KidagaaKimemwozea ya Ken Walibora Muhtasari wa Riwaya ya Paradiso Riwaya ya Paradiso iliandikwa na John Habwe na kuchapishwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2005. Kulingana na TUKI 2013:451,neno ‘paradiso’ lina maana ya edeni,pepo au firdausi. Kulingana na TUKI 2013:458,neno ‘pepo’ lina maana ya mahali patukufu panapoaminiwa kuwa baada ya kufufuliwa na kulipwa matendo yao mazuri walioishi kulingana na amri za Mungu wataishi milele. Ingawa Paradiso ni riwaya yenye mkusanyiko mwingi wa maudhui,maudhui makuu kwenye riwaya hii ni yale ya Unafiki wa kidini unaoendelezwa na viongozi wa dini pamoja na waumini wake katika matukio mbalimbali yanayopatikana kwenye riwaya hii. Unafiki huu wa kidini unaotokea unaendelezwa na wahusika tofauti na kudhihirika kwa matendo kama vile ya;ufisadi,mipango ya kando,vita baina ya waumini,chuki,anasa,biashara kwa jina la Mungu na kujitajirisha kwa kutumia Neno la Mungu miongoni mwa vitendo vingine. Matendo haya ni kinyume na mafundisho ya dini. Riwaya hii ya Paradiso imengawanyika katika sura kumi na nane zilizomo kwenye kurasa 230 ambazo kila sura ina mvuto wake unaomfanya msomaji kuwa na ari ya kubukua kitabu chenyewe kujifahamisha zaidi kuhusu maudhui makuu ya unafiki wa kidini. Ingawa dini hudhaniwa na jamii kama chombo cha usalama na afueni kwa ulimwengu uliovurugika,yanayojitokeza katika riwaya hii ni tofauti kabisa kwani baadhi ya viongozi wa dini na washirika wao wanatenda kinyume na matarajio na mafundisho ya dini. Maadili ya baadhi ya waumini yameoza kiasi cha kuwafanya vijana wanaozidi kuziduka kila uchao kukosa kuona maana ya kujihusisha na dini. Hata hivyo,riwaya hii ya Paradiso inadodoa maudhui mengine kama vile,Ndoa,Ukware,Nafasi ya kanisa kwenye jamii,Ufisadi, Tamaa, Elimu,Migogoro,Umaskini na Utabaka miongoni mwa maudhui mengine. Riwaya hii inaweza kuainishwa kama ya uhalisia kwani masuala yanayojadiliwa ndani ya kitabu yanalingana na yale IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 23 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA yanayoshuhudiwa kwenye ulimwengu wa kawaida tu. Maabadi zinawakilishwa na makanisa ya Bethany na lile la NewJerusalemu ilhali viongozi wakuu wa dini wanawakilishwa na Askofu Joshua na mkewe Kasisi Lona pamoja na Mhubiri Michael. Muhtasari wa Riwaya ya KidagaaKimemwozea Riwaya ya KidagaaKimemwozea iliandikwa na Ken Walibora na kuchapishwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2012. Riwaya hii imegawanyika katika sura 10 zilizo kwenye kurasa 162. Ingawa riwaya hii ina masuala chungu nzima yanayojadiliwa na mwandishi,suala kuu lililopo kwenye kitabu hiki ni namna ndoto walizokuwa nazo Waafrika walipokuwa wakipigania uhuru zilipogeuka na kuwa jinamizi isiyotarajiwa. Afrika inawakilishwa na taifa la Tomoko na eneo dogo la Sokomoko linaloongozwa na Mtemi Nasaba Bora.Wazalendo na wanyonge waliokuwa mstari wa mbele kupigania uhuru na kumfukuza mkoloni mweupe waligeukwa na viongozi wa kiafrika pindi tu uhuru ulipopatikana. Neno ‘Kidagaa Kimemwozea’ ni istilahi iliyotumika kuonyesha namna matarajio ya Waafrika yalivyotingwa na uongozi wa Waafrika wenzao kwa kukosa kutimiza ahadi zao na kutamausha nyoyo zilizokuwa na matarajio makuu baada ya uhuru. Kulikuwa na wanyonge waliowakilishwa na wahusika kama vile Imani,Amani,Matuko Weye,Uhuru na DJ miongoni mwa wengine ambao nyoyo zao zilitamauka kiasi cha kupatwa na msongo wa mawazo ulioathiri na kuvuruga akili zao. Familia za waliopigania uhuru kama vile Mwinyihatibu Mtembezi hazikuwa na chochote cha kujivunia ila kutaabikia kwenye nchi yao huru. Maudhui makuu kwenye riwaya hii ni yale ya Usaliti ambapo raia wanasalitiwa na viongozi wao kwa kupitishwa dhuluma za kila aina na hata wengine kuuawa pasipo na hatia. Raslimali zinazopaswa kuauni wananchi zinawakilishwa na maji ya Mto Kiberege ambapo badala ya maji haya kuleta uhai yanakisiwa kuwa ni maji ya mauti. Hadithi ya kitabu hiki inasawiriwa kupitia safari ya wahusika wawili Amani na Imani ambao wanaanza safari kutoka makwao kuelekea eneo la Sokomoko kusaka kazi ambazo labda zingeleta afueni kwa maisha yao. Wahusika hawa wanavunja mwiko kwa kunywa maji ya Mto Kiberege yaliyodhaniwa na wenyeji kuwa maji ya mauti. Kitendo cha kutoathiriwa na maji yale kinabadili dhana ya wakaaji wa Sokomoko na kuweka peupe kuwa hata haramu inaweza kuwa halali na halali kuwa haramu. Wanapofika katika kijiji cha Sokomoko, Amani na Imani wanaajiriwa na ndugu wawili;Mtemi Nasaba Bora na Mwalimu Majisifu mtawalia. Ingawa waajiri hawa walikuwa dhalimu kwa Amani na Imani, vijana hawa wanafanya bidii za mchwa kwa kazi zao kwani nia yao ilikuwa kufanya upelelezi ili kugundua waliopoka mali ya familia zao. Inadhihirika kuwa jasho la wasomi hufaidi wengine kwani Mwalimu Majisifu ni mwizi wa miswada ya wasomi ambapo badala ya kuchapisha kazi za wasomi hawa,anawajulisha kuwa kazi zao ni chapwa na kisha kuzichapisha kwa jina lake na kuziuza. Hata hivyo,Amani na Imani wanaongoza umati wa watu na kuwazidua kuhusu haki zao walizonyimwa na viongozi wao. Kupitia kwao inadhihirika kuwa Mtemi Nasaba Bora ambaye anawakilisha viongozi wa Afrika baada ya uhuru ni mnyakuzi mkuu wa ardhi za wanyonge. Inadhihirika kuwa viongozi hubadili vyeti vya kumiliki ardhi na kuwapa wenyeji vyeti bandia kwa minajili ya kunyakua ardhi zao. Baada ya siri za Mtemi Nasaba Bora kuwekwa wazi anajiona ombwe tupu na asiyeweza kuishi kwa aibu miongoni mwa watu wake na kwa hivyo anaamua kujitoa uhai kwa kujitia kitanzi. Amani anayewakilisha wanamapinduzi anaongoza utawazaji wa mtemi mpya na kuahidi kuwa makosa yaliyotokea awali hayatarudiwa. Pia anawazidua raia kuwa macho kukabiliana na dhuluma yoyote ile ambayo ingezuka na kuendelezwa na kiongozi mwingine. Mabadiliko yanayoletwa Sokomoko IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 24 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA na Amani na Imani yanadhirisha kuwa hakuna jambo lisilowezekana Barani Afrika . wanyonge wakiungana pamoja wanaweza kuleta mageuzi makubwa na kubadilisha hali ya kiuchumi ya jamii zao. Riwaya hii pia ina maudhui mengine kama vile;ufisadi,unafiki wa kidini,dhuluma,ulevi,wizi na ukware miongoni mwa maudhui mengine. Athari za Udhanaishi wa Kidini kwa Vijana Vijana Kuchoshwa na Utaratibu wa Maabadani. Maabadi ni mahali popote pa kufanyia ibada kama vile hekalu, kanisa au msikiti. Pia ni sehemu au eneo maalumu lililojengwa ambalo mtu au kundi la watu hukutana kufanya ibada au kujifunza masomo ya dini. Hata hivyo mnamo miaka ya hivi karibuni kumeibuka madhehebu ambayo hayafuati utaratibu wowote wa kufanya ibada zao kwa tetezi kuwa ibada inapaswa kuongozwa na Roho Mtakatifu. Hali hii imechosha vijana wa karne ya 21 na baadhi yao kuacha kuhudhuria ibada zenyewe na badala yake kujihusisha na starehe zao siku zilizotengwa za ibada. Suala hili la vijana kuchoshwa na taratibu za ibada limekuwa likiangaziwa na waandishi tofauti waliobobea na wale chipukizi. John Habwe Katika riwaya ya Paradiso, anamwangazia kijana Kyalo aliyeichukia dini tangia akiwa kijana, sala za dini zilimchosha na aliona tu watu wengi walijihusisha na dini tu kwa sababu ya dhiki. Kyalo alichukia dini kiasi kwamba hata baada ya kuoa mke wake Salome alimwona mjinga kwa kujishughulisha na hadaa za wahubiri. Madai ya Kyalo yanadhihirika kwenye dondoo ifuatayo ; ‘…Kyalo hakupenda masuala ya dini. Tangu alipozaliwa hakuwa amekwenda kanisani. Hakuonahajayoyoteyakujidhikinasalandefuambazozilichosha. Hakupendahasasalazakelele. Alinonakuwamkewakealikuwamjingakwakujishughulishanahadaazawahubiri’ (uk49) Kutokana na utafiti huu ni dhahiri shahiri kuwa Kyalo, anayewakilisha baadhi ya vijana katika jamii hakupenda kelele nyingi zilizopigwa na waumini wakati wa ibada na hivyo basi akafanya maamuzi ya kujiepusha na masuala ya dini. Hata alipokua na kuwa na familia msimamo wake ulibaki pale pale ; masuala ya dini haikuwa moyoni mwake kamwe. Vijana wa Kike Kukataa Kuolewa na Wahubiri. Ndoa ni muungano kati ya watu wawili au zaidi unaokubaliwa na kuheshimiwa na jamii. Tukio la kuanzisha ndoa linaitwa harusi. Kabla ya ndoa, kuna kipindi cha uchumba ambapo watu hao wawili waliokubaliana wanachunguzana tabia na kujifunza au kujuana zaidi. Katika tamaduni nyingi duniani, uhusiano huu huwa ni kati ya mwanamume na mwanamke ila miaka ya hivi karibuni kumekuwa na msukumo wa jamii fulani hasa kutoka Ulaya na Marekani kufanya ndoa ya watu wa jinsia moja. Katiba ya Kenya kifungucha 4 ibaraya 9 kila aliyefikisha miaka kumi na nane ana haki ya kuolewa au kuoa na kuwa na familia. Hata hivyo, ndoa haipaswi kuwa ya lazima na kila mmoja anapaswa kujichangulia mchumba amtakaye. Miaka ya hivi karibuni ndoa imekumbwa na nyufa ambazo zinatishia kusabaratisha taasisi hii iliyoasisiwa na mababu zetu kabla ya karne ya ishirini na moja. Linalotilia msumari moto kwenye kidonda ni kuwa hata ndoa za wahubiri na viongozi wa dini zimekuwa na atiati na migogoro isiyokoma jambo ambalo linawafanya vijana na hasa wa kike kuwa na hofu ya kuolewa na viongozi wa dini. Katika IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 25 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA riwaya ya Paradiso, kijana wa kike Nice ambaye pia ni bintiye Askofu Joshua na kasisi Lona wa kanisa la NewJerusalemu, anakataa katakata pendekezo la wazazi wao kuolewa na mhubiri Michael. Maisha ya unafiki wa kidini aliyoyaona na wazazi wake. Nice alikata kauli ya kutoolewa na mhubiri liwe liwalo kama inavyoelezwa na dondoo iliyo hapa chini ; ‘… Joshua na Lona walikaa hapo kumkabili Nice kuhusu pendekezo lao la kuolewa na Michael.Bila kificho Nice aliwaeleza hawezi. ‘’kwa nini mnitafutie mama, mama ?’’. ‘’Hebu sikiliza mama, huyo mume ni kufu yako, ni mtu wa dini na ni rika lako’’ alisema Lona…’’ Najua ni mtu wa dini, lakini mimi mama si mtu wa dini’’ Nice alisema kwa maringo’. (.uk 73) Usiku mzima Askofu Joshua na mkewe walimkorofisha binti yao angalau abadili msimamo wake na kukubali matakwa yao lakini Nice alibakia kwenye msimamo wake wa kutoolewa na mtu wa dini tena mhubiri. Nice alitamani kuachiwa uhuru wa maamuzi yake kama ataolewa au la. Alihofia kuolewa na mtu wa dini kwani alikuwa ameshuhudia mengi kwenye ndoa ya wazazi wake licha ya kuwa watumishi wa Mungu. Hata baada ya wazazi wa Nice kuwa na hasira na kumtishia binti yao kutafuta wazazi wengine endapo angekataa pendekezo lao la kuolewa na mhubiri Michael, Nice alisimama kidete kuwa yeye sio mtu wa dini na hataki kuolewa na mtu wa dini. Kwa vile fasihi ni kioo cha jamii, utafiti huu unatambua Nice ambaye ni kiwakilishi cha vijana wa kike kwenye jamii ya karne ya ishirini na moja wanaodinda kuolewa na wahubiri kwa hofu ya kutiwa pingu na dini licha ya kulelewa na jamii ya viongozi wa dini. Wao wangetaka kuwa huru kutafuta waume zao bila kulazimishwa na wazazi wao. Vijana Kushuku Uwezo wa Mungu. Kila binadamu duniani huamini kuwa kuna kiumbe mwenye nguvu na uwezo kumliko. Kiumbe huyu ndiye mpaji wa uhai na ndiye ajuaye uhai huenda wapi baada ya viumbe kufikwa na mauti. Jamii nyingi humpa kiumbe huyu majina tofauti ikiwemo Mungu, Maulana, Mola, RabanaKarima miongoni mwa majina mengine. Kiumbe huyu hudhaniwa na jamii ya mwanadamu kuwa na nguvu nyingi na uwezo wa kuamua hali ya baadaye na hatima ya mwanadamu huyu na hivyo mwanadamu humcha na kumheshimu mara nyingi. Kwa imani, kiumbe huyu hukimbiliwa hasa wakati kuna ugumu wa hali kwa imani kuwa ataleta suluhu na hali ya utulivu. Kwenye vitabu vitakatifu, Mungu hutajwa kama ngome ya kukimbiliwa wakati wa haja. Hata hivyo, vituko na kashfa miongoni mwa viongozi wa kidini kwenye madhehebu tofauti miaka ya hivi karibuni, zimefanya waumini wengi kushuku uwezo wa’ Mungu’ wa kubadili hali zikiwa na utata. Vile vile, matatizo yanayozidi kuongezeka kila uchao yakiwemo magonjwa, ajali, mauti na majanga ya kila siku yanazidi kufanya waumini wengi kushuku uwezo wa ‘Mungu’ wa kutuliza hali hizi. Vile vile, jamii inatarajia maombi na ibada zinazofanywa na waumini kila siku zifanye Mungu atulize hali ya mizozo iliyomo kwenye madhehebu mbalimbali. Ken Walibora katika riwaya yake ya KidagaaKimemwozea, anamrejelea kijana wa kike Imani ambaye anashuku uwezo wa Mungu aliyeruhusu kufikwa na dhiki iliyompata pale nyumbani aliponusurika kuchomwa na wenye wivu. Madai ya Amani yanadhihirika kwenye dondoo hii; IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 26 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA ‘Basiniliponusurikakuteketezwanilitokanikatazamambingunakuwazasana. KwaniniMungualiruhusudhikikamahiyokunikusa?’ (uk58-59) Maneno ya Imani ni kuwa Mungu mwenyewe hakuwa na uwezo wa kumlinda na hali ya maadui kutaka kumteketeza kwani hangekuwa na uwezo angemlinda kutokana na wahuni waliochoma nyumba yao na hangeruhusu wafike kwa boma lao. John habwe katika riwaya yake ya paradiso anamrejelea kijana wa kike lydia ambaye aliamini kuwa ana uwezo wa kufanya mambo mengi na kuwa mungu yuko tu anapokuwa hajiwezi. Haya yote yanajitokeza katika dondoo ifuatayo; ’’Lydia haya ya dini yalimfutu. Hakuyafuatilia kwa karibu. Angewezaje huku mama yake ndiye huyo? Au ni kweli walivyosema mwana huiga kisogo cha nina. Lydia alijua kuwa Mungu yuko anapokuwa hajiwezi. Pale unapoweza unayafanya mwenyewe’’(uk97) Utafiti huu unatambua kuwa kwenye mawazo ya Lydia ni kuwa Mungu anapaswa kuingililia kwa maisha ya mtu tu pale ambapo mtu huyo amelemewa na pale ambapo mtu huyo anaona anaweza basi anapaswa kujishughulikia. Yaani sio lazima mtu kutegemea Mungu kwa kila jambo. Vijana Kukataa ‘Kuokoka’ na Kuingia kwa Anasa. Kuokoka ni kitendo cha kutoka sehemu moja iliyo na hatari na kwenda sehemu nyingine ambayo ni salama. Kulingana na SamuelMtimbike (2022), kwa dini ya Kikristo, kuokoka ni kuitii injili ya Bwana Yesu na kisha kubatizwa katika ubatizo sahihi ambao ni wa maji mengi na kwa jina la Yesu na kupokea kipawa cha Roho mtakatifu na kisha kuishi maisha matakatifu kwa kufanya mapenzi ya Mungu. Kulingana na dini ya Kiisilamu, waliomkubali Mohamad na kufuata amri zake wamekwisha okoka na watapata Bustani zipitazo mito kati yake. Humo watadumu milele. Huku ndiko kufuzu kukubwa. Kulingana na mafundisho ya dini, wokovu ndio zawadi kubwa anayoweza kupata mwanadamu kwani inamhakikishia uzima wa milele Paradiso. Wokovu huu unahitaji kila muumini kuishi maisha ya utakatifu yasiyo na dhambi kulingana na mafundisho ya dini yake. Hata hivyo, jinsi siku zinavyosonga ndivyo waumini wengi na haswa vijana wanavyozidi kukaidi injili ya wokovu na badala yake kujiingiza kwenye ‘’dhambi’’ za kila aina zikiwemo ulevi, ukware, utovu wa maadili, anasa na starehe za kila aina kinyume na mafundisho ya dini zao. Kisa na maana, wanaowaongoza kwenye mafundisho haya ya kidini wanayatenda maovu haya wazi bila woga wa adhabu ya Muumba wao. Katika riwaya ya Paradiso, John Habwe anamrejelea kijana wa kike Nice bintiye Askofu Joshua na kasisi Lona aliyetoshwa na wokovu wa wazazi wake na kuzamia starehe zake za maisha kule NewYork. Salamu za Nice zililetwa nyumbani na Bwana Njenga aliyekutana naye kule NewYork katika shughuli zake za ukasisi. Bwana Njenga alipojaribu kumpa Nice habari za Yesu, Nice alimkumbusha kuwa baba yake ni mhubiri na kuwa hakuweza kumuokoa. Mwandishi anasema kuwa Nice alikuwa amejizika zii katika ulevi na matembezi. Ithibati ya utafiti huu imo katika nukuu ifuatayo ambayo ni mazungumzo ya Bwana Njenga na kijana wa kike Nice bintiye Askofu Joshua na Kasisi Lona; IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 27 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA ‘Nice alikuwa amesahau kisomo chake. Alijizika ziii katika ulevi na matembezi…. Well,nilitakakukuulizaunakaawapi? Unaa…YaaninilitakaumkubaliYesu’’…’’Sikiza. Babayangunimhubiri. Hakufaulukuniokoa. Wewehutafaulu. Ninakoishinanikifanyachoyakuhusuvipi?’’BaadayamjadalahuukatiyaNicenaBwanaNjenga, Nicealichomokanjebilakuaganasuruariyakeyakubanaambayokuivuakwakealikuwalazimaangesai diwa’. (uk128) Utafiti huu ulitambua kuwakijana wa kike Nice, alikuwa amechoshwa na ukosefu wa uaminifu kwa wazazi wake licha ya kuwa wao walikuwa watumishi wa Mungu na badala yake akazamia kuhamia NewYork alikoishi maisha ya ulevi na starehe alizotaka mwenyewe. Huu ndio uhuru alioutafuta maishani mbali za wazazi wake waliookoka. Vijana Kuzinduka na Kuuliza Maswali Kuhusu Dini Hadharani. Kuzinduka ni kitendo cha kutoka katika bumbuazi au kutoka katika hali ya kutoelewa jambo. Mtu yeyote anaweza kuzinduka kimawazo na kuwa na falsafa mpya kuliko aliyokuwa nayo hapo awali. Katika kipindi cha zama za giza, binadamu aliacha hali ya kimaumbile na jaala kuchukua mkondo wake bila kutia juhudi zozote za kudhibiti changamoto zilizotesa kiumbe huyu. Hata hivyo, baada ya kipindi cha ufufuo, binadamu alianza harakati za kujikomboa kutoka sirisiri za utumwa zilizomfunga kwa miaka nyingi zikiwemo zile za kidini, uchumi, teknolojia na ujinga wa kutosoma. Kiumbe huyu alianza kutafuta maarifa na ujuzi ambazo zingempunguzia taabu alizokubana nazo siku nenda siku rudi. Upande wa kidini, watu walifundishwa mafunzo na itikadi kali kwamba ili kumfikia Mungu ni lazima muumini yeyote apitie kwa Papamtakatifu. Kulingana na Ellen G. White (2023), mwanzo wa utawala wa KanisalaRumi ulikuwa mwanzo wa utawala wa giza na jinsi uwezo wa kanisa ulivyoogezeka ndivyo pia hali ya giza ilivyoongezeka. Anasema kuwa Imani ya wengi kuwa Yesu mwana wa Mungu ndiye mwazilishi wa kanisa iligeuzwa na badala yake papa na maasikofu aliowapa mamlaka kuadhimishwa. John Habwe kwenye riwaya yake ya Paradiso, anarejelea kiongozi wa kikundi cha vijana pale kwenye kanisa la Bethany lililoongozwa na kasisi Michael. Uhusiano wa Michael na Patricia na kukosa kuwa mwaminifu katika ndoa yake na Lydia, kuliwapa vijana nafasi ya kuzinduka na kuuliza hadharani kuhusu matumizi ya misaada iliyotoka ng’ambo na usimamizi wa nasari iliyokuwa chini ya kanisa jinsi inavyojitokeza kwenye nukuu iliyo hapa; ‘TayarimwanyauliingiaBethany. Kuna kikundi kilichoona hakikufaidi vizuri pale Bethany. Kikundi hiki kiliongozwa na Kariuki. Kariuki alikuwa kiongozi wa vijana kaika kanisa la Bethany. Kikundi cha vijana kilidaimisaadayoteiliyotokang’amboilikuwakatikamikonoyawachache. PiausimamiziwashuleyanasariyaBethanypiaulifaidiwachachesana. Ummamkubwauliodundulizakuijengahaupatichochote. Walimuwashuleyanasariwaliopaswakutokahumokanisanihawajuisikuhiziwanatokawapi?’ (uk153.) Utafiti huu unatambua kuwa vijana wa jana ni tofauti na wale wa sasa kwani wale wa sasa hawana woga tena na pindi waonapo jambo lenye utata wanalikashfu moja kwa moja. Ndio IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 28 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA maana Kariuki, kiongozi wa vijana katika kanisa la Bethany anaongoza vijana wenzake kuuliza maswali peupe bila woga wowote kinyume na ilivyokuwa hapo awali. Vijana Kuacha Kuhudhuria Ibada. Ibada ni kitendo chochote kinachofanywa kuonyesha unyenyekevu wa hali ya juu, utiifu, heshima, shukrani na utukufu aidha kwa Mungu au kitu kilicho na mamlaka makuu kuliko binadamu. Dini zote duniani huwa na ibada zinazofanyiwa mahala teule labda kwenye majengo ya kifahari au kachara, chini ya miti, mapangoni, juu ya miamba au hata misituni. Maabadi haya huheshimiwa na huwa muhari kila mmoja katika jamii ahudhurie ibada kulingana na muda na wakati uliotengwa. Hata hivyo, vijana wa karne ya ishirini na moja wamekuwa na mahudhurio duni ya ibada kwa tetesi kuwa matakwa yao hayatiliwi maanani na viongozi wa maabadi na haswa wazee. John Habwe katika riwaya yake ya Paradiso, anarejelea mahudhurio duni ya vijana katika kanisa la Bethany baada ya kiongozi wa kanisa hili Michael kupatikana na kashfa ya uhusiano wa nje ya ndoa na Patricia licha ya kuwa na mke wake mwanadini Lydia. Haya yanadhihirika katika maneno yafuatayo; ‘’JapobadokulikuwanawauminilukukiBethanyhasawalewaliofuatamiujiza, kundikubwalilinyofoanakujiondokea. Ahadizilipotolewabilamafanikiohapakuwanasababu yakuendeleakuning’iniaBethany.Kundilavijanatayarililijibambuakamagomelagogo.’’(uk160). Utafiti huu unadhibitisha madai kuwa vijana wanazidi kuchoshwa na masuala ya dini na wanazidi kuyakimbia na kujipa shughuli zao. Hii ni baada ya vijana hawa kutambua kuwa viongozi wa kidini wanaowaongoza wamejawa na kashfa chungu nzima. Wanaamua kujiondoa mmoja baada ya mwingine. Vijana Kuwa na Ukakamavu wa Kudharau Watumishi wa Mungu Peupe. Watumishi wa Mungu ni viongozi waliotwikwa mamlaka ya kuongoza ibada katika madhabau ya waumini. Kila dhehebu duniani huwa na viongozi wake wanaopaswa kuheshimiwa na kusikizwa kwani ndio hutwikwa jukumu la kufundisha mafunzo ya kidini kulingana na mila na itikadi za dini husika. Vile vile, watumishi hawa wa Mungu wanapaswa kujiheshimu na kuwa waangalifu kwa maneno na matendo yao kwani chochote wanachosema au kutenda hadharani hutiwa kwenye mizani na waumini walio chini yao. Hata hivyo, watumishi hawa wa Mungu wanazidi kujihusisha na vituko vya kila aina ikiwemo kulaghai waumini kwa jina la Mungu, kufanya miujiza bandia, kuwa na mipango ya kando na kashfa za pesa miongoni mwa kashfa zingine. Vituko vyao vinazidi kuwapunguzia heshima na kufanya waumini na haswa vijana waliozinduka kuwadharau hadharani. John Habwe katika riwaya yake ya Paradiso, anawarejelea vijana wanafunzi wa shule ya upili ya Alliance Girls wanaodharau mtumishi wa mungu na mke wake Michael, Lydia. Hii ni baada ya vijana hawa kughudua kuwa Patricia analea mimba ya mhubiri na mume wake mwalimu wao. Walianzisha dharau kwa mwalimu wao kwa kutupa vijikaratasi hapa na pale kukashfu vitendo vya mume wa mwalimu wao aliye mtumishi wa Mungu kwenye kanisa la Bethany. Idhibati ya dharau hili ipo kwenye dondoo ifuatayo; IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 29 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA ‘HatailipojulikanawazikuwaPatriciaanaleamimba, shulenzimahatawanafunziwalijua. Lydiaamebakiapalenarafikiwachache. Walimuwenginiwakumsengenyaakipita. Sasayeyeameamuaakaekando. KamahanajambolamnopaleshulenialikwendaBethanykusaidianakazi. Wanafunziwameandikavikaratasikusambazailikumkashfukuhusuvitendovyamumewe. LabdahilindilolililomtepuaLydiatenamoyowake. SasaaliposikiakuwaPatriciaamelazwaakaonawenzakewataendelezakashfanakumsemaovyoovyo.’ (uk204) Utafiti huu unakumbana na ukweli kuwa mtumishi wa Mungu na pia mwalimu Lydia anakumbana na hali nzito pale shuleni kwani hana uso wa kutazama wanafunzi hawa wanaosema ukweli wa jinsi hali ilivyo kuhusu ndoa yake na mume wake Michael. Anapunguza maneno yake na kuondoka shuleni pindi tu vipindi vyake vya masomo vinapokamilika. Vijana Kukataa Kazi ya Mungu Peupe. Kazi ya Mungu ni kitendo cha kutoa huduma iliyo au isiyo na malipo kufanya kazi ya Mungu. Kila dhehebu huwa na nafasi yake ya utumishi wa kazi ya Mungu kulingana na kanuni zao. Kwa yeyote kuwa na nafasi ya utumishi huu anapaswa kuwa na elimu fulani ya kithiolojia kulingana na kitengo ambacho angependa kuegemea. Ili kupata nafasi ya kutoa huduma husika ni lazima kufuata masharti fulani yaliyowekwa kulingana na kanuni za dhehebu husika. Katika karne ya 21, idadi ya vijana katika utumishi wa Mungu imepungua jambo ambalo linazidi kutia wazee na viongozi wa madhehebu kiwewe kila uchao. Tafiti na maandishi mengi kwenye masuala ya dini zinadhirihisha kuwa vijana wanazidi kukataa utumishi wa Mungu na kuwa washirika tu wasiodhibitiwa kikamilifu na dini. Ken Walibora katika riwaya yake ya KidagaaKimemwozea, anamrejelea kijana Mwalimu Majisifu Majimarefu aliyefadhiliwa na Misheni kwenda ng’ambo kusomea ukasisi ili kurithi viatu vya baba yake ya ukasisi. Majisifu anapoenda ng’ambo anaghairi mtazamo huu wa kazi ya Mungu na kuamua kuishi maisha yake yasiyo na uhusiano na kazi ya Mungu jinsi inavyojitokeza katika nukuu hapa chini; ‘Mwalimu majisifu alitarajiwa kusomea ukasisi ili aandame nyayo za babake. Lakini alipofika huko lipo lilimchusha akatoshwa na dini. Dini kwake ilikuwa kasumba iliyoulewesha umma ukalewa chakari na kupepesuka…. Aliona kwamba ingawa dini zote huhubiri Amani, udugu, na rehema, ila maovu na makuruhu mengi katika historia ya mwanadamu mathalan husuda, uongo, usongombwingo na vita yametendwa katika jina la Mungu. Kwa hivyo akaghairi nia ya kuwa kasisi’. (uk27). Utafiti huu unatambua kuwa ingawa watumishi wa Mungu wana nia nzuri ya kurithisha utumishi huu kwa watoto wao, kuna mambo nyeti yanayotinga hamu ya vijana hawa kuendeleza azma ya wazazi wao. Licha ya kuwa kasisi na baba yake Mwalimu Majisifu angetamani mtoto wake aiendeleze kazi ya Mungu kwa kufuata nyayo zake, kijana huyu alighairi nia hii kwa kutambua kuwa dini imejawa na unafiki mwingi na matendo mengi maovu yanafanyika kwa jina la Mungu. IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 30 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA Vijana Kutafuta Miungu na Ibada Zingine. Miungu ni jina linalojumlisha wahusika wanaoabudiwa katika dini mbalimbali kama wenye nguvu na enzi juu ya maisha ya mwanadamu. Tangu kipindi cha Neolithic, binadamu katika dunia wamekuwa wakifanya ibada za miungi tofauti kulingana na kipindi fulani cha mwaka. Kulikuwa na miungu ya wakati wa mavuno, wakati wa kiangazi, wakati wa mafuriko, baada ya majanga kutokea na kadhalika. Hata hivyo jinsi siku zilivyosonga ndivyo akili za waumini zilivyobadilika na kuelekeza ibada zao kwa Mungu mmoja kulingana na makubaliano. Kulingana na GasperMadumla (2014), jinsi dunia ilivyosonga ndivyo ongezeko la dhambi lilivyozidi na kumfanya mwanadamu kugeukia katika aina mbali mbali za ibada na hapo kukatengenezwa aina kubwa tatu za ibada ambazo ni; ibada kwa Mungu aliye hai, ibada kwa miungu ya jadi, mizimu, matambiko na mashetani na ibada kwa mwanadamu, vitu, fedha na mali. Katika karne ya 21, baadhi ya wanajamii na haswa vijana wamejikita katika uhuru wa kuabudu chochote watakavyo zikiwemo anasa na starehe zao. Waandishi tofauti wamekuwa wakiangazia waumini wanaoamua kuabudu vitu tofauti na kutumia mitindo tofauti ya maisha kulingana na matakwa yao. Ken Walibora kwenye riwaya yake ya KidagaaKimemwozea, anamrejelea Mwalimu Majisifu ambaye baada ya kuchoshwa na Mungu na ibada za maabadi aliamua kuwa na mungu wake ‘pombe’ na ibada yake ikawa ‘ulevi. Madai hayo yanajitokeza kwenye dondoo iliyo hapa; ‘‘…lakinihatimayealikuwamwalimutuwashuleyaupili. Nalauasingekuwanawanaomjuawenyesatua, asingalikuwahatanaualimuhuo. Mamboyakeyalikuwataibuhadialipoanzakuabudu ‘Mungu’mwinginekwahimdinatwaa. Pombeilikuwamunguwakenaulevindioibadaaliyoipendakwadhatiya moyo’’. (Uk28). Utafiti huu uling’amua kuwa hata baada ya kijana mwalimu majisifu kukua na kuoa mke wake Dora, alizidi tu na ibada yake bila hofu kwani aliamini kuwa huu ndio uhuru aliopaswa kuwa nao binadamu yeyote wa kuachiwa mwanya wa kufuata sera zake bila kuingililiwa na yeyote. Mwalimu Majisifu anakosa kuhudhuria mkutano wa kusherehekea uhuru wa taifa la Tomoko kwenye uwanja wa Sokomoko kisa na maana alikuwa ameenda ibada jinsi ilivyo kwenye maneno yafuatayo; ‘Majisifumbonasikukuonamkutanoni?’’ BwanaMtemialimuulizanduguyehatimayebaadayakimyachakitambokirefu…’’Nilikuwanimekwen daibadakaka.’’ ‘’Temboitakuuanduguyangu. Punguzaulevibwana. Unautukanishaukoowetumtukufu. Sikuhizihatanaonaaibukukuitanduguyangu. Niliambiwajanakwambaulilalamtaronisikuileyashereheusikukucha. Hiiniaibubwana. Kumbukamarehemubabayetualikuwakasisinduguyangu. Alikuwaakisemakwambawalevihawataingiakatikaufalmewambinguni’’ (uk93.) Utafiti huu ulitambua kuwa Mwalimu Majisifu alikuwa tayari akeshajitafutia ibada yake ya ulevi tangia ujanani wake licha ya baba yake kumtaka awe kasisi kama yeye. Hivyo basi akahasi Mungu na Ibada za babake na kufanya maamuzi kuwa pombe ndiyo mungu wake na ulevi ndio ibada yake daima. IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 31 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA Njia Mbadala ya Kukabiliana na hali hii ya Udhanaishi John Habwe na Ken Walibora wanapendekeza baadhi ya njia zinazoweza kutumika ili kujenga imani katika mioyo ya vijana kuhusu masuala ya dini kwa lengo la kupunguza ukataji wa tamaa unaojengekeka kwao kila uchao. Baadhi ya mapendekezo yaliyomlikwa na waandishi hawa ni pamoja na shughuli za ibada kuendeshwa kwa utaratibu wa pole pole na uungwana. katika riwaya ya Paradiso, baada ya mhubiri Michael kutoka Marekani, alifika na maoni kuwa shughuli za kanisa zilifaa kuendeshwa kwa utaratibu wa pole pole na uungwana bila kelele na kucheza kwingi kama kwamba leo dini ni disko. (uk 97-98) Pili ni kutumia maafisa wa polisi na askari kwenye sehemu za maabadi ili kutuliza ghasia zinapozuka miongoni mwa washirika. Hii ni kwa sababu uwepo wa maafisa hawa utawafanya vijana kuwa na imani kuwa wanaoazimia kuleta fujo kwenye sehemu hizi za maabadi watakuwa na hofu na hivyo kufanya ibada kwa utaratibu. Katika riwaya ya Paradiso, maafisa wa polisi wanafika kuzima fujo na kutenganisha vikundi vilivyokuwa vikipigana katika kanisa la NewJerusalemu ambapo watu kadhaa walikuwa wameumizwa kwenye vurumai zilizotokea. (uk77). Maafisa hawa hawa wa polisi ndio waliotumiwa kuchunguza kashfa ya biashara ya mihadarati na madini iliyoendeshwa katika kanisa la NewJerusalemu (uk 198). Vile vile, katika riwaya ya KidagaaKimemwozea, askari wa Mtemi Nasaba Bora wanalazimika kuzima ghasia zilizokuwa na vita baina ya makanisa mawili yaliyopigana kadamnasi sokoni juu ya uwanja wa kujenga maabadi ambapo kama haingekuwa askari hao wanamakundi hawa wangeuana waangamizane (uk 93). Njia ya tatu ni kutumia mahakama kutoa maamuzi ya ni wapi palipo na makosa vurugu zinapotokea. Katika riwaya ya Paradiso, ilibidi kanisa la NewJerusalemu kufungwa miezi minne kungojea mahakama kuamua ni nani anamiliki nini katika majengo ya maabadi(uk77). Mahakama pia inatumika kusikiza kesi kuhusu biashara ya ulanguzi wa mihadarati inayoongozwa na wa kanisa la mhubiri Boribori pale New Jerusalemu.Mahakama hii inatumika kumfunga Boribori na mkewe Judy kwa nia ya kusafisha magugu maabadani ili kujenga imani mpya kwa washiriki. (uk 217) Njia nyingine ya kujenga imani ya kidini miongoni mwa vijana ni kurekebisha tabia na mienendo ya washirika iwapo wangeendelea kumhubiri Bwana na kumfanyia kazi. katika riwaya ya Paradiso, Mhubiri Michael anasisitiza kuwa endapo wanaodai kuwa wameokoka wangejitayarisha katika ulimwengu kwa maisha ya ahera hawana budi kurekebisha na kubadili mienendo yao kwa kuhasi mauaji, ubakaji, wizi, ufisadi na kashfa zingine zilizoitanishwa na waumini la sivyo walio nje watazidi kuambaa masuala ya dini. (uk 56) Vile vile, waandishi hawa wanapendekeza kupunguza muda unaotumika kufanya ibada na kutumia lugha inayoeleweka na kila mwanaibada. Vijana wengi huchoshwa na muda mwingi unaotumika katika ibada haswa mahubiri. Kwenye riwaya ya Paradiso, mhubiri Michael wa kanisa la Bethany, alipunguza mahubiri yake kutoka saa moja hadi dakika kumi na tano. Anapoamua kutumia kiingereza, Bwana Kitwana huwa mkalimani wake ili kuwafikia watoto, wanawake, wanaume, vizee, wagonjwa na wazima walioujaa ukumbi wa Bethany. (uk 160) Pia, IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 32 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA wazazi wanapaswa kuwaasa watoto wao wakiwa wadogo na kuwaadilisha njia ambazo wangefuata ili kukua kwa uangalifu usioterereka. Hii ni kwa sababu mwalimu wa kwanza wa mtoto ni mzazi au mlezi wake na kuwa kwa asilimia pana mtoto hukua kulingana na mienendo ya mazingira aliyolelewa. Katika riwaya ya Paradiso, Patricia alikumbuka maneno alomweleza mamake Wanjiro alipopata mtoto wa pili. Patricia alionywa na mamake vikali dhidi ya kumvulia mtu yeyote nguo mpaka atakapoingia katika ndoa halali. Mama huyu alimfundisha bintiye kuwa asijipendekeze kwa mume yeyote kwani kujipendekeza kwa mwanamume ndiko kufukuzwa huko. (uk171-172) Mama huyu alimkumbusha bintiye kuwa yeye bado ni mtoto kwani hakuwa na uwezo wa kutenganisha haramu na halali. ‘Kwanguhutakuwamtumzima. Mtu mzima ni mimi mama yako niliyekuzaa na unayepagaza. Kama ungekuwa mtu mzima ungejua uharamu ulioko kutembea na mtu asiyekupenda akakutia mimba na kisha…’’ Wanjiro alighafilika kumaliza’. (uk176) Wosiakamahuu kwa vijana ungewaadilisha na kujenga misingi yao katika mafundisho ya kidini na hivyo basi kupunguza anasa, mipango ya kando na unafiki wa kidini miongoni mwa washirika na hivyo kuvutia vijana kwenye Imani yake. Viongozi wa kidini na wahubiri wanapaswa kubadilisha mkondo wa injili kutoka kwa matoleo ya kila siku na badala yake kuhubiri jinsi binadamu anapaswa kuishi na binadamu mwenzake. Hii ni kwa sababu pasipo na haki na umoja wa washirika hata maabadi yenyewe hayataweza kusimama imara. Katika riwaya ya Paradiso, baada ya Mchungaji Boribori kufungwa jela, Nana aliyechukua mahali pake aliweka mkondo mpya wa injili. Injili yake ilitoka kwenye ‘zaka na maendeleo’ hadi kwenye ‘kwenenda kwa haki na kupendana kwa majirani’. Kulingana na Nana, subira ilikuwa muhimu ili kupata ahadi za Bwana maanake Bwana Mungu alikuwa na saa yake na mikakati yake ya kufanyia mambo ambayo haikuwa lazima kwenda sambamba na ya wanadamu. Baadaye waumini walianza kuona ukweli katika injili ya Nana na baadhi ya waliokuwa wamegura walirejea na wageni kutoka ulimwengu na makanisa jirani wakaanza kufurika kwenye kanisa la NewJerusalemu. (uk 226) Hii ina maana kuwa waumini vijana wengi hukosa imani kwenye dini kutokana na matoleo ya mara kwa mara na endapo mkondo wa injili utabadilishwa watarejea maabadani kwa moyo wa dhati. Hitimisho Kulingana na utafiti uliofanywa ni ukweli usiofichika kuwa kuna masuala chungu nzima yanayofanya vijana watamaushwe na masuala ya kidini kila uchao. Kwa vile hamna lolote lisilo na athari zake, utamaushi huu una athari maridhawa kwa vijana hawa hali ambayo ikikosa kutafutiwa suluhu mwafaka itakuwa na athari mbaya kwa masuala ya ibada za siku za kesho.Mapendekezo yaliyo hapo juu yanaweza kutumika kupiga hatua kujitahidi kushughulikia kiwewe cha vijana kutamaushwa na mafundisho ya dini yanayojikita katika mafundisho ya maadili katika jamii. IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 33 IJO- INTERNATIONAL JOURNAL OF SOCIAL SCIENCE AND HUMANITIES RESEARCH ( ISSN 2811-2466 ) Jackline Njeri Murimi* https://ijojournals.com/ Volume 07 || Issue 05 || May, 2024 || ATHARI ZA UDHANAISHI WA KIDINI KWA VIJANA KATIKA RIWAYAZA PARADISO NA KIDAGAA KIMEMWOZEA MAREJELEO Camus, A(1984). The Rebel: Hamish Hamilton, Loudon. ------------(1961)Resistance, RebellionandDeath.Translated by Justin O’Brien. New York:Knopf Habwe, J. (2000). MaishaKitendawili.Nairobi.Jomo Kenyatta Foundation -------- (.2005).Paradiso.Nairobi; The Jomo Kenyatta Foundation. International Bible Society (1973). HolyBible:New International Version.New York. Katiba ya Kenya (2010).GovermentPrinters.Nairobi Makoyo,M.S. (2014). ‘‘A Critique of Christian Education for Self Reliance in Kenya i light of Existentialism’’.Tasnifu ya Uzamili. Chuo Kikuu cha Nairobi.(Haijachapishwa) Mbithi,J. (1969). .AfricanReligionsandPhilosophy.London:Heinman Education Books Ltd. Mohamed S.A. (1995). Amezidi. East African Educational publishers. Nairobi. Nkonge,G.(2006). “ Athari za Udhanaishi katika KichwaMaji na NguvuzaSala” Tasnifu ya Uzamili, Chuo Kikuu cha Nairobi( Haijachapishwa) Nyamemba,(2012).‘Uchanganuzi Linganishi wa jinsi waandishi katika TunuyaUshairi wanavyoshughulikia masuala ya vijana” Tasnifu ya Uzamili ,Chuo Kikuu cha Nairobi ( Haijachapishwa) TUKI, (2012). Kamusi ya Kiswahili Sanifu (Toleo la 3)Nairobi. Oxford University. Walibora,K .(.2012). KidagaaKimemwozea,Nairobi;Target Publication Limited ----------------(2006). KufaKuzikana .Nai robi;Target Publications IJO JOURNALS Volume 07 | Issue 05 | May 2024 | https://ijojournals.com/index.php/ssh/index 34 IKISIRI Utangulizi Yaliyoandikwa Kuhusu Mada Muhtasari wa Riwaya ya Paradiso Muhtasari wa Riwaya ya KidagaaKimemwozea Athari za Udhanaishi wa Kidini kwa Vijana Vijana Kuchoshwa na Utaratibu wa Maabadani. Vijana wa Kike Kukataa Kuolewa na Wahubiri. Vijana Kushuku Uwezo wa Mungu. Vijana Kukataa ‘Kuokoka’ na Kuingia kwa Anasa. Vijana Kuzinduka na Kuuliza Maswali Kuhusu Dini Hadharani. Vijana Kuacha Kuhudhuria Ibada. Vijana Kuwa na Ukakamavu wa Kudharau Watumishi wa Mungu Peupe. Vijana Kutafuta Miungu na Ibada Zingine. Njia Mbadala ya Kukabiliana na hali hii ya Udhanaishi Hitimisho MAREJELEO